Arusha ni Mji ulioachwa uharifu utambe

Arusha ni Mji ulioachwa uharifu utambe

Nimekaa sana majengo mapya karibu na ngarenaro mitaa ya chuo Cha sua.
Nimekaa Ngara mtoni.
Nimekaa Arumeru .
So Arusha naijua Sana Zaid ya Sana.
Kwanini matajiri wengi wanatokea Arusha kama watu wote Arusha ni wavuta bangi?
 
Nikiri kwamba mie kwa majukumu yangu ya kimaisha ni mtu ninayezunguka sana katika nchi hii na maeneo mengine ya Dunia ukipenda.

Arusha pamoja na kuwa na sifa za madhari nzuri, muingiliano wa watu wa mataifa mbalimbali, na taasisi mbalimbali za kimataifa, ukweli usemwe, Jiji hilo sio salama kabisa kwa maisha ya watu.

Arusha ndo mahali ambapo bangi inavutwa mahali popote, ni mahali ambapo watu wanatembea wakiwa wamechomekea visu kwenye nguo na vinaonekana, Arusha ndo watu wamejaa matusi ya nguoni na hakuna anayeshangaa.

Ukweli, Jiji hilo limejaa aina ya maovu ambayo mengi yake ukiyaona hakika yameruhusiwa na jamii yenyewe na vyombo vya Dola pia.

Kuna wakati najiuliza, hivi hii ni jamii Gani inayoogopa waovu kiwango hiki?

Ni kweli sitetei matumizi ya nguvu na kutofuata sheria, lakini ukweli ni kwamba, jamii ya Arusha, kwa sehemu kubwa ni jamii isiyozingatia maadili kabisa na ndo maana hata yanapofanyika matendo ya kijinai na uovu, bado utawaona watu wametulia tu na huoni kuteseka na kukereketwa kuzuia mambo ya kijinga ya viwango hivyo.

Kwa kuwa nimejitambulisha kama mtembezi, hapo ndo nawakumbuka watu kutoka kanda ya ziwa. " Jamii hailei mambo ya kijinga yaliyopitiliza kama yanayotendeka kwenye Jiji la Arusha.

Ni rahisi sana kushikwa na kutandikwa viboko hadharani na wananchi ukiwa baadhi ya maeneo kanda ya ziwa kwa sababu tu umetukana mama au mtu yeyote kinachoitwa matusi ya nguoni.

Kwa hiyo sitetei watu kuvunja sheria na kujichukulia sheria mikononi, lakini ukweli usemwe, " jamii haionekani hata kucahukia tu vitendo hivyo". Jamii ikianza kuonyesha hasira juu ya maovu na vitendo vyenye mwelekeo wa jinai, waovu na watu wanaojihusisha na mambo hayo wataogopa na kuacha au kuyafanya under cover na siyo waziwazi kama ilivyo.

Naiasa jamii ya Jiji la Arusha kubadili tabia na kuanza kuchukia aina ya matendo ya ovyo yanayoendelea jijini humo.

Kwa vyombo vya Dola, nashauri kuanza kufanya kazi zao nje ya mazoea.

Mazoea wanayofanya walinzi wetu wa amani, yatafanya jamii ianze kuishi bila kuogopa Sasa.

Uwepo wa majeshi huleta nidhamu katika jamii. Tatizo ninaloliona, uwepo wa majeshi ,Sasa unakuwa kama jambo la kawaida.

Hivi unawezaje ukiwa police, kupita mahali kwenye genge ambalo ukuta walioegemea au ukipenda kwenye kijiwe, kumechorwa picha za wavuta bangi na watu wanaovuta bangi na hata huulizi au kulazimisha magenge na vijiwe hivyo kutoweka?

Inawezekanaje ,kondakta wa gari anakutana na traffic police, wanamsikia kabisa ananuka bangi na bado hawawezi kumkamata na kumpeleka kituoni akajibu kwa Nini ananuka bangi?

Tukio lililotokea Jana la kuuawa wa kijana anayeitwa Ally Dangote, kwangu Mimi pamoja na kwamba kauawa lakini limekuja kwa kuchelewa. Kijana mwenye umri wa miaka 19 anawezaje kutamba kwenye jamii inayochukia uovu muda wote huo?

Inawezekana vipi mtu anasumbua na kuua watu hadharani Ili hali wananchi wanajua anakoishi, anachofanya na anapatikanaje? Police na vyombo vya Dola, vinawezaje kuacha mwovu anatamba karibu mwezi mzima akiua watu hadharani?

Nini maana ya uwepo wetu kama wananchi na vyombo vya Dola?

Wakati Fulani nilipatwa na taharuki nikiwa maeneo Fulani ya Jiji hilo.

Na ilikuwa hivi ," Kuna kijana mmoja aliyekuwa mwendesha pikipiki aliuawa kwa mazingira ya kugongwa na gari" sekeseke lilikuja siku ambayo kijana yule alikuwa anapelekwa mazikoni. Believe me, barabara ilichafuka. Pikipiki zilijaa barabara nzima kana kwamba mji umetekwa na boda boda, barabara ni zao na hakuna mwingine anayezitumia..

Ungewaona vijana wameshikilia chupa za pombe barabarani, wanakunywa pombe wakati wanaendesha pikipiki.

Ajabu ilifika mahali , wengine walikuwa wanabishana kwa maneno, hivyo wanachofanya ni kutelemka kwenye boda na wengine bajaji, wanapigana ngumi, huku magari ya abiria na watumiaji wengine wa magari wakiwa wanasubiri ugomvi uishe.

Pale nilipokuwa, nilishuhudia ugomvi unaisha wenyewe kwa wao kujiamua.

Sikuoni raia hata kulalamikia tu, waendesha magari wako kwenye magari wanasubiri nao bodaboda wamalize ugomvi wao.

Mbaya zaidi hakuna police waliokuja kuondoa hiyo bughudha, achilia ukweli kwamba kituo Cha police kilikuwa kama mita 200 tu kutoka eneo la tukio na magari yenyewe yalikuwa msururu mpaka eneo la kituo.

Hebu nambie katika mazingira hayo, huu uovu haujaruhusiwa?

Watu wa Arusha ni waoga hata kukemea tu ujinga. Wanajifanya wako busy kutafuta pesa. Wamejaa ulevi wa kutafuta Mali ambazo zinaibwa kijinga na watu wanaowalea kwa kuruhusu tambia mbaya kutamalaki.

Vyombo vya Dola na hasa police, woke up please.

Huu mji Sasa unataka aina nyingine ya ku curb criminality ambayo naiona inanyemelea mji huu.

Huu mji unataka psychology ya askari kubadilika Sasa. Huu mji unataka upolisi hasa na siyo kucheza na viashiria vya uhalifu.

Magenge yaliyotapakaa Kila mahali kama vijiwe yachunguzwe na yapigwe marufuku.

Unywaji wa mapombe usio na mipaka unazaa uharifu uliyopitiliza kwa kudhani Hawa ni walevi tu.

Yuko wapi RPC wa aina ya Kombe miaka ile? We need a serious police force , if at all, we want to defeat the rampant criminality hovers the city of Arusha.
Huwa nikiwaonaga vijana wa Arusha na uhuni wao wa kitoto....Nawaona kama wana kaushamba flani ivi.
 
Huwa nakosa amani ninapokuwa nazunguka mitaani jijini Arusha.

Nadhani vijana wavuta bangi wamekuwa wazee na wamezaa watoto ambao pia ni wavuta bangi (ambao wengi ni bodaboda hivi sasa). Hivyo jamii nzima ya jiji hilo inavuta bangi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nikiwa Arusha huwa najihisi nipo Jo'burg huko SA. Uhai wako mara zote huna uhakika nao . Muda wote unaweza kupata madhara usiyoyatarajia. Utashangaa pale unapopita mitaani na bangi inauzwa bila wasiwasi na pia uvutaji wake ni nje nje. Hakika Arusha inatisha.
 
Arusha vijana wanatukana matusi makubwa kwenye vituo vya Hiace balaa tena watu wazima kabisaa yaani Arusha kutukana ni moja ya kuonekana mjanja...Road mtu akiomba fair tu kidogo aingie bara bara kubwa hawatoi na magari mjini hayaishi ukitoa pua kuomba utatukanwa mbaya harafu ukimuangalia huyo anaetukana hafananiii na hayo matusi unabaki kuwaangalia tu kwa watu wenye hasira za haraka Arusha unaenda jela dakika chache tu hao Wanafunzi watu hawawajali kabisa madereva wachache usimama kuwapisha wapite wengine huwa wanapiga hadi honi kwenye Zebra wewe ukisimama wanakupigia honi muda wao wote wao ni wa kuwahi tu kwa sababu ya matumizi ya miraa na Bangi yapo juu mno...
 
Nikiwa Arusha huwa najihisi nipo Jo'burg huko SA. Uhai wako mara zote huna uhakika nao . Muda wote unaweza kupata madhara usiyoyatarajia. Utashangaa pale unapopita mitaani na bangi inauzwa bila wasiwasi na pia uvutaji wake ni nje nje. Hakika Arusha inatisha.
Hakuna sehemu Arusha utafananisha na SA bhana acha zako Arusha maduka yapo wazi mpaka saa sita usiku ni sehemu gani jo'burg utakuta duka la mtaani lipo wazi saa sita usiku pana maduka mawili ya dawa Arusha hayafungwi ni masaa 24 Jo'burg ambayo dakika yeyote Mall inavamiwa ufananishe na haya maeneo ambayo kiwango cha uharifu ni kidogo mno...
 
Arusha hakuna uhalifu wa kutisha kama mleta mada anavyotaka ionekane.

Kuna mikoa kama Mara , mbeya , kagera, uhalifu pia upo sana tatizo la watanzania ni kuishi kwa matukio.

Hili la Aly Dangote basi mleta mada akaona aingize ujuaji wake humo.

Ungefika Colombia au Mexico nadhani ungekua na habari tofauti.
 
Umeandika Mambo mengi ya maana.
Kwa kuongezea Arusha ni mji unaoishi Kijima katika Ulimwengu wa kisasa. Arusha ni washamba wablnaoishi Karne ya 18 ndani ya Karne ya 21. Nasema hivyo Kwa sababu generations za binadamu zinatengenezwa na maendeleo na ustaarabu. Lakini Arusha wanafanya maendeleo bila ustaarabu. Hata ukikutana na Mzee mwenye uwezo wa kiuchumi Arusha Hana utaarabu, ana ubabe wa kishamba na kizamani. Ikiwasikia kina Monaban, Molel, Masawe, Mrema nk, Tabia zào ni za ovyo utadhani Makuli wakati ni watu wazima na hela zao. Kiufupi Survival of the fittest inajionyesha Arusha kuliko mji wowote na serikali imebariki huo ujinga.
Naiona akili kubwa katika andiko hili. Nakukubalia kabisa.
 
Nikiri kwamba mie kwa majukumu yangu ya kimaisha ni mtu ninayezunguka sana katika nchi hii na maeneo mengine ya Dunia ukipenda.

Arusha pamoja na kuwa na sifa za madhari nzuri, muingiliano wa watu wa mataifa mbalimbali, na taasisi mbalimbali za kimataifa, ukweli usemwe, Jiji hilo sio salama kabisa kwa maisha ya watu.

Arusha ndo mahali ambapo bangi inavutwa mahali popote, ni mahali ambapo watu wanatembea wakiwa wamechomekea visu kwenye nguo na vinaonekana, Arusha ndo watu wamejaa matusi ya nguoni na hakuna anayeshangaa.

Ukweli, Jiji hilo limejaa aina ya maovu ambayo mengi yake ukiyaona hakika yameruhusiwa na jamii yenyewe na vyombo vya Dola pia.

Kuna wakati najiuliza, hivi hii ni jamii Gani inayoogopa waovu kiwango hiki?

Ni kweli sitetei matumizi ya nguvu na kutofuata sheria, lakini ukweli ni kwamba, jamii ya Arusha, kwa sehemu kubwa ni jamii isiyozingatia maadili kabisa na ndo maana hata yanapofanyika matendo ya kijinai na uovu, bado utawaona watu wametulia tu na huoni kuteseka na kukereketwa kuzuia mambo ya kijinga ya viwango hivyo.

Kwa kuwa nimejitambulisha kama mtembezi, hapo ndo nawakumbuka watu kutoka kanda ya ziwa. " Jamii hailei mambo ya kijinga yaliyopitiliza kama yanayotendeka kwenye Jiji la Arusha.

Ni rahisi sana kushikwa na kutandikwa viboko hadharani na wananchi ukiwa baadhi ya maeneo kanda ya ziwa kwa sababu tu umetukana mama au mtu yeyote kinachoitwa matusi ya nguoni.

Kwa hiyo sitetei watu kuvunja sheria na kujichukulia sheria mikononi, lakini ukweli usemwe, " jamii haionekani hata kucahukia tu vitendo hivyo". Jamii ikianza kuonyesha hasira juu ya maovu na vitendo vyenye mwelekeo wa jinai, waovu na watu wanaojihusisha na mambo hayo wataogopa na kuacha au kuyafanya under cover na siyo waziwazi kama ilivyo.

Naiasa jamii ya Jiji la Arusha kubadili tabia na kuanza kuchukia aina ya matendo ya ovyo yanayoendelea jijini humo.

Kwa vyombo vya Dola, nashauri kuanza kufanya kazi zao nje ya mazoea.

Mazoea wanayofanya walinzi wetu wa amani, yatafanya jamii ianze kuishi bila kuogopa Sasa.

Uwepo wa majeshi huleta nidhamu katika jamii. Tatizo ninaloliona, uwepo wa majeshi ,Sasa unakuwa kama jambo la kawaida.

Hivi unawezaje ukiwa police, kupita mahali kwenye genge ambalo ukuta walioegemea au ukipenda kwenye kijiwe, kumechorwa picha za wavuta bangi na watu wanaovuta bangi na hata huulizi au kulazimisha magenge na vijiwe hivyo kutoweka?

Inawezekanaje ,kondakta wa gari anakutana na traffic police, wanamsikia kabisa ananuka bangi na bado hawawezi kumkamata na kumpeleka kituoni akajibu kwa Nini ananuka bangi?

Tukio lililotokea Jana la kuuawa wa kijana anayeitwa Ally Dangote, kwangu Mimi pamoja na kwamba kauawa lakini limekuja kwa kuchelewa. Kijana mwenye umri wa miaka 19 anawezaje kutamba kwenye jamii inayochukia uovu muda wote huo?

Inawezekana vipi mtu anasumbua na kuua watu hadharani Ili hali wananchi wanajua anakoishi, anachofanya na anapatikanaje? Police na vyombo vya Dola, vinawezaje kuacha mwovu anatamba karibu mwezi mzima akiua watu hadharani?

Nini maana ya uwepo wetu kama wananchi na vyombo vya Dola?

Wakati Fulani nilipatwa na taharuki nikiwa maeneo Fulani ya Jiji hilo.

Na ilikuwa hivi ," Kuna kijana mmoja aliyekuwa mwendesha pikipiki aliuawa kwa mazingira ya kugongwa na gari" sekeseke lilikuja siku ambayo kijana yule alikuwa anapelekwa mazikoni. Believe me, barabara ilichafuka. Pikipiki zilijaa barabara nzima kana kwamba mji umetekwa na boda boda, barabara ni zao na hakuna mwingine anayezitumia..

Ungewaona vijana wameshikilia chupa za pombe barabarani, wanakunywa pombe wakati wanaendesha pikipiki.

Ajabu ilifika mahali , wengine walikuwa wanabishana kwa maneno, hivyo wanachofanya ni kutelemka kwenye boda na wengine bajaji, wanapigana ngumi, huku magari ya abiria na watumiaji wengine wa magari wakiwa wanasubiri ugomvi uishe.

Pale nilipokuwa, nilishuhudia ugomvi unaisha wenyewe kwa wao kujiamua.

Sikuoni raia hata kulalamikia tu, waendesha magari wako kwenye magari wanasubiri nao bodaboda wamalize ugomvi wao.

Mbaya zaidi hakuna police waliokuja kuondoa hiyo bughudha, achilia ukweli kwamba kituo Cha police kilikuwa kama mita 200 tu kutoka eneo la tukio na magari yenyewe yalikuwa msururu mpaka eneo la kituo.

Hebu nambie katika mazingira hayo, huu uovu haujaruhusiwa?

Watu wa Arusha ni waoga hata kukemea tu ujinga. Wanajifanya wako busy kutafuta pesa. Wamejaa ulevi wa kutafuta Mali ambazo zinaibwa kijinga na watu wanaowalea kwa kuruhusu tambia mbaya kutamalaki.

Vyombo vya Dola na hasa police, woke up please.

Huu mji Sasa unataka aina nyingine ya ku curb criminality ambayo naiona inanyemelea mji huu.

Huu mji unataka psychology ya askari kubadilika Sasa. Huu mji unataka upolisi hasa na siyo kucheza na viashiria vya uhalifu.

Magenge yaliyotapakaa Kila mahali kama vijiwe yachunguzwe na yapigwe marufuku.

Unywaji wa mapombe usio na mipaka unazaa uharifu uliyopitiliza kwa kudhani Hawa ni walevi tu.

Yuko wapi RPC wa aina ya Kombe miaka ile? We need a serious police force , if at all, we want to defeat the rampant criminality hovers the city of Arusha.

Ndo wote mnasumbuliwa na kakijana ka miaka 19 hadi mnafanya sherehe kameuwawa? Mnasikitisha sana wazee, mjitafakari!
 
Arusha hakuna uhalifu wa kutisha kama mleta mada anavyotaka ionekane.

Kuna mikoa kama Mara , mbeya , kagera, uhalifu pia upo sana tatizo la watanzania ni kuishi kwa matukio.

Hili la Aly Dangote basi mleta mada akaona aingize ujuaji wake humo.

Ungefika Colombia au Mexico nadhani ungekua na habari tofauti.
@ stroke, sijaelewa wewe unaposikia uhalifu unaelewa nini? Maana ya andiko langu haikuwa kufanya comparative analysis na uhalifu mwingine ulioko mahali pengine . Nataka tuuone uhalifu kama uhalifu. Hiyo magnitude ya uhalifu unayoitaka utaipata tu siku Moja wakati unaacha viashiria vinavyotupeleka kwenye uhalifu mkubwa pasipo kuthibitiwa.
 
Hakuna sehemu Arusha utafananisha na SA bhana acha zako Arusha maduka yapo wazi mpaka saa sita usiku ni sehemu gani jo'burg utakuta duka la mtaani lipo wazi saa sita usiku pana maduka mawili ya dawa Arusha hayafungwi ni masaa 24 Jo'burg ambayo dakika yeyote Mall inavamiwa ufananishe na haya maeneo ambayo kiwango cha uharifu ni kidogo mno...
Kwa hiyo unataka uhalifu ufikie kiwango Cha Johannesburg ndo uwe uhalifu? Yaani mtoto wako mpaka awe jambazi ndo ujue zile pesa alizokuwa anakuibia lilikuwa kosa? Uhalifu ni uhalifu tu. Acha kutaka kujisikia vizuri kwa kufanya comparative analysis.

Hata hivyo nikwambie tu, Jo ' burg kuwa wahalifu siyo kipimo Cha sisi kuwa wahalifu pia . Two mistakes can't make one right!
 
@ stroke, sijaelewa wewe unaposikia uhalifu unaelewa nini? Maana ya andiko langu haikuwa kufanya comparative analysis na uhalifu mwingine ulioko mahali pengine . Nataka tuuone uhalifu kama uhalifu. Hiyo magnitude ya uhalifu unayoitaka utaipata tu siku Moja wakati unaacha viashiria vinavyotupeleka kwenye uhalifu mkubwa pasipo kuthibitiwa.
kumbuka " Two mistakes can't make one right" naomba uisome hii @ stroke .
 
We semaaaaaa lkn personally I love Arusha!
We also love it ,so to speak. The only difference between us is how we perceive things. Justifying the elements of criminality as you try to do, won't be doing justice upon this beautiful city.
 
Unaongea as if hakuna Panya road.

Nina wasiwasi na haya maoni yako maana yamejaa bias.

Wakazi wa Arusha ndo watalalamika.

Otherwise pita na shughuli yako kaishi unapopaona ni salama kama huko kanda ya ziwa ulipopasema. Ambapo watu wanatandika wenzao viboko.
Kuwa kwa panya road mahali kwingine, hakuhalalishi , uhalifu huko Arusha nilipopasema. Kumbuka wahenga husema, kosa Moja halilahalishi kosa lingine mahali pengine au ukipenda " Two mistakes can't make one right".
 
Acha ujinga. Mtu ambaye hayupo Arusha au hajawahi kufika Arusha akikusoma anaweza akakuamini. Arusha ni jiji salama sana hapa nchini.
Hakuna bangi ikiyotapakaa.
Hakuna wahuni waliotapakaa.
Arusha ni patamu balaa.
Philips, Kijenge, Njiro, Lemara, Sakina, Mbauda, Kwa Morombo, Mjini Kati, Moshono, Chekereni, Ngulelo, Kimandolu, Sanawari, Mianzini, Kaloleni, Levolosi, Olmatejoo, Daraja Mbili, Tengeru, Ngaramtoni, Ngarenaro, Majengo: Kote kutamu balaa.
Kuna outskirts pia kama vile Ilboru, Ilkiurei, Kiserian, Kiranyi, Usa River, Mulangarini, Mwandent, Kisongo, Muriet, Olasiti..Kutamu balaa.
Arusha ni jiji bora kabisa la kuishi.
Hakuna tishio la kiusalama kama mleta mada anavyodai.
Chalii wa chuga umeandika undezi sana. Chuga ni pa kipumbavu na masela mavi wengi kuliko sehemu nyingine

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ningekuwa ninakipaji cha kuandika, ningekuwa nimeandika jambo kama hili muda mrefu sana.

Kuna wakati nafikiria kwanin serikali imeamua kuwa kimya kwa yanayoendelea A town??

1. Najiuliza, pengine ni mpango wa serikali?

2. Nazidi kujiuliza, kama serikali ina Wizara ya mambo ya ndani, kwanini Tarime walifanikiwa, na kwann Arusha wameshindwa?

3. Najiuliza, vyombo vya ulinzi havioni yanayoendelea Arusha?? POLICE NA TISS,

4. Kwanini mji ambao ni kitovu cha utalii Tanzania unakuwa nataharuki na mambo yanayohatarisha maisha ya Raia?

Masauni, fanya jambo Arusha, watu waishi kwa amani!
TISS wanachojua ni kupambana na upinzani
 
@ stroke, sijaelewa wewe unaposikia uhalifu unaelewa nini? Maana ya andiko langu haikuwa kufanya comparative analysis na uhalifu mwingine ulioko mahali pengine . Nataka tuuone uhalifu kama uhalifu. Hiyo magnitude ya uhalifu unayoitaka utaipata tu siku Moja wakati unaacha viashiria vinavyotupeleka kwenye uhalifu mkubwa pasipo kuthibitiwa.
Unazua taharuki kwa kuandika mambo ya kufikirika kwa kubebwa na tukio moja la Aly Dangote, sitakai uhalifu upo ila sio kwa kiwango unachokizungumzia hapa.

Mbona huko Arusha tukija tunafanya mishe zetu kwa amani kabisa??

Matukio kama haya yapo almost kila mkoa na tunayasikia kila mara kwa hiyo Arusha sio special case kama unavyotaka ionekane.
 
Kwa hiyo unataka uhalifu ufikie kiwango Cha Johannesburg ndo uwe uhalifu? Yaani mtoto wako mpaka awe jambazi ndo ujue zile pesa alizokuwa anakuibia lilikuwa kosa? Uhalifu ni uhalifu tu. Acha kutaka kujisikia vizuri kwa kufanya comparative analysis.

Hata hivyo nikwambie tu, Jo ' burg kuwa wahalifu siyo kipimo Cha sisi kuwa wahalifu pia . Two mistakes can't make one
Arusha ni Pepo kwa Jo'burg nina makazi Arusha nipo na familia ila Jo'burg ndio nakochukua magari isikie tuu SA maana wengine uharifu wao mnaona kwenye TV baadhi ya Gari ili ifike Mpaka wa Botswana/SA mnaisindikiza ili majambazi wasije kuivamia na muda mwingine nanyi mnatakiwa kuwa na siraha matukio yalipo SA pana muda unaweza kudhani hawa jamaa sio binadamu kama sisi na hilo gari unalolisindika lina karibu tracker za Kampuni mbili au tatu tofauti...Arusha hii nazunguka muda wowote usiku na popote ufananishe na Thembisa,Soweto, Mamelodi hata CBD yenyewe wahuni wanakukaba ukigoma unauawa muda huo huo na wezi wapya kila siku wanaingia mjini tofauti na miaka ya nyuma ukiwajua wezi unaweza kupita baadhi ya maeneo sasa hivi anaekujua ndio anakunyooshea kidole kwa wezi usiowajua yule nendeni mkachukue hela...SA na usizwa wangu wote nina muda lazima niwe ndani tena mapema tuu maana kufa ni dakika moja na watu hata hawashangai wanajua umekanyaga katiba...
 
Back
Top Bottom