Hata usilie wala kujilaumu my dear. Hivi huyo aliyekuacha kisa tu kasikia maneno ya uongo na hajapata hata proof ukute, ndo angekuoa ingekuwaje sasa? Si angekuja akutelekeze ndani ya ndoa kisa maneno ya watu. Mtu asiyekuamini na hana msimamo, hastahili kuna na wewe kamwe. Tupa kuleee hao wote.
Ila ukipata mtu mwingine nafikiri mueleze mapema kuwa kuna dume-jike nililiacha linaniganda na maneno ya uongo. Afu nimegundua kitu, watu wanaoachwaga kwa makosa yao, ndo huwa wanajifanya wana visasi vya kipuuzi sana. Na ndo hao hao wakiulizwa kwa nini umeachana na fulani, basi atakavyomkandia huyo ex khaa kujisafisha tu mfyuuu. Mungu yupo nawe my dear, atakutetea tu dhidi ya huyo mzandiki.