Arusha: Rais Samia atoa TZS 520BL sawa na 80% ya bajeti nzima ya maji ya Taifa ya mwaka

Watu wanabadili majina wewe utachelewa hoja zake zinauzito hata kama kajiunga leo,
 
Inapendeza na Ahsante kwa taarifa...
Smart911
good
 
TAARIFA KWA UMMA

KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU CHINI

23.10.2021
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi na wakazi wa Bagamoyo Mkoani Pwani hadi Kigamboni Jijini Dar es salaam kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji .

Sababu: Upungufu wa maji katika chanzo cha Mto Ruvu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Maji kupitia Bonde la Wami Ruvu, kina cha maji cha mto Ruvu kimepungua kufuatia kiangazi cha muda mrefu.

Kufuatia upungufu wa maji mtoni, uzalishaji wa Maji umepungua kutoka lita milioni 520 kwa siku hadi kufikia lita milioni 460. Upungufu huo unatokana na kupungua kwa uzalishaji katika mtambo wa Ruvu Chini ambao husambaza maji kwa asilimia 70 ya eneo la huduma la DAWASA. Mtambo wa Ruvu Chini kwa kawaida huzalisha lita milioni 270 kwa siku na hivi sasa unazalisha kiasi cha lita milioni 210 kwa siku.

DAWASA kwa kushirikiana na Ofisi za Bonde la Wami Ruvu wanaendelea na zoezi la kusitisha matumizi ya maji kwa watumiaji wengine katika mto huo ikiwa ni pamoja kusitisha vibali vya umwagiliaji ili kuruhusu maji kufika mitamboni.

Ili kuhakikisha kuwa maji yanapatikana kwa usawa katika eneo linalohudumia na mtambo wa Ruvu Chini, DAWASA imehamisha sehemu ya maji ya Ruvu Juu ili yatumike kwa maeneo yaliyokuwa yanahudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini. Mabadiliko haya yanapelekea kupungua kwa msukumo wa maji kwa baadhi ya maeneo.

Maeneo yatakayo athirika: Maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Maji Ruvu chini, kuanzia Bagamoyo hadi Kigamboni.

DAWASA inawaomba wananchi kutumia maji kwa uangalifu katika kipindi hiki.

Tupigie kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 au ujumbe mfupi 0735202121 (WhatsApp)

Imetolewa na
*Kitengo cha Mawasiliano na .
 
Madam President tangu aingie madarakani hakuna mradi hata mmoja aliouanzisha na iliyopa anadai hakuna pesa ya kuiendeleza, Mradi pekee aliouanzisha kikamilifu ni wa CORONA. Hata pesa ya kujenga stand mkoani Arusha anataka kuomba mkopo. What a Shame!!
 
Good
 
Nitatizo la muda tu hili
 

Waongo wakubwa 😂 pesa ni mradi wa siku nyingi sana toka wakati wa Kikwete na ni pesa za bank ya Dunia. Mradi umeisha wakati wa Magufuli leo Mama katoa pesa😂😂
 
Hivi Arusha hawaishi watu wa mikoa mingine kwa kazi, biashara, au utalii? Huu uwekezaji kwenye maji in turn utafaidisha nani haswa? si nchi nzima? Mbona Dar na Dodoma panapojengwa miundo mbinu mingi ya kisasa hamsemi Raisi kwa watu wa Dar usipime, au Rasi kwa Dodoma usipime? Tuwe rational kwenye arguments zetu tafadhali
 
Ni uandishi tu mkuu Wangu,
Nisamehe kama nimekuudhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…