CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita amemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge.

Isaya Doita ametoa tuhuma hizi baada ya CHADEMA kupoteza Madiwani 3 pamoja na Katibu wa CHADEMA katika Jiji la Arusha. Mpaka sasa CHADEMA katika Jiji la Arusha imepoteza Madiwani 12 ambao wamejiunga CCM.

‘’Kuna tatizo nadhani viongozi wetu wa chama wilaya,mkoa, Kanda na hata taifa wanapaswa kukaa chini na kujiuliza ni nini kinaendelea Arusha’’, Isaya Doita alisema.

Ameendelea kusema, ‘’Badala ya viongozi kutoa matusi na kuwakashifu kwenye mitandao wanaohama, ni wakati sasa tujitathmini ili kujua tatizo liko wapi na njia gani zitumike ili kuzuia hali hii. Tatizo linalotusumbua CHADEMA ni kutoambiana ukweli na kama tutaendelea hivi na kutojitambua basi kuna uwezekano nafasi za madiwani na Mbunge tulizoshinda zikafutika katika Jiji la Arusha kwenye Uchaguzi ujao’’.

‘’Shida ninayoiona kwa sasa hapa Arusha tumekuwa kama familia ambayo imekosa mtu wa kutuunganisha pamoja. CHADEMA hatuna kiunganishi kizuri kati ya Mkoa na Kanda. Mwenyekiti wa Kanda, Godbless Lema lazima arudi hapa Arusha na akae na wanaCHADEMA na athamini uwepo wa wanaCHADEMA/viongozi wengine’’ Isaya Doita Alisema.

Alimalizia kwa kusema, ‘’Sitaki kuwa muongo na mnafiki, Wabunge wetu katika Jimbo la Arusha Mjini hawana impact, hawajawahi kugusa maisha ya Wananchi wa Arusha. Kuna tatizo katika ubunge wetu, hata wale wa Viti maalum. Mbunge Lema, Joyce Mukya na Catheline Magige siwaoni hapa Arusha.

Nadhani wanadhani Ubunge ni kwenda tu Bungeni na kusaini posho na kurudi. Leo ukiwauliza kuna shule ngapi na vituo vya afya vingapi na maendeleo yake hawajui. Tuna wabunge ambao hawajitambui na hawajui wajibu wao. Kwa mantiki hii ni bora kuchagua Mbunge yoyote anayejitambua na kujua majukumu yake bila kujali anatoka chama gani''.

Video ya alichokisema Diwani Isaya Doita.
 
Haya yote unayoyaona na hata mawazo yako mwenyewe ni wazi kuna kitu unahitaji huko unakotaka kutimkia. Kame ww ni Diwani ulishawahi kutimiza hayo kwenye kata yako? Je hao madiwani akiwemo meya huko walikotimkia wameondoka hata na mwanachama wa kawaida?? Chadema maslahi wote watakimbia na kutuacha Chadema ASILI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya yote unayoyaona na hata mawazo yako mwenyewe ni wazi kuna kitu unahitaji huko unakotaka kutimkia. Kame ww ni Diwani ulishawahi kutimiza hayo kwenye kata yako? Je hao madiwani akiwemo meya huko walikotimkia wameondoka hata na mwanachama wa kawaida?? Chadema maslahi wote watakimbia na kutuacha Chadema ASILI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini msiwatimue hao CHADEMA maslahi ili ibakie CHADEMA asili?
 
Mkuu nadhani ni bora kusikiliza hoja ya huyu Diwani na kuifanyia kazi. Watu wanaona ingawa viongozi wanaweka earphone zenye Muziki mnene wakati Miwani yao ni ya Mbao
Ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa wakati uongo hutumia lift!

Zile hoja za kusema ''WANANUNULIWA" zimeanza kujifuta zenyewe baada ya ukweli kuanza kuonekana!

Kuendelea kusema waache waende na wananunuliwa ni sawa na kuficha kichwa chini ya mchanga kama Mbuni na pia haina tofauti na kondoo wanaopelekwa kwenye machinjio kuchinjwa!
 
Back
Top Bottom