Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 3,032
- 8,383
1. Mwanafunzi wa chuo kikuu ambaye amejiunga kwa kufuata hatua zote, maombi yake kujiunga chuo yamepita idara kadhaa za serikali leo Uraia wake una utata. Hii inaitwa HUJAFA HUJAUMBIKA
2. Mr Nondo kabla ya sakata la kutekwa sorry kujiteka alikuwa chuo anasoma vizuri , anasafiri kwenda sehemu kadhaa nchini, anafanya shughuli za kiraia nchini huku akipishana na Mamlaka husika. Hii inaitwa NIGUSE BAHATI MBAYA NIKULIPUE MAKUSUDI.
3. Mr Nondo anapaswa kupeleka uhamiaji documents ambazo hata viongozi wakubwa wakiambiwa wapeleke kukiri uraia wao hawana . Hii inaitwa BINADAMU WOTE NI SAWA LAKINI WENGINE NI MUHIMU ZAIDI.
4. Taarifa zinaonesha babu yake Abdu Nondo yaani mzee Nondo alikuwa sehemu ya waasisi wa TANU lakini mjukuu uraia wake una mashaka unapaswa kuthibitiwa. Hii inaita MBWA ANAWEZA KUZAA PAKA.
5. Mr Nondo alikuwa mtu wa kawaida sana alifahamika kwa watu wachache mno kiasi angepuuzwa kwa kujiteka kwake leo habari zake ingekuwa historia tu sasa kila sehemu Nondo Nondo Nondo . Hii inaitwa HASIRA FAIDISHI.
6. Kwa kawaida chuo kikuu kuna wanafunzi wa kigeni ( Sio Raia watanzania) na wanafunzi wazawa ( Raia wa Tanzania ) Mr Nondo akiwa na uraia wenye utata amekuwa mnufaika wa mahitaji ya wanafunzi wazawa chuo kikuu mpaka alipojiteka. Hii inaitwa USINGIZI MZITO KWA UTAWALA WA CHUO.
7. Mr Nondo ni mtu maarufu sasa kuna watu wengi mno wenye kupaza sauti kisa Nondo ,wapo wanasiasa maarufu wa kusema kwa niaba ya Nondo, vipi Mr Nondo mwanakijiji ambaye yupo kule kigoma ndani kabisa ambaye hata kiswahili hawezi vyema. Hii inaitwa MACHOZI YA SAMAKI MAJINI.
8. Mpaka sasa kila mtanzania mwenye uwezo wa kupata habari amejuzwa uraia wa Mr Nondo una madoa unapaswa kuthibitishwa kwa documents. Vipi ikitokea documents na ushahidi mwingine kuonesha ni mtanzania hili doa atafutwa. Hii inaitwa MKUBWA HAKOSEI.
9. Kwa kuwa utata wa Uraia wa Mr Nondo unagusa idara nyingi chuo kikuu anaposoma kama mzawa, usajili alipopata cheti cha kuzaliwa kama mzawa ( chuo huwezi kujiunga bila birth certificate), shule alisoma primary, o level na a level ( kama alisoma Tanzania) na idara nyingi vipi mpaka sasa wamechukuliwa hatua. Hii inaitwa UTATA UTATANI.
10. Kama ulishangazwa na Uraia wa Jenerali Ulimwengu miaka ile , ukashtushwa na Uraia wa Hussein Bashe mwaka 2010 , unahuzunishwa na Uraia wa Mr Nondo subiri zamu yako itafika.
Katika vitu ambavyo vinaweza kuondoa umoja wetu ni kubaguana kwa namna yeyote, Tanzania ya mzee wetu Mwl Nyerere ni moja yenye kuheshimu kila mtu hata akiwa mkosefu kiasi gani bado utanzania inakuwa haki yake .
Pamoja na changamoto tulizonazo mioyo ya watanzania bado ina matumaini kwa gharama yeyote tunapaswa kulinda matumaini ya watanzania maana ndiyo umoja wetu ,upendo wetu ,ukarimu wetu na uvumilivu wetu .
Tanzania, Tanzania , Tanzania nakupenda nchi yangu , nakupenda kwa moyo wangu wote .
Copy and Paste from LAMU ELIZAYO PASCAL KILIMBA
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331