Gwiji wa Siasa Tanzania na Katibu Mkuu CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amefurahishwa na ukarimu wa watu wa Kigoma tangia aanze ziara ya kichama mkoani humo.
Akizungumza katika Baraza la Uongozi la Mkoa wa Kigoma kiongozi huyo wa kisiasa nchini alisema watu wa Kigoma wameonyesha mshikamano mkubwa na kupambana na wahuni wote waliokuwa wameagizwa kuvuruga ziara yake.
Kauli hiyo ya Dr Slaa inafuatia wahuni na wavuta bangi kujaribu kuvuruga mikutano yake lakini nguvu ya UMMA ilidhibiti hujuma hizo.
Wiki iliyopita watu walionyweshwa gongo na wengine walevi wa bangi waliandamana Kigoma mjini kulaani ujio wa Dr Slaa na kujiapiza endapo kama kiongozi huyo angekanyaga Kigoma mjini wangemdhuru.
Hata hivyo Dr Slaa aliingia Kigoma mjini kwa Kishindo kikubwa na kulakiwa na msururu wa magari na Pikipiki huku umati ukijipanga kandokando ya barabara na kupeperusha majani ya miti.
Kutokana na ujasiri wa Dr Slaa kupuuza vitisho vya wahuni hao baadhi ya watu wa Kigoma wamempachika jina la SIMBA WA TANZANIA.
..
....Kamanda Molemo ukimwona Sixgate huko msalimie!!!
uhuni ni kama dawa ya kutuliza maumivu.sio tiba.
Dr Slaa ni Jasiri na ana uwezo mkubwa sana... Hawa ndiyo aina ya viongozi wanaotakiwa Tanzania hii na tunashukuru hii Ziara imeyafunga midoma Magazeti yanayotumika vibaya kama Mwananchi, Habari Leo Uhuru na RAI.
Big up Dr Slaa Rais Mtarajiwa 2015, tumeshashinda mtego mwingine wa kukukwamisha usigombee tena.
Mimi kama mwanachama halili wa Chadema ninayeifahamu Katiba ya Chadema na ninayeheshi maamuzi ya Viakao halali vya Chama sioni umuhimu wa kubadili Uongozi wa juu wa Chama mpaka 2016 tutakapokuwa na serikali ya Chadema Tanzania.
VIVA CHADEMA VIVA!!!!!!!!!!!!!!!!!
Peoples Power... Hakuna kulala mpaka kielweke, Chadema ni mpango wa Mungu.
..
....Kamanda Molemo ukimwona Sixgate huko msalimie!!!