Godbless Lema: CHADEMA imepata baraka kuondokewa na Lowassa

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,438
2,000
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kurejea CCM.

Lema amedai kuwa uamuzi wa Lowassa unadhihirisha kuwa ameweka mbele maslahi yake binafsi kuliko mabadiliko aliyokuwa anayahubiri alipoingia Chadema.

Alidai kuwa Lowassa alifikia uamuzi huo ili kulinusuru shamba lake linaloshikiliwa Mkoani Tanga, shamba lake la mifugo linaloshikiliwa Dodoma pamoja na kumnusuru mkwewe Sioi Sumari na kifungo dhidi ya kesi inayomkabili.

Sumari anatuhumiwa kwa kula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kughushi pamoja na utakatishaji wa fedha.

“Mtu huyu alitaka kuwa Rais, hali ya kisiasa ilivyo sasa watu wapo magerezani, wanapata misukosuko ya kibiashara, hawana cha kuipa CCM ili wapate ahueni, lakini kwa sababu yeye anacho cha kuwapa CCM ilia pate amani. Hajaona gharama ya kufanya hivyo,” Lema amekaririwa na Gazeti la Mwananchi

“Chadema imepata baraka kuondokewa na mtu kama huyu. Alikuja kwa ajili ya kutaka urais na sio mabadiliko aliyokuwa akiyanadi. Nchi inataka demokrasia, katiba mpya, sheria mpya na inakabiliwa na ubanaji wa vyombo vya habari… mwanasiasa makini hawezi kuungana na CCM,” aliongeza.

Lowassa alijiunga na Chadema mwaka 2015 baada ya jina lake kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha watu waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Aligombea urais na kuleta ushindani mkubwa dhidi ya Dkt. John Magufuli wa CCM.

Juzi alipokewa na Dkt. Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lowassa alieleza kwa ufupi kuwa amerejea nyumbani. Alipokewa katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 
Kagemro

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
1,395

😬😬😬😬😬😬😬😬😬😬😬😬😬😬😬
 
thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,117

Bado hamjasema,ongeeni yote,bila kusahau idadi ya wabunge na kura za urais alizowapatia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
5,612

Lowasa, Malaya wa siasa. Amejiaibisha mno.
 
dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,399
2,000
Naendelea kusisitiza kwamba Lowassa ni fisadi. Alipojiunga CHADEMA alipigwa sala ya toba, Mungu akamsamehe. Sasa ameamua kurudi kwa mafisadi wenzie aliowaacha, uvumilivu umemshinda. Sasa ajiandae gadhabu ya Mungu inaenda kumshukia. Mungu huwa hadhihakiwi.

Unafanya toba na kusema umebadilika hadi unazungusha mikono. Mungu nakuruhusu umshughurikie Lowasaa na kizazi chake. Kafanya ufisadi hadi nywele zimekuwa nyeupe.
 
jani

JF-Expert Member
Aug 8, 2011
854
1,000
“Chadema imepata baraka kuondokewa na mtu kama huyu. Alikuja kwa ajili ya kutaka urais na sio mabadiliko aliyokuwa akiyanadi. Nchi inataka demokrasia, katiba mpya, sheria mpya na inakabiliwa na ubanaji wa vyombo vya habari… mwanasiasa makini hawezi kuungana na CCM,” aliongeza.
.
hahahahaha...ohooooooooooo....kumbe alikuja kuufuata uraisi, alafu mkawaweka pembeni waliokua wa maana...mkampa kupeperusha bendera kugombea nafasi ya juu kuliko zote.....sasa nani tumuogope hapa...yeye au chama kilicho ruhusu yote haya yatokee na kushindwa kufanya lolote mpaka alivyojitoa mwenyewe....? samahani lakini
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,405
2,000
Bado hamjasema,ongeeni yote,bila kusahau idadi ya wabunge na kura za urais alizowapatia

Sent using Jamii Forums mobile app

Napenda kumuita Lema ni mnafiki wa kiwango kikubwa sana, tena bora akakaa kimya. Yeye na viongozi wenzake wa cdm ndio walimpokea Lowassa baada ya kupokea hela yake na kumsafisha, leo ndio anatoka na lugha za kipuuzi eti shamba sijui ujinga gani.kwani walipompokea huku sisi tukisema ni makosa hayo anayosema leo alikuwa hayajui?

Hakuna kura wala idadi ya wabunge tuliopatiwa na Lowassa kwani alikuwa na miezi miwili tu ndani ya cdm, hata bila yeye cdm ingepata kura na viti vingi na chama kingebaki na heshima yake. Kama yeye ndio alileta hizo kura akiwa na miezi miwili, aliongeza wabunge wangapi akiwa na miaka mitatu ndani ya cdm? Acha upotoshaji.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,405
2,000
hahahahaha...ohooooooooooo....kumbe alikuja kuufuata uraisi, alafu mkawaweka pembeni waliokua wa maana...mkampa kupeperusha bendera kugombea nafasi ya juu kuliko zote.....sasa nani tumuogope hapa...yeye au chama kilicho ruhusu yote haya yatokee na kushindwa kufanya lolote mpaka alivyojitoa mwenyewe....? samahani lakini

Kweli kwa maneno haya nimemdharau sana Lema.
 
Lucas Sabuni

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
610
500
Naendelea kusisitiza kwamba Lowassa ni fisadi. Alipojiunga CHADEMA alipigwa sala ya toba, Mungu akamsamehe. Sasa ameamua kurudi kwa mafisadi wenzie aliowaacha, uvumilivu umemshinda. Sasa ajiandae gadhabu ya Mungu inaenda kumshukia. Mungu huwa hadhihakiwi.

Unafanya toba na kusema umebadilika hadi unazungusha mikono. Mungu nakuruhusu umshughurikie Lowasaa na kizazi chake. Kafanya ufisadi hadi nywele zimekuwa nyeupe.
Maneno ya mkosaji
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom