Asikuambie mtu kuoa ni raha

Asikuambie mtu kuoa ni raha

colin_morgan

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,443
Reaction score
2,929
Habari zenu wakuu,

Ni mda sasa sijaleta uzi humu jukwaani tangia nifunge pingu za maisha na mwanamke wa ndoto zangu ila leo kidogo nimeona nije na hili.

Nilileta uzi humu miezi minne iliopita kwamba nimemuoa mwanamke wa ndoto zangu.

Kiukweli safari ya kuoa kwangu haikua rahisi, kwani kila mtu alijua nimekurupuka kwakua sikua ninetimiza hata mwaka toka nianze kupata mishe na kua napata angalau risk yangu ya halali.

Wengi walinibeza na kukataa kata kata kunipa ushirikiano ila hatimae leo nimekamilisha adhma yangu na nafurahi maisha haya matamu ya ndoa.

Japo wengi mtasema safari bado ndo kwanza nakula honeymoon ila waswahili wanasema nyota njema inaonekana asubuhi.

Kwa wale walionibeza wanafikia kuomba mualiko kuja kwangu, wengine wanaleta tu watoto wao angalau wakae kwangu siku mbili tatu.

Wengine wananipiga virungu kila leo.

Ushauri kwa vijana wenzangu kama una wazo la kuoa na unahisi umepata mwanamke sahihi kwako ambae mnapendana kweli kweli sasa basi challenge za watu kukutoa moyo tupa pembeni wewe pigana na muombe Mungu akufanikishe.

Laiti ningesikiliza kelele za chura hadi leo maji yangenishinda kunywa.

Nafurahia maisha na mke hata bajeti yangu imeimarika tofauti na kipindi cha ubachela.

Namalizia: Ndoa tamu sana asikwambie mtu iwapo utapata mtu sahihi akakupenda kweli nawe ukampenda na akawa muelewa na kukubaliana na hali yako.
 
Ukishachapiwa ndio utajua kuwa ni bora uchapiwe demu kuliko kuchapiwa mke..

na ndio hapo utaukumbuka ule msemo wa kuchapiwa ni siri ya ndani

mimi bado nipo sana chama la bachela hadi nipewe uenyekiti ... kamwe sitakuja saliti hili chama
 
hongera mkuu ila uwe unakubaliana na hali halisi za changamoto... umeepuka uzinzi safi... mimi sijui nitaoa lini kwa kweli watoto wazuri kila nikikatiza mitaa kila aina dah Muumba anitie nguvu nifikie kama wewe...
 
BADO ZAWADI & PESA ZA HARUSI HAZIJAISHA. Miezi minne unafurahi, wengine angalau huanza na mwaka kufurahia hiyo kitu, ungetulia kidogo mkuu maana kuna watu wapo ICU ya nyumbani kwenye mambo ya ndoa
 
Mkuu haujui utamu wa ndoa
Yaan unapikiwa chakula kitamu , unafanyiwa everything yaan we acha tu

Ukitoka shart kwanza uwekwe smart

Yaan sjui ata niongeeje ila owa mkuu ujionee mambo mengine si yakuyaanika mtandaoni
 
hongera mkuu ila uwe unakubaliana na hali halisi za changamoto... umeepuka uzinzi safi... mimi sijui nitaoa lini kwa kweli watoto wazuri kila nikikatiza mitaa kila aina dah Muumba anitie nguvu nifikie kama wewe...
Ameen mkuu
Mungu atakujaalia pia

Sku akitokea right someone 4 u hautoambiwa na mtu mwenyewe utaitaka ndoa mithili ya chizi
 
BADO ZAWADI & PESA ZA HARUSI HAZIJAISHA. Miezi minne unafurahi, wengine angalau huanza na mwaka kufurahia hiyo kitu, ungetulia kidogo mkuu maana kuna watu wapo ICU ya nyumbani kwenye mambo ya ndoa
Mkuu sikupewa mchango hata mia

Nikama vile niliibeba dunia mgongon nimemaliza ndoa sina shilling hapa ndo naanza kujiweka sawa upyaaa
 
Back
Top Bottom