Asante Magufuli kumfunza mdogo wangu Ujasiriamali

Asante Magufuli kumfunza mdogo wangu Ujasiriamali

Safi sana mkuu,ngoja nami nijaribu .......cjui nitaweza
 
"karibuni vifuniko vya asali na shuka za mihogo"

Kwani chupi siriiii.... mi niliuzaga hizi kitu long. Kikubwa ni kuiheshimu kazi yako na kutafuta genuine bidhaa. Pia suala la kubadilika kadri ya fashion ndo unatusua. Suala la kuomba ajipime uone kama inamfit ni kuachana nayo maana hukawii kupoteza mtaji wote kiboya.

But hii trick yako iko poa pia
 
Tishio la kurudi kijijini hatimaye limefungua ubongo wa kijana uliokuwa umelala. Hili ni somo kubwa sana kwa watu wengi. Ngoja nikareplicate hii kitu somewhere.

Pamoja rafiki, ujasiliamali ni akili yako tu
 
Hiyo imekaa poa sana!
Umemnunulia dogo ndoano subiri ayavue manoti...
Nawewe fungua jicho la tatu mkuu...
Ukimbwela na kumtumbulia macho huyo chalii wakati anazimake, hakyaMungu one day you are going to be his/her employee!!
Siyo mbaya, kila mtu na bahati yake
 
Inaonekana vyupi na sidiria vinanunulika sana aisee..!
 
Bavicha wao kulialia kwenye mitandao ya kijamii ndio ajira yao mpya!!!
 
Ni wewe tu na uncle wako mlichelewa kubuni wazo la biashara, Sizonje hastahili pongezi yoyote!
 
Asante magu na mimi baada ya kukaa nyumbani nikiwa sina ajira na kulala kuanzia asubuhi hatimaye akili zimeniKaa sawa!! Nimepata ujasiri wa kutafuta kazi binafsi kwa sasa ,nimepata mshahara ni sawa na huo wa ualimu!!! Kwa hiyo stress za kusubiri ajira za anko magu zimeisha!!
 
Wana ukumbi,
Mtoto wa shangazi yangu alikulia kwangu na kwa bahati mbaya hakufanya vzr matokeo ya form 4, ila alipata credit za chuo cha ualimu huko Kasulu TTC. Nilijitahidi kumlipia mahitaji yake na akamaliza vyema kisha akarudi Arusha kusubilia kupangiwa kituo cha kazi. Muda wa masubirio, dogo alikuwa anashinda home tu, alimaliza CD zote, series, movies na magazeti hasa baada ya rais kusitisha ajira. Kiufupi alinipa wakati mgumu hasa alipokuwa akitegemea kila kitu from me. Nilimshauri afanye issues za pesa, akawa ananijibu nasubiria ajira.

Akili mpya
Mwaka huu mwezi wa 7 nilinunua chupi mpya 30 za wadada, nikamfuata na kumwambia "nakupa huu mzigo, ukirudi nao after 7 days, nakupa nauli unarudi bush." Dogo alimind sana ila after 5 days alimaliza mzigo na kunipatia hesabu nzuri. Nilimuachia pesa zote, nikampa chupi nyingine 50 na sidiria10, akazizungusha hasa vyuoni, ndani ya 11 days akaja na bonge la profit na akaanza kuuza flash discs, calculators na sasa kaanzisha mradi wa kuku na kijibustani. Dogo anapiga hela sana na nikimuuliza issue za ajira anatoa nje....

Last week kaja na proposal ya kuhama hapa kwangu akapange, nimemgomea.......

Japo tunaisoma namba tasa, kwa hili asante JPM kwa kutunyoosha na kutupa akili za kujiajiri....
Kuna mtu ukimpa wazo lakufanya biashara kama hii atakwambia mtaji hana wakati ana simu ya 1.5m!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom