Asante!!!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,806
59,285
Nadhani baadhi yetu kama sio wengi tunajua nguvu ya neno asante na umuhimu wa kushukuru pale mtu/watu wengine wanapokua wamejituma, jitolea kwaajili yetu.Kwa kushukuru mtu anapokuwia mkarimu inafanya kesho awe tayari kuwa mkarimu tena mwako, kwakushukuru pale mtu anapokua amejituma/jitahidi kufanya kitu kwaajili yako kunafanya huyo mtu aongeze juhudi. Kinyume cha hapo ndio unakuta mtu anafanya na kulipua kitu kwasababu analazimika na ingekua uamuzi wake asingefanya kabisa.

Mimi nimewahi kukutana na watu ambao hata kusema asante kwa chakula hawajui au sijui niseme hawawezi.Mimi niliwashangaa kwa kutokushukuru na wao walinishangaa kwa kuuliza mbona hawashukuru, ila baada ya kuwaeleza kwanini nadhani ni muhimu kufanya hivyo wakanielewa na kuanza kulitumia neno "ASANTE" ipasavyo.

Je wewe kama wewe mara mwisho umemwambia dada wa kazi, mzazi wako, mwenzi wako asante baada ya kula ni lini?
Mara ya mwisho kumwambia mtu asante baada ya kutekeleza kitu chochote kile ulichomwomba/mwagiza afanye ni lini?
Mara ya mwisho umemshukuru hata mpishi/mhudumu wa hoteli au mgahawa ni lini?
Mara ya mwisho kumshukuru mwenzi wako kwa kuwa na wewe bega kwa bega ni lini?
Mara ya mwisho kumshukuru dada wa kazi kwa kukulelea mwana/wanao ilikua lini?
Mara ya mwisho kumshukuru mtu yeyote yule kwa sababu yoyote ile ni lini?

Kama hukumbuki au ilikua muda mrefu sana badilika.Hata mtu unaemlipa anastahili asante kwasababu angeweza kufanya anachofanya kwa kulipua pamoja na kwamba unamlipa.Jifunze kushukuru uwape watu morale ya kuendelea kukusaidia na kukutumikia kikamilifu, pia raha ya kuwa karibu nawe.

Jumatatu njema.
 
Mimi huwa natoa shukrani popote paleninopokuwa nimefanyiwa jambo zuri na mtu
mimi asante yangu ya mwisho imeenda kwa my nephew leo asubuhi kwa kuninyooshea suruali maana mkono wangu wa kushoto umeumia haufanyi kazi
 
ahsante kubwa nimepewa leo alfajiri na mama Kayai,you can imagine ilikuwa ni ya nini............hahahhaaa.....hao ndo masenks bana!!
 
Mimi huwa natoa shukrani popote paleninopokuwa nimefanyiwa jambo zuri na mtu
mimi asante yangu ya mwisho imeenda kwa my nephew leo asubuhi kwa kuninyooshea suruali maana mkono wangu wa kushoto umeumia haufanyi kazi

Hapo hata siku ukiwa huumwi anaweza kujitolea kukupasia tena.
 
Mie hii nimeipenda sana,
Hakika namshukuru mungu kwa kuniwezesha kuwa na shukuran na hata kuwashukuru wengine,
Asante yangu nimeitoa mda si mrefu msaidizi wetu wa oficin alipoenda kunichukulia lunch.
 
ahsante kubwa nimepewa leo alfajiri na mama Kayai,you can imagine ilikuwa ni ya nini............hahahhaaa.....hao ndo masenks bana!

Ona ulivyofurahi.
Iwe ya maneno ya matendo asante inamwonyesha mtu kwamba unam
-appreciate.
 
Mie hii nimeipenda sana,
Hakika namshukuru mungu kwa kuniwezesha kuwa na shukuran na hata kuwashukuru wengine,
Asante yangu nimeitoa mda si mrefu msaidizi wetu wa oficin alipoenda kunichukulia lunch.
Endelea hivyo hivyo mwaya siku moja asije akajifanya haelekei huko au hata akatemea chakula chako mate akilazimika kukuletea.
 
Mara nyingi huwa naitoa kwa mpendwa wangu na yeye sio mchoyo huwa ananipa asante kwa mambo mengi
Iwe ni asante ya maneno au ya matenzo zaidi
Ila ni neno zuri sana kulisikia na kuambiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom