Arusha ni Mji ulioachwa uharifu utambe

Arusha ni Mji ulioachwa uharifu utambe

Arusha ni Pepo kwa Jo'burg nina makazi Arusha nipo na familia ila Jo'burg ndio nakochukua magari isikie tuu SA maana wengine uharifu wao mnaona kwenye TV baadhi ya Gari ili ifike Mpaka wa Botswana/SA mnaisindikiza ili majambazi wasije kuivamia na muda mwingine nanyi mnatakiwa kuwa na siraha matukio yalipo SA pana muda unaweza kudhani hawa jamaa sio binadamu kama sisi na hilo gari unalolisindika lina karibu tracker za Kampuni mbili au tatu tofauti...Arusha hii nazunguka muda wowote usiku na popote ufananishe na Thembisa,Soweto, Mamelodi hata CBD yenyewe wahuni wanakukaba ukigoma unauawa muda huo huo na wezi wapya kila siku wanaingia mjini tofauti na miaka ya nyuma ukiwajua wezi unaweza kupita baadhi ya maeneo sasa hivi anaekujua ndio anakunyooshea kidole kwa wezi usiowajua yule nendeni mkachukue hela...SA na usizwa wangu wote nina muda lazima niwe ndani tena mapema tuu maana kufa ni dakika moja na watu hata hawashangai wanajua umekanyaga katiba...
Mleta mada anaandika vitu vya kufikirika.

Arusha tunakuja na tunafanya mambo yetu mpaka mida mibovu kwa amani kabisa.

Anakuja na stori zake za kutunga tunga hapa.
 
Kwa hiyo unataka uhalifu ufikie kiwango Cha Johannesburg ndo uwe uhalifu? Yaani mtoto wako mpaka awe jambazi ndo ujue zile pesa alizokuwa anakuibia lilikuwa kosa? Uhalifu ni uhalifu tu. Acha kutaka kujisikia vizuri kwa kufanya comparative analysis.

Hata hivyo nikwambie tu, Jo ' burg kuwa wahalifu siyo kipimo Cha sisi kuwa wahalifu pia . Two mistakes can't make one right!
Jo'burg polisi wakikukamata na hela nyingi wanaua tuu kama huko Mtwara na kwingineko Dunia ni ile ile Mkuu na watu ni wale wale ni kweli Arusha ina matukio ya Ujambazi sana tena vijana wetu hawa hawa na wanatukana sana ila usifananishe na huko SA pana matukio yapo SA yaliyotokea miaka kumi iliyopita Tanzania hayajawahi kutokea na hatuwezi kuongea hapa wacha iwe hivi hivi na matukio yetu ya kuibiana simu kwa kutumia boda boda mjini au maeneo mengine...
 
Mleta mada anaandika vitu vya kufikirika.

Arusha tunakuja na tunafanya mambo yetu mpaka mida mibovu kwa amani kabisa.

Anakuja na stori zake za kutunga tunga hapa.
Watu wanafanya biashara usiku mkubwa na zinaenda...bar nyingi Arusha usiku zinakua zimejaa kungekua na uharifu watu wangekaa nje?
 
Nikiri kwamba mie kwa majukumu yangu ya kimaisha ni mtu ninayezunguka sana katika nchi hii na maeneo mengine ya Dunia ukipenda.

Arusha pamoja na kuwa na sifa za madhari nzuri, muingiliano wa watu wa mataifa mbalimbali, na taasisi mbalimbali za kimataifa, ukweli usemwe, Jiji hilo sio salama kabisa kwa maisha ya watu.

Arusha ndo mahali ambapo bangi inavutwa mahali popote, ni mahali ambapo watu wanatembea wakiwa wamechomekea visu kwenye nguo na vinaonekana, Arusha ndo watu wamejaa matusi ya nguoni na hakuna anayeshangaa.

Ukweli, Jiji hilo limejaa aina ya maovu ambayo mengi yake ukiyaona hakika yameruhusiwa na jamii yenyewe na vyombo vya Dola pia.

Kuna wakati najiuliza, hivi hii ni jamii Gani inayoogopa waovu kiwango hiki?

Ni kweli sitetei matumizi ya nguvu na kutofuata sheria, lakini ukweli ni kwamba, jamii ya Arusha, kwa sehemu kubwa ni jamii isiyozingatia maadili kabisa na ndo maana hata yanapofanyika matendo ya kijinai na uovu, bado utawaona watu wametulia tu na huoni kuteseka na kukereketwa kuzuia mambo ya kijinga ya viwango hivyo.

Kwa kuwa nimejitambulisha kama mtembezi, hapo ndo nawakumbuka watu kutoka kanda ya ziwa. " Jamii hailei mambo ya kijinga yaliyopitiliza kama yanayotendeka kwenye Jiji la Arusha.

Ni rahisi sana kushikwa na kutandikwa viboko hadharani na wananchi ukiwa baadhi ya maeneo kanda ya ziwa kwa sababu tu umetukana mama au mtu yeyote kinachoitwa matusi ya nguoni.

Kwa hiyo sitetei watu kuvunja sheria na kujichukulia sheria mikononi, lakini ukweli usemwe, " jamii haionekani hata kucahukia tu vitendo hivyo". Jamii ikianza kuonyesha hasira juu ya maovu na vitendo vyenye mwelekeo wa jinai, waovu na watu wanaojihusisha na mambo hayo wataogopa na kuacha au kuyafanya under cover na siyo waziwazi kama ilivyo.

Naiasa jamii ya Jiji la Arusha kubadili tabia na kuanza kuchukia aina ya matendo ya ovyo yanayoendelea jijini humo.

Kwa vyombo vya Dola, nashauri kuanza kufanya kazi zao nje ya mazoea.

Mazoea wanayofanya walinzi wetu wa amani, yatafanya jamii ianze kuishi bila kuogopa Sasa.

Uwepo wa majeshi huleta nidhamu katika jamii. Tatizo ninaloliona, uwepo wa majeshi ,Sasa unakuwa kama jambo la kawaida.

Hivi unawezaje ukiwa police, kupita mahali kwenye genge ambalo ukuta walioegemea au ukipenda kwenye kijiwe, kumechorwa picha za wavuta bangi na watu wanaovuta bangi na hata huulizi au kulazimisha magenge na vijiwe hivyo kutoweka?

Inawezekanaje ,kondakta wa gari anakutana na traffic police, wanamsikia kabisa ananuka bangi na bado hawawezi kumkamata na kumpeleka kituoni akajibu kwa Nini ananuka bangi?

Tukio lililotokea Jana la kuuawa wa kijana anayeitwa Ally Dangote, kwangu Mimi pamoja na kwamba kauawa lakini limekuja kwa kuchelewa. Kijana mwenye umri wa miaka 19 anawezaje kutamba kwenye jamii inayochukia uovu muda wote huo?

Inawezekana vipi mtu anasumbua na kuua watu hadharani Ili hali wananchi wanajua anakoishi, anachofanya na anapatikanaje? Police na vyombo vya Dola, vinawezaje kuacha mwovu anatamba karibu mwezi mzima akiua watu hadharani?

Nini maana ya uwepo wetu kama wananchi na vyombo vya Dola?

Wakati Fulani nilipatwa na taharuki nikiwa maeneo Fulani ya Jiji hilo.

Na ilikuwa hivi ," Kuna kijana mmoja aliyekuwa mwendesha pikipiki aliuawa kwa mazingira ya kugongwa na gari" sekeseke lilikuja siku ambayo kijana yule alikuwa anapelekwa mazikoni. Believe me, barabara ilichafuka. Pikipiki zilijaa barabara nzima kana kwamba mji umetekwa na boda boda, barabara ni zao na hakuna mwingine anayezitumia..

Ungewaona vijana wameshikilia chupa za pombe barabarani, wanakunywa pombe wakati wanaendesha pikipiki.

Ajabu ilifika mahali , wengine walikuwa wanabishana kwa maneno, hivyo wanachofanya ni kutelemka kwenye boda na wengine bajaji, wanapigana ngumi, huku magari ya abiria na watumiaji wengine wa magari wakiwa wanasubiri ugomvi uishe.

Pale nilipokuwa, nilishuhudia ugomvi unaisha wenyewe kwa wao kujiamua.

Sikuoni raia hata kulalamikia tu, waendesha magari wako kwenye magari wanasubiri nao bodaboda wamalize ugomvi wao.

Mbaya zaidi hakuna police waliokuja kuondoa hiyo bughudha, achilia ukweli kwamba kituo Cha police kilikuwa kama mita 200 tu kutoka eneo la tukio na magari yenyewe yalikuwa msururu mpaka eneo la kituo.

Hebu nambie katika mazingira hayo, huu uovu haujaruhusiwa?

Watu wa Arusha ni waoga hata kukemea tu ujinga. Wanajifanya wako busy kutafuta pesa. Wamejaa ulevi wa kutafuta Mali ambazo zinaibwa kijinga na watu wanaowalea kwa kuruhusu tambia mbaya kutamalaki.

Vyombo vya Dola na hasa police, woke up please.

Huu mji Sasa unataka aina nyingine ya ku curb criminality ambayo naiona inanyemelea mji huu.

Huu mji unataka psychology ya askari kubadilika Sasa. Huu mji unataka upolisi hasa na siyo kucheza na viashiria vya uhalifu.

Magenge yaliyotapakaa Kila mahali kama vijiwe yachunguzwe na yapigwe marufuku.

Unywaji wa mapombe usio na mipaka unazaa uharifu uliyopitiliza kwa kudhani Hawa ni walevi tu.

Yuko wapi RPC wa aina ya Kombe miaka ile? We need a serious police force , if at all, we want to defeat the rampant criminality hovers the city of Arusha.
We Arusha huijui, na wala hakuna nchi yoyote uloenda we endelea kukaa huko mashambani kwenu. Arusha iko salama kuliko unavyofikiri ndio maana mji umejaa wazungu na raia wa mataifa mbalimbali. Kinachikusumbua ni wivu tu na Geneva ya Africa
 
Huko hata wanawake wenye asili ya huko Wana tabia ya ukatiri.

Kuna demu Kaloleni tulizoeana ..Kuna siku hakuwa sawa me nikapita na Kama kawaida niliyozoea kumtania... Aliamka na pande la mlunda Bila kuguard R.I.P hii hapa.
 
Ni kweli uhalifu uko Kila mahali, nisichojua ni kama unatetea uhalifu kutamba badala ya kidhibitiwa!
Ukienda kituo cha polisi pale unakuta kesi za gongo ndio nyingi badala ya waharifu kweli unategemea nini zile defender muda wote zimebeba walevi wafike huko watoke kwa kuchangia unategemea matukio ya Ujambazi yatapungua kama watu wanaotakiwa kufanya hivyo hawafanyi kazi yao ipasavyo...
 
Kuwa kwa panya road mahali kwingine, hakuhalalishi , uhalifu huko Arusha nilipopasema. Kumbuka wahenga husema, kosa Moja halilahalishi kosa lingine mahali pengine au ukipenda " Two mistakes can't make one right".
Umeonyesha “bias” na malengo yako inawezekana siyo mazuri.

Sijasema kuwa kwa Panya road ndiyo sababu ya kuhalalisha “bias” yako. Wakazi wa Arusha hawana hizo shida unazozibebea bango.

For your info, it is “two wrongs don’t make one right “
 
Umeonyesha “bias” na malengo yako inawezekana siyo mazuri.

Sijasema kuwa kwa Panya road ndiyo sababu ya kuhalalisha “bias” yako. Wakazi wa Arusha hawana hizo shida unazozibebea bango.

For your info, it is “two wrongs don’t make one right “
mleta mada hakupaswa kuitaja kanda ya ziwa!

hapo ndo amekukosea japo amenena ukweli tupu

zee jinga sana wewe.
 
Hakuna sehemu Arusha utafananisha na SA bhana acha zako Arusha maduka yapo wazi mpaka saa sita usiku ni sehemu gani jo'burg utakuta duka la mtaani lipo wazi saa sita usiku pana maduka mawili ya dawa Arusha hayafungwi ni masaa 24 Jo'burg ambayo dakika yeyote Mall inavamiwa ufananishe na haya maeneo ambayo kiwango cha uharifu ni kidogo mno...
Asante kwa maoni yako. Nilijikita zaidi kwenye uvutaji wa ganja hadharani. Ila kwa usalama ktk kigezo cha Tanzania wengi wetu wanapaogopa kwa matukio mengi ya uhalifu.
 
Umeonyesha “bias” na malengo yako inawezekana siyo mazuri.

Sijasema kuwa kwa Panya road ndiyo sababu ya kuhalalisha “bias” yako. Wakazi wa Arusha hawana hizo shida unazozibebea bango.

For your info, it is “two wrongs don’t make one right “
Ni pale tu unapo entertain vitendo vya kihalifu ndo unaweza ona biasness yangu kama unavyofanya hapa.

Kimantiki hata sielewi unatetea nini? Je unatetea bangi kuvutwa hadharani? Unatetea watu kutembea na kuchomama visu hadharani? Unatetea maadili mabovu ya kutafuta pesa vyovyote hata kwa kukanyaga haki za wengine?

I will regard you to be one of the criminals if you persist on advocating wickedness such as this!

Nashukuru unajua kiingereza, ingawa sijui ukubwa wa msamiati ulionao. Sentensi ya kiingereza uliyoandika haina tofauti na niliyoandika unless kama ulikariri huo husemi mahali.
 
Asante kwa maoni yako. Nilijikita zaidi kwenye uvutaji wa ganja hadharani. Ila kwa usalama ktk kigezo cha Tanzania wengi wetu wanapaogopa kwa matukio mengi ya uhalifu.
Wanaopinga wangeenda kwenye vyombo vya usalama waeleweshwe ni miji Gani hapa kwetu yenye matukio makubwa ya uhalifu. Arusha imo kwenye orodha hiyo.

Wanaopinga tuwaambie ule usemi wa zamani" No Data/ research, no right to speak. Asante KUTATABHETAKULE.
 
We Arusha huijui, na wala hakuna nchi yoyote uloenda we endelea kukaa huko mashambani kwenu. Arusha iko salama kuliko unavyofikiri ndio maana mji umejaa wazungu na raia wa mataifa mbalimbali. Kinachikusumbua ni wivu tu na Geneva ya Africa
Ha ha ha ha ha ha. Mashambani ni kutamu saigilomagema. Kujaa watu hakumaanishi hakuna uhalifu ndugu yangu. Rafiki yako kasema hapa ,Jo' burg Kuna uhalifu kedekede, lakini bado kumejaa watu.

Hivi hujui kwamba Arusha Kuna kikosi maalumu Cha polisi Cha kulinda watalii?

Kwa Nini Kuna tourist police unit? Simple, wizi na uhalifu ulikuwa umekithiri dhidi ya watalii. Sijajua unatetea nini hata kama uhalifu ungekuwa na kiwango kidogo kulinganisha na kwingine ? Narudia, uhalifu ni uhalifu tu.
 
Ni pale tu unapo entertain vitendo vya kihalifu ndo unaweza ona biasness yangu kama unavyofanya hapa.

Kimantiki hata sielewi unatetea nini? Je unatetea bangi kuvutwa hadharani? Unatetea watu kutembea na kuchomama visu hadharani? Unatetea maadili mabovu ya kutafuta pesa vyovyote hata kwa kukanyaga haki za wengine?

I will regard you to be one of the criminals if you persist on advocating wickedness such as this!

Nashukuru unajua kiingereza, ingawa sijui ukubwa wa msamiati ulionao. Sentensi ya kiingereza uliyoandika haina tofauti na niliyoandika unless kama ulikariri huo husemi mahali.
Huwezi kujuwa natetea nini kwasababu sitetei chochote.

Wewe umesema natetea na kuhalalisha uhalifu wa hao wa Arusha unaowasema kwa kutaja Panya road.

Wewe hauishi Arusha lakini unapiga kelele kuliko watu wa Arusha. Si ukae huko kanda uliposema watu wanachapwa viboko?

Na kule Panya road nao wachapwe viboko?

Unasema nimekariri wakati ni usemi wenye originality yake umeusema kwa namna ambayo ni ndivyo sivyo na wala haukuwa na mantiki kwenye hoja yangu. Wewe ndo utakuwa umekariri kwasababu haujui matumizi yake.

You regard me as a crimina? Wewe ni flight attendant?

Watu wa Arusha wangekuwa wamezoea hayo unayosema, wasingelalamika kuhusu vitendo vya kihalifu vya Ally Dangote.

Tumia akili kama unayo.
 
Arusha hakuna uhalifu wa kutisha kama mleta mada anavyotaka ionekane.

Kuna mikoa kama Mara , mbeya , kagera, uhalifu pia upo sana tatizo la watanzania ni kuishi kwa matukio.

Hili la Aly Dangote basi mleta mada akaona aingize ujuaji wake humo.

Ungefika Colombia au Mexico nadhani ungekua na habari tofauti.
Mkuu, kujifananisha na Mexico au Colombia sio sahihi! Criminal rate kuwa kubwa katika izo Nchi inachagizwa na Biashara ya madawa ya kulevya na makundi mengi ya kihalifu.

Je lengo lako unataka tufikie hali hiyo ndio Serikali ichukue hatua.

Ni muhimu kudhibi uhalifu kabla haujaota miziz kama ilivyo kwa Mexico, Colombia, Paraguay na Brazil.
 
Nimesoma na jamaa mmoja chuo alikua ni mchuga ,yaan muda wote kiunoni Ana kisu .
Kwenye bag lake yamejaa maminyororo, Rungu ,viwembe had nikawa nashangaa silaha zote hizi za nini?

Matusi Sasa ni Kama breakfast ,yaan kijana alikua anatukana hovyo na huna chakumfanya.
Mirungi ,bangi ,mipombe na mifegi kwake ni Kama mswaki..

Alafu alikua anajifanya mtu wa mbele huko New York City ,mziki anafungulia anavyotaka mihip hop migumu ya huko mambele.

Sema Mimi damu ziliendana Sana baada ya cku moja kuwashiana pira ile mbaya .Nikamweleza kabisa Mimi ni Mtoto wa Mbeya mnyakyusa pure huwez kunitisha kindez watishe wajinga wengine.

Tokea hapo tulikua marafiki Sana na alikua ananidownlodia Sana ma movie na kunipa games kibao kwenye pc yangu maana jamaa alikua mtundu Sana wa Mambo ya IT.
Nilichogundua watu wa chuga wanajiona unique Sana na hawatak kufananishwa na mtu mwingine wakat uhalisia haupo hivo maana ni makima tu Kama walivyo makima wengine.
Then wanaishi maisha yakusadikika Sana kuliko uhalisia wenyew.

Askar wafanye Kaz ya kufa mtu ili kiwabadili mindsets walizojisetia na kujikatia kipande Chao ndani ya hii nchi.
Nilivyokuwa chuo Kuna binti wa chuga alikuwa anapigana na watu ovyo, kidogo tu mkono, mpaka alirudishwa nyumbani.
 
Back
Top Bottom