Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Watoto watatu kati ya wanne ambao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Ngoile na wakazi wa kijijj Cha Ngoile wilayani Ngorongoro Mkoani hapa wameuawa kwa kuliwa na Simba huku mmoja akijeruhiwa wakati wakitoka shuleni.
Akiongea ofisini Kwa kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Olobiko Metui(10),Ndaskoi Sangau(9) na Sanka Saning'o (10) ambao wote ni wanafunzi wa darasa la tatu .
Aidha kamanda amedai kuwa kati ya watoto hao ,mtoto mmoja,Kiambwa Lektonyi(11) alinusurika kifo baada ya kujeruhiwa vibaya na Simba na anapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo.
Masejo alifafanua kuwa tukio hilo limetokea juzi agosti 3 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi katika Kijiji hicho wakati wanafunzi hao wakijerea nyumbani kutoka shuleni .
Ends.....