Arusha na Moshi kuna shida gani hasa kiroho?

Arusha na Moshi kuna shida gani hasa kiroho?

Matukio mengi ya kutisha na kushangaza mkoani Arusha yanatafsiriwa na jamii kwa mitazamo miwili tofauti

imani za kiroho/giza (kama vile ushirikina na laana) na sababu halisi za kijamii na kisaikolojia.

Mkoa wa Arusha umekuwa ukigonga vichwa vya habari kwa matukio ya ukatili uliopindukia, ikiwemo mauaji ya kutumia silaha kali kama visu, visasi vya kinyama, na ukatili wa kijinsia.
Ripoti za hivi karibuni za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) hata zinautaja mkoa huo kuongoza kwa matukio ya ukatili kwa watu wazima.

Ninini kinachoendelea nyuma ya matukio haya?

Ukigawanywa katika mitazamo ya kiroho na uhalisia wa kijamii Utagundua yafuatayo..

1. Mtazamo wa Kiroho na Imani za Giza
Katika fikra za wenyeji na watu wengi wa kiroho, mfululizo wa matukio ya kinyama Arusha unahusishwa na mambo yafuatayo:
"Roho ya Umwagaji Damu" (Laana ya Ardhi)
Kuna imani kwamba baadhi ya maeneo yana vizuizi au "madhabahu za giza" zilizojengwa kutokana na historia ya visasi au umwagaji damu wa tangu zamani.

Damu inayomwagika inatajwa "kuisumbua ardhi" na kuvuta roho za hasira na ukatili.
Ushirikina na Kupatwa na Pepo
Baadhi ya mauaji ya ajabu (kama ya ndugu wa karibu au watu kukatwa viungo) mara nyingi huhusishwa na imani za kishirikina za kusaka utajiri wa haraka au nguvu za giza.

Mmomonyoko wa Hofu ya Mungu
Viongozi wa dini mkoani humo wanasisitiza kuwa jamii imegeuka nyuma na kuacha misingi ya kiroho, jambo linalofungua milango kwa nguvu za uovu kutawala akili za vijana.
Nimeish Arusha miaka 5,haya yanayotokea leo hii ni matokeo ya mmongonyoko wa maadil wa muda mrefu ambao ulifumbiwa macho na serikal na wazaz pia.

Nan asiyeijua Arusha kwa sifa zake za BANGI nzuri( Cha Arusha)?,bangi zinavutwa hovyo bila woga,mirungi inachanjwa openly yan chuga ni kama jamaica ndogo,hapo hujagusia suala la watoto kuvuta gundi za viatu yan kifup Arusha vichaa ni wengi mno.

Alipoingia Makonda nikasema chuga itanyooka,nikashangazwa makonda akawa anacheza ngoma ya vijana,yale makund ya vichaa yakawa praised,wakawa wanapewa mpaka hela,hapo ndo ikawa balaa mana walikua wanapewa mpaka airtime kwenye Tv kubwa tu.

Haya yanayotokea sio issue ya mungu,ni jamii na serikal imeshindwa kuwasimamia vijana,vijana wanajiendesha wenyewe,weng ni vichaa kwasabau bangi,gongo,pombe kal za bei rahis zipo free kabisa,yan kijana akiwa na Mia 500 ni tosha kuamsha ubongo na bidhaa zinapatikana Kila mahali mpaka mashuleni,sokoni,stand mpaka majumban..Hakuna wakuwaongoza vijana ni kama vile tumewaachia wajitawale,hakuna SERA ZA VIJANA,MIONGOZO,DIRA...badala yake nchi inaongozwa na BETTING,SPORTS,UCHAWA,SIASA.
 
1000330454.png
 
Back
Top Bottom