Arusha ni Mji ulioachwa uharifu utambe

Huko walishasahau hata maadili ni kitu gani, si watoto wazee wanaume wanawake, vijana hao ndo vinara ovyo kabisa,
 
Hakuna sehemu Arusha utafananisha na SA bhana acha zako Arusha maduka yapo wazi mpaka saa sita usiku ni sehemu gani jo'burg utakuta duka la mtaani lipo wazi saa sita usiku pana maduka mawili ya dawa Arusha hayafungwi ni masaa 24 Jo'burg ambayo dakika yeyote Mall inavamiwa ufananishe na haya maeneo ambayo kiwango cha uharifu ni kidogo mno...
Dunia ya Sasa imejikita kwenye 24 hours economy, wewe unaongea juu ya maduka mawili ya dawa yanayokesha yaliyoko katikati ya mji?

Ningekuelewa kama ungenambia maduka Arusha kwa ujumla wake hufanya kazi 24 /7.
 
Nikiri kwamba mie kwa majukumu yangu ya kimaisha ni mtu ninayezunguka sana katika nchi hii na maeneo mengine ya Dunia ukipenda.

Arusha pamoja na kuwa na sifa za madhari nzuri, muingiliano wa watu wa mataifa mbalimbali, na taasisi mbalimbali za kimataifa, ukweli usemwe, Jiji hilo sio salama kabisa kwa maisha ya watu.

Arusha ndo mahali ambapo bangi inavutwa mahali popote, ni mahali ambapo watu wanatembea wakiwa wamechomekea visu kwenye nguo na vinaonekana, Arusha ndo watu wamejaa matusi ya nguoni na hakuna anayeshangaa.

Ukweli, Jiji hilo limejaa aina ya maovu ambayo mengi yake ukiyaona hakika yameruhusiwa na jamii yenyewe na vyombo vya Dola pia.

Kuna wakati najiuliza, hivi hii ni jamii Gani inayoogopa waovu kiwango hiki?

Ni kweli sitetei matumizi ya nguvu na kutofuata sheria, lakini ukweli ni kwamba, jamii ya Arusha, kwa sehemu kubwa ni jamii isiyozingatia maadili kabisa na ndo maana hata yanapofanyika matendo ya kijinai na uovu, bado utawaona watu wametulia tu na huoni kuteseka na kukereketwa kuzuia mambo ya kijinga ya viwango hivyo.

Kwa kuwa nimejitambulisha kama mtembezi, hapo ndo nawakumbuka watu kutoka kanda ya ziwa. " Jamii hailei mambo ya kijinga yaliyopitiliza kama yanayotendeka kwenye Jiji la Arusha.

Ni rahisi sana kushikwa na kutandikwa viboko hadharani na wananchi ukiwa baadhi ya maeneo kanda ya ziwa kwa sababu tu umetukana mama au mtu yeyote kinachoitwa matusi ya nguoni.

Kwa hiyo sitetei watu kuvunja sheria na kujichukulia sheria mikononi, lakini ukweli usemwe, " jamii haionekani hata kucahukia tu vitendo hivyo". Jamii ikianza kuonyesha hasira juu ya maovu na vitendo vyenye mwelekeo wa jinai, waovu na watu wanaojihusisha na mambo hayo wataogopa na kuacha au kuyafanya under cover na siyo waziwazi kama ilivyo.

Naiasa jamii ya Jiji la Arusha kubadili tabia na kuanza kuchukia aina ya matendo ya ovyo yanayoendelea jijini humo.

Kwa vyombo vya Dola, nashauri kuanza kufanya kazi zao nje ya mazoea.

Mazoea wanayofanya walinzi wetu wa amani, yatafanya jamii ianze kuishi bila kuogopa Sasa.

Uwepo wa majeshi huleta nidhamu katika jamii. Tatizo ninaloliona, uwepo wa majeshi ,Sasa unakuwa kama jambo la kawaida.

Hivi unawezaje ukiwa police, kupita mahali kwenye genge ambalo ukuta walioegemea au ukipenda kwenye kijiwe, kumechorwa picha za wavuta bangi na watu wanaovuta bangi na hata huulizi au kulazimisha magenge na vijiwe hivyo kutoweka?

Inawezekanaje ,kondakta wa gari anakutana na traffic police, wanamsikia kabisa ananuka bangi na bado hawawezi kumkamata na kumpeleka kituoni akajibu kwa Nini ananuka bangi?

Tukio lililotokea Jana la kuuawa wa kijana anayeitwa Ally Dangote, kwangu Mimi pamoja na kwamba kauawa lakini limekuja kwa kuchelewa. Kijana mwenye umri wa miaka 19 anawezaje kutamba kwenye jamii inayochukia uovu muda wote huo?

Inawezekana vipi mtu anasumbua na kuua watu hadharani Ili hali wananchi wanajua anakoishi, anachofanya na anapatikanaje? Police na vyombo vya Dola, vinawezaje kuacha mwovu anatamba karibu mwezi mzima akiua watu hadharani?

Nini maana ya uwepo wetu kama wananchi na vyombo vya Dola?

Wakati Fulani nilipatwa na taharuki nikiwa maeneo Fulani ya Jiji hilo.

Na ilikuwa hivi ," Kuna kijana mmoja aliyekuwa mwendesha pikipiki aliuawa kwa mazingira ya kugongwa na gari" sekeseke lilikuja siku ambayo kijana yule alikuwa anapelekwa mazikoni. Believe me, barabara ilichafuka. Pikipiki zilijaa barabara nzima kana kwamba mji umetekwa na boda boda, barabara ni zao na hakuna mwingine anayezitumia..

Ungewaona vijana wameshikilia chupa za pombe barabarani, wanakunywa pombe wakati wanaendesha pikipiki.

Ajabu ilifika mahali , wengine walikuwa wanabishana kwa maneno, hivyo wanachofanya ni kutelemka kwenye boda na wengine bajaji, wanapigana ngumi, huku magari ya abiria na watumiaji wengine wa magari wakiwa wanasubiri ugomvi uishe.

Pale nilipokuwa, nilishuhudia ugomvi unaisha wenyewe kwa wao kujiamua.

Sikuoni raia hata kulalamikia tu, waendesha magari wako kwenye magari wanasubiri nao bodaboda wamalize ugomvi wao.

Mbaya zaidi hakuna police waliokuja kuondoa hiyo bughudha, achilia ukweli kwamba kituo Cha police kilikuwa kama mita 200 tu kutoka eneo la tukio na magari yenyewe yalikuwa msururu mpaka eneo la kituo.

Hebu nambie katika mazingira hayo, huu uovu haujaruhusiwa?

Watu wa Arusha ni waoga hata kukemea tu ujinga. Wanajifanya wako busy kutafuta pesa. Wamejaa ulevi wa kutafuta Mali ambazo zinaibwa kijinga na watu wanaowalea kwa kuruhusu tambia mbaya kutamalaki.

Vyombo vya Dola na hasa police, woke up please.

Huu mji Sasa unataka aina nyingine ya ku curb criminality ambayo naiona inanyemelea mji huu.

Huu mji unataka psychology ya askari kubadilika Sasa. Huu mji unataka upolisi hasa na siyo kucheza na viashiria vya uhalifu.

Magenge yaliyotapakaa Kila mahali kama vijiwe yachunguzwe na yapigwe marufuku.

Unywaji wa mapombe usio na mipaka unazaa uharifu uliyopitiliza kwa kudhani Hawa ni walevi tu.

Yuko wapi RPC wa aina ya Kombe miaka ile? We need a serious police force , if at all, we want to defeat the rampant criminality hovers the city of Arusha.

Huijui Arusha hata kidogo, Ni mitazamo yako tu ya kipumbavu ya mitandaoni.
 
Huwezi kujuwa natetea nini kwasababu sitetei chochote.

Wewe umesema natetea na kuhalalisha uhalifu wa hao wa Arusha unaowasema kwa kutaja Panya road.

Wewe hauishi Arusha lakini unapiga kelele kuliko watu wa Arusha. Si ukae huko kanda uliposema watu wanachapwa viboko?

Na kule Panya road nao wachapwe viboko?

Unasema nimekariri wakati ni usemi wenye originality yake umeusema kwa namna ambayo ni ndivyo sivyo na wala haukuwa na mantiki kwenye hoja yangu. Wewe ndo utakuwa umekariri kwasababu haujui matumizi yake.

You regard me as a crimina? Wewe ni flight attendant?

Watu wa Arusha wangekuwa wamezoea hayo unayosema, wasingelalamika kuhusu vitendo vya kihalifu vya Ally Dangote.

Tumia akili kama unayo.
Ungekuwa na akili hiyo Wala usingetumia nguvu kupinga jambo ambalo ni noble kabisa. Usipobadilika nakuona utakuja kuwa notorious criminal hapo baadae.
 
Huijui Arusha hata kidogo, Ni mitazamo yako tu ya kipumbavu ya mitandaoni.
Kama siyo kwamba wewe ni mhalifu basi uko kwenye maandalizi ya kuwa hivyo.

Kutukana hapa ndo kunafanya nipate mawazo haya. Hakuna mtu asiye na element za uhalifu anaweza kutukana kwa mawazo mazuri yaliyowekwa hapa.

Angalia, ukiwa na wewe uko hivyo" we are coming after you".
 
Nimeishi Arusha from nina miaka 9, nimesoma Levolosi, Arusha Seco, nimesoma UD nikarudi Kufanya Masters Esami, nimejenga Arusha Njiro kwa Msola, nimekuja Dar kibiashara nikiwa na miaka 50...

Nime experince Vibaka Dar es salaam zaidi ya Arusha, mna ulimbukeni tu kwa hizi habari za ajabu ajabu zinazo represent sehemu ndogo sana Arusha.

Kwa miaka yangu yote, kama nimewahi muona mtu anavuta Bangi public ni wakati nasoma secondary, there after kwenye utu uzima wangu sijawahi kuona mtu anavuta bangi.

Nikiwa Arusha, ninaweza kushuka kwenye ki Aic saa 4 usiku, nikatembea kuelekea home bila shida bila Mgogoro. HAYO Mnayoyaona na kuyaandikia maelezo marefu ya kipumbavu, ni kama maeneo ya Mazense ambayo yapo dunia nzima. HATA LA carlifonia kuna mahali huwa hatupiti.

Kukuongezea fact, Arusha kuna wazungu wengi sana wanatembea, angalia comment zao na maelezo yao kuhusu Arusha utasikia wanavyosema, mmekaa tu kwenye mitandao mnaandika mambo ya hovyo yasiyo maana wala ukweli.

Huijui Arusha Mpumbavu kabisa wewe!
 
Nimeishi Arusha from nina miaka 9, nimesoma Levolosi, Arusha Seco, nimesoma UD nikarudi Kufanya Masters Esami, nimejenga Arusha Njiro kwa Msola, nimekuja Dar kibiashara nikiwa na miaka 50...

Huijui Arusha Mpumbavu kabisa wewe!
Bado naziona element za kuwa mhalifu kwako. Wapi utamkuta mtu na masters cjui biashara na umri huo anatukana mtu pumbavu.

Wewe ni case study ya uhalifu ninaousema.

Kama wewe na sifa zote unatukana hivyo, nambie wale walioko huko Sasa, wasiojua hata mlango wa masters ulipo.
 
Upo sahihi.
 
Kwanini matajiri wengi wanatokea Arusha kama watu wote Arusha ni wavuta bangi?
Wapi nimesema watu wote wa Arusha ni wavuta bangi?
Alafu hao matajiri wa Arusha wanatoka wapi na kwenda wapi?

Bakhresa ,mo,ni watu wa Arusha ? Maana hao ndio matajiri.
Alaf hao matajiri wa Arusha wanapimwa katika angle ipi?
Ndo hizo mentality za kishamba kujiona nyie ni watu unique Sana wakat kiuhalisia nyie ni watu wa kawaida Sana.
 
Mo na Bakhresa ni watanzania? wale ni Mwarabu na Mhindi
 
Nikiri kwamba mie kwa majukumu yangu ya kimaisha ni mtu ninayezunguka sana katika nchi hii na maeneo mengine ya Dunia ukipenda.

Arusha pamoja na kuwa na sifa za madhari nzuri, muingiliano wa watu wa mataifa mbalimbali, na taasisi mbalimbali za kimataifa, ukweli usemwe, Jiji hilo sio salama kabisa kwa maisha ya watu.

Arusha ndo mahali ambapo bangi inavutwa mahali popote, ni mahali ambapo watu wanatembea wakiwa wamechomekea visu kwenye nguo na vinaonekana, Arusha ndo watu wamejaa matusi ya nguoni na hakuna anayeshangaa.

Ukweli, Jiji hilo limejaa aina ya maovu ambayo mengi yake ukiyaona hakika yameruhusiwa na jamii yenyewe na vyombo vya Dola pia.

Kuna wakati najiuliza, hivi hii ni jamii Gani inayoogopa waovu kiwango hiki?

Ni kweli sitetei matumizi ya nguvu na kutofuata sheria, lakini ukweli ni kwamba, jamii ya Arusha, kwa sehemu kubwa ni jamii isiyozingatia maadili kabisa na ndo maana hata yanapofanyika matendo ya kijinai na uovu, bado utawaona watu wametulia tu na huoni kuteseka na kukereketwa kuzuia mambo ya kijinga ya viwango hivyo.

Kwa kuwa nimejitambulisha kama mtembezi, hapo ndo nawakumbuka watu kutoka kanda ya ziwa. " Jamii hailei mambo ya kijinga yaliyopitiliza kama yanayotendeka kwenye Jiji la Arusha.

Ni rahisi sana kushikwa na kutandikwa viboko hadharani na wananchi ukiwa baadhi ya maeneo kanda ya ziwa kwa sababu tu umetukana mama au mtu yeyote kinachoitwa matusi ya nguoni.

Kwa hiyo sitetei watu kuvunja sheria na kujichukulia sheria mikononi, lakini ukweli usemwe, " jamii haionekani hata kucahukia tu vitendo hivyo". Jamii ikianza kuonyesha hasira juu ya maovu na vitendo vyenye mwelekeo wa jinai, waovu na watu wanaojihusisha na mambo hayo wataogopa na kuacha au kuyafanya under cover na siyo waziwazi kama ilivyo.

Naiasa jamii ya Jiji la Arusha kubadili tabia na kuanza kuchukia aina ya matendo ya ovyo yanayoendelea jijini humo.

Kwa vyombo vya Dola, nashauri kuanza kufanya kazi zao nje ya mazoea.

Mazoea wanayofanya walinzi wetu wa amani, yatafanya jamii ianze kuishi bila kuogopa Sasa.

Uwepo wa majeshi huleta nidhamu katika jamii. Tatizo ninaloliona, uwepo wa majeshi ,Sasa unakuwa kama jambo la kawaida.

Hivi unawezaje ukiwa police, kupita mahali kwenye genge ambalo ukuta walioegemea au ukipenda kwenye kijiwe, kumechorwa picha za wavuta bangi na watu wanaovuta bangi na hata huulizi au kulazimisha magenge na vijiwe hivyo kutoweka?

Inawezekanaje ,kondakta wa gari anakutana na traffic police, wanamsikia kabisa ananuka bangi na bado hawawezi kumkamata na kumpeleka kituoni akajibu kwa Nini ananuka bangi?

Tukio lililotokea Jana la kuuawa wa kijana anayeitwa Ally Dangote, kwangu Mimi pamoja na kwamba kauawa lakini limekuja kwa kuchelewa. Kijana mwenye umri wa miaka 19 anawezaje kutamba kwenye jamii inayochukia uovu muda wote huo?

Inawezekana vipi mtu anasumbua na kuua watu hadharani Ili hali wananchi wanajua anakoishi, anachofanya na anapatikanaje? Police na vyombo vya Dola, vinawezaje kuacha mwovu anatamba karibu mwezi mzima akiua watu hadharani?

Nini maana ya uwepo wetu kama wananchi na vyombo vya Dola?

Wakati Fulani nilipatwa na taharuki nikiwa maeneo Fulani ya Jiji hilo.

Na ilikuwa hivi ," Kuna kijana mmoja aliyekuwa mwendesha pikipiki aliuawa kwa mazingira ya kugongwa na gari" sekeseke lilikuja siku ambayo kijana yule alikuwa anapelekwa mazikoni. Believe me, barabara ilichafuka. Pikipiki zilijaa barabara nzima kana kwamba mji umetekwa na boda boda, barabara ni zao na hakuna mwingine anayezitumia..

Ungewaona vijana wameshikilia chupa za pombe barabarani, wanakunywa pombe wakati wanaendesha pikipiki.

Ajabu ilifika mahali , wengine walikuwa wanabishana kwa maneno, hivyo wanachofanya ni kutelemka kwenye boda na wengine bajaji, wanapigana ngumi, huku magari ya abiria na watumiaji wengine wa magari wakiwa wanasubiri ugomvi uishe.

Pale nilipokuwa, nilishuhudia ugomvi unaisha wenyewe kwa wao kujiamua.

Sikuoni raia hata kulalamikia tu, waendesha magari wako kwenye magari wanasubiri nao bodaboda wamalize ugomvi wao.

Mbaya zaidi hakuna police waliokuja kuondoa hiyo bughudha, achilia ukweli kwamba kituo Cha police kilikuwa kama mita 200 tu kutoka eneo la tukio na magari yenyewe yalikuwa msururu mpaka eneo la kituo.

Hebu nambie katika mazingira hayo, huu uovu haujaruhusiwa?

Watu wa Arusha ni waoga hata kukemea tu ujinga. Wanajifanya wako busy kutafuta pesa. Wamejaa ulevi wa kutafuta Mali ambazo zinaibwa kijinga na watu wanaowalea kwa kuruhusu tambia mbaya kutamalaki.

Vyombo vya Dola na hasa police, woke up please.

Huu mji Sasa unataka aina nyingine ya ku curb criminality ambayo naiona inanyemelea mji huu.

Huu mji unataka psychology ya askari kubadilika Sasa. Huu mji unataka upolisi hasa na siyo kucheza na viashiria vya uhalifu.

Magenge yaliyotapakaa Kila mahali kama vijiwe yachunguzwe na yapigwe marufuku.

Unywaji wa mapombe usio na mipaka unazaa uharifu uliyopitiliza kwa kudhani Hawa ni walevi tu.

Yuko wapi RPC wa aina ya Kombe miaka ile? We need a serious police force , if at all, we want to defeat the rampant criminality hovers the city of Arusha.
Tembelea UNGA LTD uone maisha ya watu wa kule halafu ujiulize mtoto anayezaliwa na kukulia kule anaweza kuwa raia wa aina gani
 
Mo na Bakhresa ni watanzania? wale ni Mwarabu na Mhindi
Acha hiyo Netanyahu. Wale ni watanzania wenye asili ya kihindi na kiarabu.

Kuwasema vinginevyo ni kitowatendea haki alafu inatufanya Mimi na wewe tuonekane ni watu washamba( naive).

Kuna wamarekani weusi, Kuna waingereza weusi nk. Hawa ni watanzania wenye asili hiyo. Vinginevyo hata wewe tutakubagua, maana wewe ni Netanyahu Myahudi!
Ha ha ha ha ha!
 
Dunia ya Sasa imejikita kwenye 24 hours economy, wewe unaongea juu ya maduka mawili ya dawa yanayokesha yaliyoko katikati ya mji?

Ningekuelewa kama ungenambia maduka Arusha kwa ujumla wake hufanya kazi 24 /7.
Mkuu wewe unaweza kuwa una goggle kupata taarifa za Dunia ya sasa mimi huko walikoendelea ndio sehemu nayozunguka sana ila siwezi kuifananisha Tanzania iwe sawa na Singapore au Hong Kong leo kwa kuwa nimeona huko maduka hayafungwi sina ushamba huo wa kuponda Tanzania kwa sababu pana vitu naviona USA au UK....Bus hizi zimeanza kusafiri usiku tena kitu ambacho hakikuwepo kilikuwepo kipindi cha nyuma sana wakasitisha kwa hiyo kila kitu ni hatua ukiambiwa maduka mawili matatu jua Hospital zote nazo zina maduka ukitaka kwenda kupata dawa usiku unanunua tuu shida ipo wapi hapo Mkuu...
 
Mkuu, kujifananisha na Mexico au Colombia sio sahihi! Criminal rate kuwa kubwa katika izo Nchi inachagizwa na Biashara ya madawa ya kulevya na makundi mengi ya kihalifu.

Je lengo lako unataka tufikie hali hiyo ndio Serikali ichukue hatua.

Ni muhimu kudhibi uhalifu kabla haujaota miziz kama ilivyo kwa Mexico, Colombia, Paraguay na Brazil.
Hakuna uhalifu Arusha kwa extent anayosema mleta mada.

Arusha ni mji ambao taasisi nyingi zinafanya makongamano yake, taasisi za kitaifa na kimataifa, watu wanafanya mambo yao hakuna madhara yeyote.

Watalii wanajiachia mpaka mida mibovu.

huyu anashindwa kutofautisha life style na uhalifu, kwake yeye labda aina yabmaisha ndio anayoiona kama uhalifu ,

Ila uhalifu kwa maana ya uhalifu kwa Arusha hauna tofauti sana na mikoa mingine, Dar panda Road walikua wanasimamishab mji.

Kagera kulikua na matukio ya utekaji nyara mengi tu, njombe, mbeya rate ya uhalifu ipo juu pia

Arusha haipo hata katika top 5 ya mikoa inayoongoza kwa uhalifu dhidi ya binadamu hivyo hoja ya mletavmada na yako pia inakosa nguvu.
 
Ripoti hiyo ya uhalifu ya jeshi la polisi kwa mwaka 2021 Arusha haipo hata top five.

Mleta mada analeta chuki zake binafsi.

Ni wa kumpuuza.
 
Attachments

  • Crime_Report_January_to_ December_2020.pdf
    5.8 MB · Views: 2
Nchi hii utajua watu wapo serious na kazi zao pale uhalifu unapoleta madhara makubwa. Ila huu mwingine wa kitaa, mikoa mingi tu ina mitaa yenye uhalifu na wahalifu wanaojulikana Ila hawaguswi

Ni sawa na dar, hadi panya road waue na kufanya matukio makubwa ndio unaona vyombo vya usalama vinashtuka. Ila kuna sehemu hadi navyoandika hapa hazipitiki bila hofu ya kudhuriwa na zimeachwa tu. Sio tatizo la chugga, ni la taifa zima
Uko sahihi. Hata moro kuna mitaa ikifika jua limezama ukikatisha kama sio mwenyeji unatafuta jambo lako na kitakachokukuta usilaumu mtu. Kama wizi wa kupora na pikipiki nahisi hata ulianzia moro
 
Hakuna uhalifu Arusha kwa extent anayosema mleta mada.

Arusha ni mji ambao taasisi nyingi zinafanya makongamano yake, taasisi za kitaifa na kimataifa, watu wanafanya mambo yao hakuna madhara yeyote.

Watalii wanajiachia mpaka mida mibovu.

huyu anashindwa kutofautisha life style na uhalifu, kwake yeye labda aina yabmaisha ndio anayoiona kama uhalifu ,

Ila uhalifu kwa maana ya uhalifu kwa Arusha hauna tofauti sana na mikoa mingine, Dar panda Road walikua wanasimamishab mji.

Kagera kulikua na matukio ya utekaji nyara mengi tu, njombe, mbeya rate ya uhalifu ipo juu pia

Arusha haipo hata katika top 5 ya mikoa inayoongoza kwa uhalifu dhidi ya binadamu hivyo hoja ya mletavmada na yako pia inakosa nguvu.
Mr stroke, ckujui, lakini kama ulienda shule basi hiyo shule haikukusaidia sana kujua mambo.

Mimi nimesema Arusha Kuna uhalifu wa kizembe ambayo jamii na vyombo vya Dola inabidi viungalie .

Mbona wewe Kila wakati unaleta kujilinganisha na wengine? Hivi ukijilinganisha na wengine ndo uhalifu wako unageuka kuwa si uhalifu?

Nakuona wewe ni mtu usiyejua kujadili mambo kisomi. Bila shaka una damu ya siasa inayokusukuma kushinda hoja kwa kupiga kelele badala ya kujadili mada katika mukhitadha wake( context).

Hatushindanishi uhalifu wa sehemu Moja na nyingine. Mimi nimetoa taarifa ya uhalifu niliona hapo Arusha muda niliokuwa hapo, Sasa unalinganisha Ili upate nini?

Mada yangu haijasema Arusha ni mji wenye uhalifu kuliko miji/ majiji yote duniani. Hiyo comparative analysis ungeifanya kama tungekuwa tunalinganish a hali ya uhalifu na maeneo mengine.

Mbona unakazana sana kukataa uhalifu ambao mie nimeuona? Je wewe nae uko kwenye syndicate ya huo uhalifu?

Takwimu zako za uhalifu za polisi ulizoweka hapa, ukiachia mbali kuhoji auntenticity yake, tayari hizo takwimu ni outdated. Niletee walau takwimu za 2002-2003.
 
Back
Top Bottom