Chademakwanza,
Point of correction Pls siyo tyer ni tyre.
Pia sijaona Lema nini amekufanya hapo Arusha let's be sincere and open kweli miaka mitano kukomboa kiwanda hata kazi hakijaanza kweli inatosha kwa miaka mitano?
Lema hujafanya chochote kwa kweli hata mbunge Wangu wa Iramba Magharibi Mh Mwigulu kafanya mengi sana mfano vijijini umeme vijiji 46 Sasa vikikamilika 89% Ya Iramba itakuwa na umeme, vituo vya afya 4, zahanati 9, barabara Sasa kila corner Ya Iramba inapitika, maji vijiji 13, CHF ndio kinara Iramba, food security 100%, ufaulu umeongezeka primary na secondary, Sasa sekondari inahitajika walimu 120 tu Kati Ya hao 74 wa Sayansi kumaliza tatizo la walimu kabisa.
Viwanda vidogovidogo 53 vya kukamua Alizeti vipo kila kijiji na tayari vimeanza kazi na vi kubwa viwili vya Ndago na Ulemo ambayo jumla Ya vijana 600 wataajiriwa.
Hayo ndio mambo Ya kuwaambia wananchi siyo ambulance tena Ya kufikirika kweli? Mwigulu katoa ambulance 2 na kazi zinafanya Sasa! Acha USANII Lema kama huwezi siasa kaa mbali na kamwe usidanganye watu maana mwisho wa siku watajua na watakuchukia milele