Asante Mh. Mbowe!

Asante Mh. Mbowe!

Alisema "Utanikana mara tatu kabla jogoo hajawika". sasa kumbe mnategemea nini zaidi ya hilo (Traitor never change= Judas Iscariot).
 
Mbowe nakukumbusha kwenye kama wewe ni jasiri ongelea ufisadi tena tuone,

Kamuulize yule aliekuwa na siasa na hoja za kutaja watu,kuhusu ufisadi anamuandama Lowasa tuu mbona wengine hawataji?
 
Kwani falsafa iliyowajenga cdm ulikuwa ni nini?kumuulize kilichomsaidia nsdari kushinda ubunge kama sio Richmond na wizi wa lowasa wa milion300 kwenye jumbo lake

Nassari anashinda tena Mwaka huu tena kwa kishindo,baada ya 25 October tunakuomba uje hapa utueleze Nassari kashinda kwa hoja ipi tena.
 
Tuache kukurupuka Demokrasia ni wengi wape na mawazo ya wachache yaheshimiwe..........Mzee yule ana haki ya kuongea anachoona ni sahihi!

Kama wengi wape na wengi ndio walioamua kumpokea Lowasa,sasa yeye anapiga ndila za nini?si atulie tuu.
 
ccm mnapoteza muda mwingi badala ya kumnadi mgombea wenu. Hivi naye akiamua kuhama mtafantaje
 
Salaam kwako Mzee Mwanakijiji na wanavijiji wengine!

Kwa haya tunayoyaona, wale waliotuhaminisha kwamba wanatuongoza kuelekea kwenye ukombozi wa pili wa Kifikra na Kiuchumi, wanageuka na kutaka kutuaminisha kwamba "Kijani" ndiyo chagua sahihi-nina mashaka. Tunajuwa wanaye kiongozi mwenye uwezo wa kukariri maili za barabara, idadi ya samaki na mifugo wengine, hata idadi ya wapiga kura. kama hiyo ni sifa, anafaa kwelikweli.

Kwa kiongozi, ambaye, katika karne hii bado anaamini katika kutembeza bakuli kwa wafadhili-ndiko kunakoleta maendeleo- ilhali nchi yake ina rasilimali nyingi kuliko hata kwa hao mabwana wakubwa-kweli anatufa kwelikweli!

Karne hii, kama tumefika sehemu tunataka tuwaaminishe watanzania kuwa bila Kijani, nchi itakuwa kama Libya...this is too wrong. Kwani ni mazingira mawili tofauti kabisa. watanzania wanaenda kupiga kura na kupractice democracy, ya Libya ilikuwa ni uhasi uliochochewa na Mataifa ya Magharibi-hatufanani nao hata kwa chembe....Kiongozi wa aina hii- waTanzania, anatufaa kwelikweli...

Wataalamu wa saikolojia ya elimu wanasema, miongoni mwa vitu vinavyoathiri afya ya akili ni pamoja na kukariri bila utaratibu, kwani hii hali inamfanya mtu kupoteza uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo (Critical thinking). Ikifikia hapa mtu hujaa sifa akiamini anaweza...

Naamini UKAWA ni ya waTanzania, naamini CHADEMA ni ya waTanzania,..Naamini CCM ni ya baadhi ya waTanzania wachache sana. Hii ndiyo maana waTanzania wanaonekana "Wapumbavu na Malofa". Wanasababu ya kuwaita watanzania hivyo, kwa sababu kila mwaka wa uchaguzi wanatuahidi vitu vingi visivyotekelezeka, na tunawachagua iwe kwa uhalali wa kura ama vinginevyo, na waTanzania hatusemi, na hatulalamiki....

Naamini waTanzania wamefikia kiwango cha juu cha uelewa, wameshalalamika vyakutosha, sasa ni muda wa vitendo. Naamini "vichinjio" vyao vitatumika vyema kutupa kiongozi atakaye tuongoza kuelekea ukombozi wa pili...

Mimi siyo muumini wa Chama chochote cha Siasa, ila ni muumini wa mabadiliko, hasa mabadiliko ya kweli...ukitaka kupitisha njia penye mlima, ni vema ukauvunjilia mbali huo mlima ili upate njia...

Watanzania lazima wajiulize...siku zote hizo alikuwa wapi? kwanini hakutokea siku walipofanyamakubaliano? Tumewaona akina Gasia na Nchimbi walivyoreact siku mpendwa wao alipokatwa...angalau ilileta mashiko...huyu wetu alikuwa anasubiri nini?????........

Mabadiliko ni sasa, mabadiliko ni wewe, yule, na mimi, mabadiliko ni sisi! Tusipuuze maumivu na vilio vya waTanzania vinavyotokana na ukosefu na uhaba wa huduma za msingi na ajira...waTanzania wamechoka kuwachoma watoto na vijana wao kwa kesi za ukabaji na uporaji mdogomdogo, huku tukiambiwa kuwa rasilimali zetu zinatoroshwa kwa ving'ora! Tusipuuze kabisa.

Big up sana Mkuu umemaliza kila kitu,huyo Mwanakijiji ni wa kupuuzwa tuu maana yeye siku zote huwa anaangaliaga maslai yake binafsi kwanza then yanafuata ya Taifa.
 
Siyo labda tupo tena mamilion tunaamini ivyo kwamba chadema ni mali yetu, then mbona majibu yako yametawaliwa na hofu hofu sana kama magamba?

Chadema ni mali ya wa kaskazini that am sure, ngoja kura zipigwe hamta amini, unafikili rais anachaguliwa na wa kaskazini pekee, just wait october 25, hamna rangi hamta ona...
 
Naona maasai na chaga are well organized. Working as a team..

Anhaahaa!! Ikulu hamnusi hata kwa ndumba.

Kila mkibanwa kwa hoja mnakimbilia Udini,Ukanda na Ukabila,Mwaka huu mbona mtakoma,
 
Hawa ni wanachama wa Chadema wanaimba "Mbowe ondoka na Lowassa" na kadri msafara unavyosonga mbele idadi ya waandamamaji inaongezeka. Polisi wanawatazama tu!

Kama wanaimba hivyo hao watakuwa wanatumiwa, usijali sana ukawa tutachukua nchi asubuiii na mapemaaaa..!!
 
Na kweli mpo mnaoamini ni mali ya Watanzania? well.. labda kweli mpo mnaoamini hivyo.
Mzee mwanakijiji, hata CCM ina wenyewe, na sio kweli kuwa ni "mali ya watanzania"! There is no group power, power is invariably personal! Katika kila jambo/organisation, Kuna mtu "yuko juu" ambaye ana commanding heights kwa "niaba ya wengine"???????!!!!!!
 
Na kweli mpo mnaoamini ni mali ya Watanzania? well.. labda kweli mpo mnaoamini hivyo.
Binafsi naamini kwamba Watanzania walio wengi wameichoka CCM wako tayari kuchagua jiwe kuliko kuirudisha CCM madarakani sijui mawazo ya watanzania wa huko Texas.
 
Mbowe tatizo lake anszani wtz hakuna kumbukumbu 2010 agenda ya Richmond ndo iliwapaisha Leo hii anasema mini?

Hatuhitaji kujikumbusha ya kale.Sasa kama richmond ndio ilipaisha Chadema unataka ndio iishushe?
 
Kila mtu anakuja kivyake Lissu anadai Dr.Slaa ndio mtu aliepitishwa na kikao kikuu cha CDM na Dr.Slaa ameligusia hili vilevile.

Leo tena Mbowe naye anasema Lowassa formal processes hizo hizo za chama zilimpitisha. Kwa utaratibu huo inawezekana vipi kikao cha pili tena kimteue mwengine bila ya ridhaa ya Dr.Slaa kuafiki kuachia kwanza au vinginevyo kutumia mabavu kumwambia aachie nafasi the latter makes sense. Ongezea na shabiki Mbatia naye all of a sudden anaijua katiba ya CDM na kutetea kuteuliwa kwa Lowassa na kamati kuu na kuenguliwa kwa Dr.Slaa.

Inasikitisha watanzania wanavyoweza chezewa akili kirahisi sana, hawa jamaa (CDM) walikuwa wanasubiri Lowassa akatwe kwanza na CCM kwa sababu zao wenyewe, lakini Lowassa huyohuyo ajatokea mbinguni kuingia CDM alikuwa na dhamira ya kugombea kupitia CCM kwanza na atakuwa anasababu zake binafsi za kuutaka uraisi.

Leo tena CDM inawaaminisha wafuasi wake sababu za Lowassa zimebadilika kisa kaingia CDM, mtu ambae ni wazi huku ilikuwa kama backup plan kwenye strategy yake ya kugombea uraisi; in other words wakati CDM wanajianda kukatwa kwake isingetokea leo hii Lowassa huyu huyu angekuwa mgombea wa CCM ndio angekuwa anawapiga madongo na CDM wanamwita kila aina ya neno la mtu mbadhirifu (all this changed in a space of two weeks) jamani ata NARC muungamo wao aukuwa hivi agenda yao ilipangwa muda mrefu.

Tanzanians are gullible bunch of people (I always believed that anyway); I mean how stupid is all this even to defend ata kama unataka mabadiliko ndio haya kweli wakati ni wazi hawa jamaa ni wasanii tu.
 
Kila kukicha watu wajinga na waerevu wanazaliwa kwani katika hotuba ya Dr.Slaa alikuwa anazungumzia ni nani mmiliki wa Chadema, KWA mantiki hio hata huyo aliesema hayo ni zwazwa tu
 
Hakuna chama cha mtu kila Chadema ni Mali ya watanzania wale ni viongozi tu! Haturudi nyuma kwa wimbo uliokwisha muda wake mbona Nyimbo zingine nyingi hawaziimbi wanaimba wimbo wa Richmond tu! Hizo nyingine wanamwachia nani? Aimbe wakati wao ndiyo watunzi Wa Nyimbo hizo zote.
 
Tuache kukurupuka Demokrasia ni wengi wape na mawazo ya wachache yaheshimiwe..........Mzee yule ana haki ya kuongea anachoona ni sahihi!

Yaah na sisi tunaongea tunachoona ni sasa safi sana usahihi wetu ni kuwa babu alikurupuka na kajimaliza
 
Back
Top Bottom