Arusha ina hadhi zote kuitwa Kitongoji

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
Ukisikia jinsi Arusha inatangazwa na kusifiwa utasema yes.. ni sehemu baabu kubwa sana... kila atakayesimama atasema lake..wapo waliothubutu kuiita Geneva of Africa... ni waongo..

1. Arusha ni chafu kupita maelezo
2. hakuna barabara
3. Ni sehemu pekee umeme unakatika masaa 21 (like yesterday)

Najiuliza hawa wanaosimama na kuisifia Arusha..haya hawayajui... au..
 
La uchafu -mbona dar nayo chafu,...pengine kuliko hata arusha,..barabara its natio agenda.....na hata huo umeme pia ni sehemu zote,....hapa labda tuseme hatuna jiji hata moja tz kwa vigezo hivyo labda moshi kidogo
 
Arusha ilikuwa mji mzuri sana hadi mwaka 1998. Tangia mwaka 1999 mji ulivamiwa na watu kutoka kila pande ya dunia ndio maana unaona power supply imelemewa na hata bara bara hazitoshi achilia mbali jinsi watu wanavyojenga slums kwa kasi.

Nikiwa kama mkazi mkongwe wa Arusha, nalisikitikia sana jiji letu, tuelekeako hali itakuwa mbaya zaidi pindi mipaka ya East African countries itakapofunfuliwa rasmi.
All in all I love Arusha.
 
Kiukweli mtoa maada nakuunga mkono asilimia 91. Maana ukicheki mapato ya nayo patikana na manispaa ya Arusha ni kubwa na wanashindwa hata kuendeleza zile barabara ndogo ndogo acha hizi za tanroad. Na vile vile ukiangalia arusha unakuta ATM ziko down muda mwingi foleni kubwa kwa mabenk hasa CRDB na NBC inatisha hawataki kuanzisha ma branch mengi arusha. Arusha imekua kitongoji cha Engarenarok.
 
Kiukweli mtoa maada nakuunga mkono asilimia 91. Maana ukicheki mapato ya nayo patikana na manispaa ya Arusha ni kubwa na wanashindwa hata kuendeleza zile barabara ndogo ndogo acha hizi za tanroad. Na vile vile ukiangalia arusha unakuta ATM ziko down muda mwingi foleni kubwa kwa mabenk hasa CRDB na NBC inatisha hawataki kuanzisha ma branch mengi arusha. Arusha imekua kitongoji cha Engarenarok.

hapo kwenye red nimepapenda..... kuna mchangiaji amesema mpk ya E.A itakapofunguliwa sijui patakuwaje.....
 
Tatizo ni uongozi wa Manispaa hapa wala tusilaumu wageni. Nasema hivi kwa sababu wageni wamesababisha vipii barabara za Mianzini kuelekea Kz, Kijenge, Sanawari ya juu, UngaLTD ,Matejoo, Sombetini , mitaa ya nyuma ya Golden rose mpaka stadium zisitengenezwe?.

Meya aliyepita Mr. Hedi amekwiba hela nyingi na akshindwa kusimamia haya tuyasemayo na alichofanya ni kubomoa paa la nyumba yake ya awali na kujenga ghorofa. Huyu Meya ameuza mlima Kimandolu na eneo la Tindigani ameliweka rehani kwa kisingizio cha uwekezaji .

Viongozi wabinafsi ndio wanaochangia mji wetu kuharibika
 
Tatizo madiwani wengi waliopita especially sisimu wa manispaa ya AR wanakula sana KiMo-Rally ndio maana issue kama hizi wanashinda kuzifanyia uamuzi.
 
Tatizo kubwa la Arusha ni hao madiwani, Meya na manaibu Meya waliokuwa huko nyuma. Hata huyo Meya wa sasa alishawahi kuwa naibu meya hapo nyuma. Ni nini wamefanya kuwasimamia hao watumishi wa halmashauri, they did f*** all. Kingine watumishi wengi wa Halmashauri ya Arusha wamefanya kazi hapo muda mrefu mno, wengi wao wana magari, majumba, guest houses n.k. Wamezitafuna kweli kweli! Siku hizi ukiendapale Manispaa, hakuna parking jinsi magari ya watumishi wa halmashauri hiyo yalivyojaa. Madiwani wapya waliochaguliwa safari hii wanaweza kuleta mabadiliko ijapokuwa ni wachache kulinganisha na idadi ya madiwani walioko. Arusha itabadilika pale tu watakapohamishwa watumishi waliofanya kazi kwa zaidi ya miaka kumi na kuwahamishia Arusha fresh staff ambao watashirikiana na hawa madiwani wapya wa CDM na wachache wa CCM.
 
Hata mi nilishangaa sana siku yangu ya kwanza kufika Arusha.. sifa zinazosifia Arusha ukiwa nje ya mkoa huo ni kubwa mno, tofauti kabisa na hali halisi ilivyo,,
 
Na hizi hela za parking wanazopokea kila cku zinaenda wapi.. Na jinsi wanavyo fatilia kwa makini kukusanya hizo hela wange tumia nguvu au mwendo kama huo kwenye kwendeleza mji, tungekua mbali.
jama ukikanyaga msitale wa parking 2...dakika mbili baada ya kushuka kwenye gari yako...hao hapo....unarudi unawakuta wanakusubiri na risiti ya 50,000 mkononi....m*therf**kers
 
Ukisikia jinsi Arusha inatangazwa na kusifiwa utasema yes.. ni sehemu baabu kubwa sana... kila atakayesimama atasema lake..wapo waliothubutu kuiita Geneva of Africa... ni waongo..1. Arusha ni chafu kupita maelezo2. hakuna barabara3. Ni sehemu pekee umeme unakatika masaa 21 (like yesterday)Najiuliza hawa wanaosimama na kuisifia Arusha..haya hawayajui... au..
You have serious problems upstairs... think with your head not your bottom... Is it true kwamba Arusha hakuna barabara?
 
Mji wa Moshi ulijiwekea utaratibu wa kujenga angalau km 1 ya barabara ya lami kila mwaka, tangu wameanza utaratibu huo wameweza kujenga barabara nyingi za mji wa Moshi kuliko miji mingi TanzaniaSwala la usafi ukweli ni kwamba wako mbali sana, ukiwa mjini jaribu kutupa karatasi au hata vocha iliyotumika ndio utajua wamejipanga vipi, ajabu ni kwamba miji mingine imeshindwa kuiga, huhitaji kuwa na kisomo cha hali ya juu kuweka mipango kama ilivyo Moshi mjini, mafanikio haya yana msukumo zaidi toka kwa wanamageuzi, hawa hawakubaliani na maswala ya rusha na uzembe katika utendaji.Jiji la Arusha limechangiwa pamoja na uzembe ni ufisadi ulio kithiri, mwaka jana au juzi kama sikosei mkurugenzi alileta mradi wa kupanda miti kando ya barabara ambazo ni finyu na hakuna maegesho ya magari ya kutosha, hili lilishangaza wakazi wengi wa 'jiji' hili lakini kwakuwa hapo ndipo palipokuwa na ulaji mzuri walishinikiza mpaka mradi huo ukafanyika. Baadhi ya watendaji ndani ya manispaa wanadokeza kwamba kiasi cha pesa kilichotumika kwa mradi kingetosha kujenga angalau km 1 ya barabara ya lami, lakini kwa upofu, ufisadi na kukosa uzalendo mradi uliofanyika ni huo wa vyungu vya miti mjini ambavyo leo vingi miti yake imekufa.Maeneo ya Clock Tower napo pana mambo yake, hapo ndio kitovu cha 'jiji' la Arusha lakini cha kushangaza hivi sasa pamekuwa mahali hatari na wala si salama tena kwani kuna kundi la vijana (chokoraa) kati ya 15 - 20 ambao wamepageuza ni mahali pao pa kutengenezea maisha, ukihitaji kupaki gari wao ndio watakuongoza kwa hiari au lazima na ukijifanya hutaki ujue kuna hasara zake (utaibiwa side mirror nk). Haya yote yanafanyika kama vile hakuna serikali japo vijana wa Mwema hawakosekani eneo hilo, hivi kweli tutafika?
 
Moja ya vielelezo vya watawala wetu kushindwa kuona mbali ni msongamano wa magari ktk jiji la Dsm na barabara ya dar - chalinze,na ujenzi holela na barabara finyu ktk manispaa ya Arusha. Ungetegemea mji huo wa kitalii na wenye mashirika na taasisi za Kimataifa kuwa mfano kwa usafi,ujenzi uliopangiliwa vizuri na miundombinu mizuri,lakini ni kinyume kabisa. Barabara ktkt ya mji ni chache na ni nyembamba. Soko la Kilombero sijui ni kwanini lilijengwa eneo lililobanana. Matokeo ni foleni na usumbufu mwingi kwa wakazi na watumiaji barabara ya Sokoine. Ukifika uwanja wa Sheikh Amri Abeid utashangaa kama huo uwanja ujenzi wake ulifuata mipango miji. Hauna parking na main stand iko ndani ya hifadhi ya barabara. Ukiingia ndani ni mchafu mpaka kutia kinyaa! Ukiona ujinga unaofanywa na madereva wa daladala ktk traffic lights za Sanawari unashindwa kuelewa kama kuna jeshi la polisi.
 
Ukisikia jinsi Arusha inatangazwa na kusifiwa utasema yes.. ni sehemu baabu kubwa sana... kila atakayesimama atasema lake..wapo waliothubutu kuiita Geneva of Africa... ni waongo..

1. Arusha ni chafu kupita maelezo
2. hakuna barabara
3. Ni sehemu pekee umeme unakatika masaa 21 (like yesterday)

Najiuliza hawa wanaosimama na kuisifia Arusha..haya hawayajui... au..
MIKAKATI NA vISASI VYA JK
 
Ukisikia jinsi Arusha inatangazwa na kusifiwa utasema yes.. ni sehemu baabu kubwa sana... kila atakayesimama atasema lake..wapo waliothubutu kuiita Geneva of Africa... ni waongo..1. Arusha ni chafu kupita maelezo2. hakuna barabara3. Ni sehemu pekee umeme unakatika masaa 21 (like yesterday)Najiuliza hawa wanaosimama na kuisifia Arusha..haya hawayajui... au..
Hawajui wanachoKINENA, Arusha makazi duni, hakuna nyumba za kutosha, hakuna hata maegesho ya magari, mji haupanuki etc, mji unakila aina ya kero.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom