Habar zenu wakuu ,
Ni mda sasa sjaleta uzi humu jukwaani tangia nifunge pingu za maisha na mwanamke wa ndoto zangu ila leo kidoog nimeona nije na hili
Nilileta uzi humu miezi minne iliopita kwamba nimemuowa mwanamke wa ndoto zangu
Kiukwel safar ya kuowa kwangu haikua rahisi , kwani kila mtu alijua nimekurupuka kwakua skua ninetimiza hata mwaka toka nianze kupata mishe na kua napata angalau risk yangu ya halali
Wengi walinibeza na kukataa kata kata kunipa ushirikiano ila hatimae leo nimekamilisha adhma yangu na nafurahis maisha haya matamu ya ndoa
Japo wengi mtasema safar bdo ndo kwanza nakula honeymoon ila waswahil wanasema nyota njema inaonekana asubuh
Kwa wale walionibeza wanafikia kuomba mualiko kuja kwangu , wengine wanaleta tu watoto wao angalau wakae kwangu sku mbili tatu
Wengine wananipiga virungu kila leo
Ushauri kwa vijana wenzangu kama una wazo la kuowa na unahis umepata mwanamke sahihi kwako ambae mnapendana kwel kwel asa basi challenge za watu kukutoa moyo tupa pembeni wewe pigana na muombe mungu akufanikishe
Laiti ningeskiliza kelele za chura hadi leo maji yangenishinda kunywa
Nafrahia maisha na wife hata bajet yangu imeimarika tofaut na kipind cha ubachela
Namalizia :Ndoa tamu sna askwambie mtu iwapo utapata mtu sahihi akakupenda kwel nawe ukampenda na akawa muelewa na kukubaliana na hali yako