Asante sana Mr. Abdul Nondo kwa kuleta maajabu ya aina yake

Muda ni Tabibu Mujarabu. Wacha niendelee kusubir
 
1. Mwanafunzi wa chuo kikuu ambaye amejiunga kwa kufuata hatua zote, maombi yake kujiunga chuo yamepita idara kadhaa za serikali leo Uraia wake una utata. Hii inaitwa HUJAFA HUJAUMBIKA

2. Mr Nondo kabla ya sakata la kutekwa sorry kujiteka alikuwa chuo anasoma vizuri , anasafiri kwenda sehemu kadhaa nchini, anafanya shughuli za kiraia nchini huku akipishana na Mamlaka husika. Hii inaitwa NIGUSE BAHATI MBAYA NIKULIPUE MAKUSUDI.

3. Mr Nondo anapaswa kupeleka uhamiaji documents ambazo hata viongozi wakubwa wakiambiwa wapeleke kukiri uraia wao hawana . Hii inaitwa BINADAMU WOTE NI SAWA LAKINI WENGINE NI MUHIMU ZAIDI.

4. Taarifa zinaonesha babu yake Abdu Nondo yaani mzee Nondo alikuwa sehemu ya waasisi wa TANU lakini mjukuu uraia wake una mashaka unapaswa kuthibitiwa. Hii inaita MBWA ANAWEZA KUZAA PAKA.

5. Mr Nondo alikuwa mtu wa kawaida sana alifahamika kwa watu wachache mno kiasi angepuuzwa kwa kujiteka kwake leo habari zake ingekuwa historia tu sasa kila sehemu Nondo Nondo Nondo . Hii inaitwa HASIRA FAIDISHI.

6. Kwa kawaida chuo kikuu kuna wanafunzi wa kigeni ( Sio Raia watanzania) na wanafunzi wazawa ( Raia wa Tanzania ) Mr Nondo akiwa na uraia wenye utata amekuwa mnufaika wa mahitaji ya wanafunzi wazawa chuo kikuu mpaka alipojiteka. Hii inaitwa USINGIZI MZITO KWA UTAWALA WA CHUO.

7. Mr Nondo ni mtu maarufu sasa kuna watu wengi mno wenye kupaza sauti kisa Nondo ,wapo wanasiasa maarufu wa kusema kwa niaba ya Nondo, vipi Mr Nondo mwanakijiji ambaye yupo kule kigoma ndani kabisa ambaye hata kiswahili hawezi vyema. Hii inaitwa MACHOZI YA SAMAKI MAJINI.

8. Mpaka sasa kila mtanzania mwenye uwezo wa kupata habari amejuzwa uraia wa Mr Nondo una madoa unapaswa kuthibitishwa kwa documents. Vipi ikitokea documents na ushahidi mwingine kuonesha ni mtanzania hili doa atafutwa. Hii inaitwa MKUBWA HAKOSEI.

9. Kwa kuwa utata wa Uraia wa Mr Nondo unagusa idara nyingi chuo kikuu anaposoma kama mzawa, usajili alipopata cheti cha kuzaliwa kama mzawa ( chuo huwezi kujiunga bila birth certificate), shule alisoma primary, o level na a level ( kama alisoma Tanzania) na idara nyingi vipi mpaka sasa wamechukuliwa hatua. Hii inaitwa UTATA UTATANI.

10. Kama ulishangazwa na Uraia wa Jenerali Ulimwengu miaka ile , ukashtushwa na Uraia wa Hussein Bashe mwaka 2010 , unahuzunishwa na Uraia wa Mr Nondo subiri zamu yako itafika.

Katika vitu ambavyo vinaweza kuondoa umoja wetu ni kubaguana kwa namna yeyote, Tanzania ya mzee wetu Mwl Nyerere ni moja yenye kuheshimu kila mtu hata akiwa mkosefu kiasi gani bado utanzania inakuwa haki yake .

Pamoja na changamoto tulizonazo mioyo ya watanzania bado ina matumaini kwa gharama yeyote tunapaswa kulinda matumaini ya watanzania maana ndiyo umoja wetu ,upendo wetu ,ukarimu wetu na uvumilivu wetu .

Tanzania, Tanzania , Tanzania nakupenda nchi yangu , nakupenda kwa moyo wangu wote .

Copy and Paste from LAMU ELIZAYO PASCAL KILIMBA
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331
Asubiri zamu ya TRA na NSSF kuona kama alikuwa akilipa kodi na kuwasilisha michango ya baraza lake.
 
si kwa hilo toto tundu lilolotaka kufanya ujinga na masikhara katika nchini,eti ni msomi wa chuo kikuu UDSM,hivi kweli UDSM imekuwa mbovu kiasi hiki hata kupelekea kudahili vituko kama huyo dogo anayepambwa na watu wale?
Unajiita akili tatu wakati hata nusu huna
 
Wenye uraia usio na shaka hapa Tz wapo sana sana watatu Mkulu, Hpolepole, Bashite
[emoji54][emoji54][emoji54][emoji54][emoji54][emoji54]
Na kweli hao ndiyo RAIA daraja la kwanza wengine wote hatuaminiki
 
Yote hayo hayaondoi haki ya Uhamiaji kuuliza uraia wa mtu yeyote wakati wowote, ni wajibu wao ambao wamepewa kisheria.
9. Kwa kuwa utata wa Uraia wa Mr Nondo unagusa idara nyingi chuo kikuu anaposoma kama mzawa, usajili alipopata cheti cha kuzaliwa kama mzawa ( chuo huwezi kujiunga bila birth certificate), shule alisoma primary, o level na a level ( kama alisoma Tanzania) na idara nyingi vipi mpaka sasa wamechukuliwa hatua. Hii inaitwa UTATA UTATANI.
 
Mtu yeyote katika nchi hii akionekana ni mkosoaji wa serikali hubambikiwa na vitu vingi kama vile siyo raia halali au mkwepa kodi. Watawala wanadhani wakosoaji wengi sio raia wa nchi hii kweli tutafika?Nafia Africa#
 
Nani kakudanganya?

9. Kwa kuwa utata wa Uraia wa Mr Nondo unagusa idara nyingi chuo kikuu anaposoma kama mzawa, usajili alipopata cheti cha kuzaliwa kama mzawa ( chuo huwezi kujiunga bila birth certificate), shule alisoma primary, o level na a level ( kama alisoma Tanzania) na idara nyingi vipi mpaka sasa wamechukuliwa hatua. Hii inaitwa UTATA UTATANI.
 
kuna akati nahisi hizi story zinatengenezwa kutupotezesha kwenye mrengo fulani

mara Dr Shika, mara Mange Kimambi, mara huyu sasa Abdul Nondo

KWELI????
 
Hivi mtu mzima kupoteza muda wake kuandika maelezo marefu kama haya ni kuonyesha huna kazi ya kufanya na Rais wa nchi amesema tufanye kazi. Sasa wewe kazi yako kutunga mambo ya umbea mareeeefu JF halafu unalalamika ajira hamna. Huu ni ukichaa, acheni siasa za majitaka fanyeni kazi. Kama hamna mambo ya kuongelea ya maana yenye tija kwa taifa na huna kazi ya kufanya kaokote basi haya taka mjini jiji liwe safi.
 
Hii awamu ya sasa bila kutumia roho mbaya haitafika mahali maana hawana hoja ya msingi
 
Kivipi mkuu?
Mkuu ukiniuliza kivipi utakuwa unanionea tu! Ukimwuliza mkulu anaweza kukujibu in detail kuna uhusiano gani Nondo kuwekwa ndani na maendeleo ya viwanda au kununua upinzani/kuua upinzani na uchumi wa viwanda.
 
kuna akati nahisi hizi story zinatengenezwa kutupotezesha kwenye mrengo fulani

mara Dr Shika, mara Mange Kimambi, mara huyu sasa Abdul Nondo

KWELI????
Mkuu unatokea Kijiji gani au pori gani kiasi kwamba hata hizi taarifa hauko familia nazo? So sad
 
1. Mwanafunzi wa chuo kikuu ambaye amejiunga kwa kufuata hatua zote, maombi yake kujiunga chuo yamepita idara kadhaa za serikali leo Uraia wake una utata. Hii inaitwa HUJAFA HUJAUMBIKA

2. Mr Nondo kabla ya sakata la kutekwa sorry kujiteka alikuwa chuo anasoma vizuri , anasafiri kwenda sehemu kadhaa nchini, anafanya shughuli za kiraia nchini huku akipishana na Mamlaka husika. Hii inaitwa NIGUSE BAHATI MBAYA NIKULIPUE MAKUSUDI.

3. Mr Nondo anapaswa kupeleka uhamiaji documents ambazo hata viongozi wakubwa wakiambiwa wapeleke kukiri uraia wao hawana . Hii inaitwa BINADAMU WOTE NI SAWA LAKINI WENGINE NI MUHIMU ZAIDI.

4. Taarifa zinaonesha babu yake Abdu Nondo yaani mzee Nondo alikuwa sehemu ya waasisi wa TANU lakini mjukuu uraia wake una mashaka unapaswa kuthibitiwa. Hii inaita MBWA ANAWEZA KUZAA PAKA.

5. Mr Nondo alikuwa mtu wa kawaida sana alifahamika kwa watu wachache mno kiasi angepuuzwa kwa kujiteka kwake leo habari zake ingekuwa historia tu sasa kila sehemu Nondo Nondo Nondo . Hii inaitwa HASIRA FAIDISHI.

6. Kwa kawaida chuo kikuu kuna wanafunzi wa kigeni ( Sio Raia watanzania) na wanafunzi wazawa ( Raia wa Tanzania ) Mr Nondo akiwa na uraia wenye utata amekuwa mnufaika wa mahitaji ya wanafunzi wazawa chuo kikuu mpaka alipojiteka. Hii inaitwa USINGIZI MZITO KWA UTAWALA WA CHUO.

7. Mr Nondo ni mtu maarufu sasa kuna watu wengi mno wenye kupaza sauti kisa Nondo ,wapo wanasiasa maarufu wa kusema kwa niaba ya Nondo, vipi Mr Nondo mwanakijiji ambaye yupo kule kigoma ndani kabisa ambaye hata kiswahili hawezi vyema. Hii inaitwa MACHOZI YA SAMAKI MAJINI.

8. Mpaka sasa kila mtanzania mwenye uwezo wa kupata habari amejuzwa uraia wa Mr Nondo una madoa unapaswa kuthibitishwa kwa documents. Vipi ikitokea documents na ushahidi mwingine kuonesha ni mtanzania hili doa atafutwa. Hii inaitwa MKUBWA HAKOSEI.

9. Kwa kuwa utata wa Uraia wa Mr Nondo unagusa idara nyingi chuo kikuu anaposoma kama mzawa, usajili alipopata cheti cha kuzaliwa kama mzawa ( chuo huwezi kujiunga bila birth certificate), shule alisoma primary, o level na a level ( kama alisoma Tanzania) na idara nyingi vipi mpaka sasa wamechukuliwa hatua. Hii inaitwa UTATA UTATANI.

10. Kama ulishangazwa na Uraia wa Jenerali Ulimwengu miaka ile , ukashtushwa na Uraia wa Hussein Bashe mwaka 2010 , unahuzunishwa na Uraia wa Mr Nondo subiri zamu yako itafika.

Katika vitu ambavyo vinaweza kuondoa umoja wetu ni kubaguana kwa namna yeyote, Tanzania ya mzee wetu Mwl Nyerere ni moja yenye kuheshimu kila mtu hata akiwa mkosefu kiasi gani bado utanzania inakuwa haki yake .

Pamoja na changamoto tulizonazo mioyo ya watanzania bado ina matumaini kwa gharama yeyote tunapaswa kulinda matumaini ya watanzania maana ndiyo umoja wetu ,upendo wetu ,ukarimu wetu na uvumilivu wetu .

Tanzania, Tanzania , Tanzania nakupenda nchi yangu , nakupenda kwa moyo wangu wote .

Copy and Paste from LAMU ELIZAYO PASCAL KILIMBA
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331
Kwenye hili la uraia tuanze na SIZONJE aliingiaje tanzania
 
Yote hayo hayaondoi haki ya Uhamiaji kuuliza uraia wa mtu yeyote wakati wowote, ni wajibu wao ambao wamepewa kisheria.

Ukitafuta sana utaona hata mkapa naye si raia wa tanzania. pengine katoka kwenye vijiji vya mpakani na msumbiji au mkuu wa kaya naye si araia. Sasa ujinga huu wa kiwango cha PhD lazima ukome. Tanzania badala ya kwenda mbele tunarudiu nyuma kwa kasi ya ajabu na ya kipumbavu. Hiyo bdo serikali tuliyonayo ya kuhoji wewe umetoka wapi? babu zako wametoka nchi gani? hatuwezi kujenga viwanda kwa ujinga na ubaradhauli huu. ulimbukeni umeikumba Tz. Loo.
 
Back
Top Bottom