Ahsante Rais Samia, kwa hili Watumishi wa Umma tumekuelewa sana

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,807
13,056
Niliajiriwa 2013 tokea hapo sijawahi panda daraja.

Mwendazake alinyonya sana haki yetu.

Tena zile haki za kisheria kama increments ila mama ameponya majeraha ya msukuma.

Watumishi kwenye BAJETI 2021/22.

1. PAYE imeshushwa kutoka 9% mpaka 8%.

2. Bil 449 kwa ajili ya kupandisha vyeo watumishi 92,619.

3. Kutolewa kwa 6% ya tozo ya kulinda thamani ya mkopo wa elimu ya juu (Value Retention Fees).

4. Madiwani, Maafisa Tarafa na Watendaji kata kulipwa 100,000 kila mwezi kama posho.

5. Michango ya PSSF kulipwa direct kutoka Hazina badala ya ofisi za serikali kupeleka zenyewe.

TUMEKUELEWA mama, tunasubiri nyongeza ya mwakani.

Ijumaa nilipata barua yangu ya daraja safiii na sasa nasubiri NMB kitu kipya kiteme.

Ila kiukweli ukisomaa sheria za utumishi, kwasasa nilistahili kuwa juu ya daraja hili nililopandishwa sasa, ila yule msukuma yule sijui anaenda kuongoza malaika gani wanaozuia haki za watu tena za kisheria.

#ASANTE MAMA.

Cha ajabu kupandishwa huku madaraja mpaka MATAGA wamefurahia.

Yaani MATAGA walewale waliokuwa wana "support" mwendazake asiongeze kitu, ndio haohao wanaokenua mama alivyoongeza..!!!

#YNWA
 
Ndugu.
Pamoja na kumuelewa lakini pia tafakari na hii. PAYE imeshushwa kutoka 9% hadi 8% ni jambo jema lakini inawezekana isiwe na maana kushuka kwa sababu kama hizi.

1. Kodi ya laini za simu imeanzishwa jambo ambalo litahitaji ile hela ya punguzo kwenye PAYE.

2. Kodi ya majengo kupitia kununua LUKU ambapo utalazimika kulipa pale unapolipa bill ya umeme ukiwa kwenye nyumba ya kupanga au ya kwako.

3. Kuwepo kwa kodi mpya kwenye miamala ya simu kila unapotuma na kutoa hela.

4.Ongezeko la kodi kwenye bidhaa za mafuta ya dizeli na petrol ambapo gharama za usafiri na usafirishaji zinatarajiwa kupanda.

Kwa hizi baadhi ya kodi mpya ni vigumu kumuelewa mama kwani ni kama mtu amekukupunguzia shs. Mia kwenye hela unayopata ila atachukua elfu moja kwako.
 
Hivi ni lini mwalimu wa Tanzania naye ataanza kulipwa posho?

Kumkubali huyo mama ambaye ni zao la udhalimu wa mwendazake mimi wala siungani naye. Kipindi nateseka alikuwa VP na hakuwahi hata kutoa tamko.

Watumishi tuna madai mengi sana kuanza kusifia mapema namna hii wakati hadi muda hakuna kilichobadilika mfukoni inaonesha ni jinsi gani watumishi wa umma hatujielewi.

CCM ni ileile na viongozi ni walewale. Watumishi wa umma ni muda kutafuta malisho mengine huku tukifanya kazi zao kadiri tunavyolipwa.

Mtumishi wa umma kumsubiri mwanasiasa akupe mishahara minono ni sawa kumtegemea shetani akupeleke mbinguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni lini mwalimu wa Tanzania naye ataanza kulipwa posho?

Kumkubali huyo mama ambaye ni zao la udhalimu wa mwendazake mimi wala siungani naye. Kipindi nateseka alikuwa VP na hakuwahi hata kutoa tamko...
Babu relax is new financial yr coming.
Everything will be alright.

Ofisini kwetu tumemaliza calculation za arrears na likizo kwa walimu.
Na zimetumwa Dodoma.

Kuhusu hili..

""Mtumishi wa umma kumsubiri mwanasiasa akupe mishahara minono ni sawa kumtegemea shetani akupeleke mbinguni.""

Mbona watu Wana business na investment zao...
Ila unataka kusema Moh aache kuokota buku kwakua ana mamilioni?

Madaraja ni haki yangu ambayo msukuma alininyima na biashara zangu nafanya.

#YNWA
 
Hivi ni lini mwalimu wa Tanzania naye ataanza kulipwa posho?

Kumkubali huyo mama ambaye ni zao la udhalimu wa mwendazake mimi wala siungani naye. Kipindi nateseka alikuwa VP na hakuwahi hata kutoa tamko
Na nyie ndio mliokua mkitukatalia kutuandika kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Usitake kumlaumu Mama kwa yasiyomuhusu. Tumuunge mkono mama mkuu. Kila mmoja atafikiwa tu.
 
Babu relax is new financial yr coming.
Everything will be alright.

Ofisini kwetu tumemaliza calculation za arrears na likizo kwa walimu...
Mzee mwenzangu concern yangu ni pale ulipokuja na sifa za kumtetea huyo mama as if malaika ametua madhabahuni.

Kingine, sijamaanisha kwamba unategemea mshahara tu, hata mimi sitegemei mshahara tu.

Halafu madeni ninayowadai nimeshayasamehe hizo faranga tumbueni tu huko juu, baada ya kuzungushwa kama mtoto kwenye madai yangu nimeshaapa kutopeleka nyaraka ya madai popote pale. Nimeridhika na mshahara wangu huu. Laki 2 zinanitosha mimi na familia yangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom