Arusha halisi ilivyo na watu wake

Arusha halisi ilivyo na watu wake

Mleta mada kajichanganya ,hakupaswa kuhusisha vitu vilivyo karibu na Mkoa wa Arusha kwa msingi wa hoja yake anauzungumzia mkoa wa Arusha sasa kuzungumzia eti Mkoa waArusha upo karibu na mkoa mwingine hapo si sawa,angalia sifa nyingi alizoziorodhesha ni za mkoa wa Arusha tu sasa kama alikua anataka kuuzungumzia mkoa wa Arusha hakupaswa kukodi majeshi na kufanya kama ndio sifa ya mkoa wa Arusha
Rudia kusoma utamwelewa
 
Wewe umeona Serengeti pekee?? Kwani Kilimanjaro upo Arusha?? Alichosema ni zipo au zipo karibu.. Serengeti watalii wote wanaoenda huko wanapitia Arusha.. Kampuni zote za kitalii zinazopeleka watalii Serengeti ni za Arusha.. Ebu niambie wewe ni watalii wangapi wanapitia Mwanza?? Ni kampuni gani ya tours inapeleka watalii Serengeti ambayo HQ zake ni Mwanza au huko Mara?? Purposefully anayefaidika na Serengeti zaidi ni Arusha kuliko hata huyo Mara na Mwanza..
Unajua mimi nilichokua nataka aeleze sifa za Arusha tu kama mkoa ukisimama wenyewe kwa mambo yaliyo ndani ya mkoa kama alivyoainisha hapo mwanzo kwamba kuna makao makuu ya jumuia ya Afrika mashariki, Mahakam ya UN,Azimio la Arusha lilianzishwa hapo nk bila kuingiza au kuazima ujiko wa mkoa mwingine au sehemu nje ya Arusha.
 
Unajua mimi nilichokua nataka aeleze sifa za Arusha tu kama mkoa ukisimama wenyewe kwa mambo yaliyo ndani ya mkoa kama alivyoainisha hapo mwanzo kwamba kuna makao makuu ya jumuia ya Afrika mashariki, Mahakam ya UN,Azimio la Arusha lilianzishwa hapo nk bila kuingiza au kuazima ujiko wa mkoa mwingineau sehemu nje ya Arusha.

Na kwanini wewe concern yako ni Serengeti tu na Kilimanjaro hujaitaja?? Kuna ukanda katika hilo au??
 
Na kwanini wewe concern yako ni Serengeti tu na Kilimanjaro hujaitaja?? Kuna ukanda katika hilo au??
Kwa sababu wapo watu mpaka kesho wanadhani na wanafahamu katika uelewa wao kwamba Serengeti ipo Arusha na kwa kweli hiyo ndio ilikua concern yangu.
 
Salute KAKA mkubwa, Ar nimekaa Sana baadae nikahamia Dar, ni kweli, ni mji tofauti na miji mingi, Arusha maisha yako juu sana,pili wakazi wake wengi wanajituma sana, Moshi na Arusha watu wake ni wachapa KAZI tofauti na Dar kutwa umbea na story, tofauti nyigine ni kujitambua, wakisema no ni no, sweet home sweet.
 
Mimi naipendea hali ya hewa...hasa kipindi cha baridi....huwa najisikia raha sanna zaid ya nilipo dar.....lkn ntaendelea kuipenda zaid maana ninehamishiwa arusha kazin.....naamin ntaipenda zaidi.....naamini ntaoa pia Arusha..Mungu anisaidie.
 
jengo gani hili? inaonekana kama magari yanapandishwa juu kwa lift! FYI hii ni first automated and sophisticated car park
DSC02002.jpg
Lipo pembezoni mwa Natron hotel,ama nyuma ya Shekh amr abeid stadium.
 
Kwa sababu wapo watu mpaka kesho wanadhani na wanafahamu katika uelewa wao kwamba Serengeti ipo Arusha na kwa kweli hiyo ndio ilikua concern yangu.

Wengi wanajua hivyo kwakuwa hata mtalii wa ndani akitaka kwenda huko lazima facilities zote za kutalii kule azilipie na aanzie safari yake Arusha.. Ila Serengeti iko Mara lakini gateway ya kufika huko ni Arusha..
 
Habari zenu wadau.

Kwanza naomba niseme huu uzi hauna lengo la kuilinganisha Arusha na mkoa wowote Tanzania pia nataka huu uzi utumike kama reference kwa threads zote zitakazouongelea mji wa Arusha.

Dhumuni la kuuanzisha uzi huu ni kutokana na wimbi kubwa la members huku kuusema mji wa Arusha kwa namana tofauti ambazo pengine kutokana na kuwa sio wakazi wa Arusha wanaweza wasiwe sahihi sana.

MAMBO YA KIPEKEE KUHUSU MKOA WA ARUSHA.

1. Hati rasmi za uhuru wa Tanzania zilitiwa sahihi hapa na Uingereza mwaka 1961.

2. Azimio la Arusha la kujitegemea lilipitshwa mjini hapa karibu na maeneo ya mnara wa saa.

3. Makubaliano ya Arusha accords ya kusitisha vita nchini Rwanda yalipitishwa mjini Arusha mwaka 1993.

4. Una mbuga nyingi barani Africa, Hali ya hewa ni nzuri sana. Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Arusha National Park,Tarangire na mlima Kilimanjaro zipo ndani\karibu na mji huu.

5. Arusha imechezwa movie ya Hollywood maarufu kama HATARI mwaka 1962.....Hatari! (pronounced [hɑtɑri], Swahili for "Danger!") is a 1962 Americanaction/adventure romantic drama film directed by Howard Hawks and starringJohn Wayne. It portrays a group of professional wildlife catchers in Africa.[2]The film includes dramatic wildlife chases and the scenic backdrop of Mount Meru, Arusha a dormant volcano.

6. Wakati mikoa yote inahangaika na madawati likiwemo jiji kuu la Dar, Arusha haikuwahi kuwa na upungufu wa dawati hata moja na kila secondary school inayo maabara hata kabla ya agizo la Rais. (shule nyingi za serikali za Arusha zina computer labs)

7. Arusha ndio mkoa wenye matumizi makubwa ya Internet kuliko Mkoa wowote Tanzania and East Africa.

8. Arusha ni mkoa wa kwanza kwa Social Development Index (Huduma Bora za Kijamii kama maji, life expetancy, Health services, Education) By UNDP

9. Arusha ndio mkoa unaofatia ukitoka Dar kwa wingi wa viwanda na kuchangia katika pato la Taifa.

10. Arusha ndio mkoa wenye gharama za juu za maisha kuliko mkoa wowote Tanzania, kama unataka kuanzia maisha Arusha na una uhakika hauna kipato cha kujitosheleza nakushauri ujaribu Mwanza.

CHANGAMOTO ZA JIJI LA ARUSHA

1. Roads Roads Roads, Barabara Arusha zipo nyingi ila ni nyembamba kutokana na mji huu kuwa na masterplan ambayo ni ya muda mrefu, Maeneo ambayo yanatakiwa kuwekewa mkazo ni pamoja na Olasiti, Olasiver, Englesheraton, USARiver, Moshono, Kisongo, Ngaramtoni ambapo ndipo mji unaelekea.

Mimi kama kama mzaliwa Arusha na nimetembea mikoa yote sio kupita kwa bus wala kukaa siku 2 bali nimeishi mikoa mingi kwa kweli, nimekuja koconclude Arusha ni ya kipekee sana kuanzia tabia za watu wa Arusha ni tofauti 100% na watanzania wote, Maisha ya watu wa Arusha ni tofauti na mikoa mingine na hata wa mikoani wakija Arusha wanakiri maisha ya Arusha na watu wake ni wa tofauti.

#Arusha #GenevaOfAfrica #SafariCity #UN #A-Town #Machalii #Mamong'oo #Arachugga #Mabillionare #Meli #Mafogo #MjiWaMabilionea #HalfLondon #TheOnly #MjiWaWajanja #Tanzanite #HeadQuaters #EastAfricaCommunity #Zurich #TanzaniteInTheSky #Wakakamavu #ChaliAraa #Jombii #Ungalelo #Matejoo #Ungalimii #Arifu #Makamanda #USARiver #Watengwa #Weusi #Nako2Nako
We mwenye umeishaipambanua Arusha kwa kutofautisha na mikoa mingine #6, halafu bado hutaki anayechangia na yeye aipambamue tofauti na mikoa mingine, tukueleweje sasa?
 
kisu cha ngariba
Na wewe pia usome thread zote pia utaelewa msingi wa hoja yangu ni ipi,kwa kuwa hujasoma thread zote ni kwamba mimi nilikua nataka nadhani hata yeye ndivyo alivyokua anataka aorodheshe sifa za Arusha tu bila kutaja sifa za eneo lingine nje ya Arusha kwani hata ukisoma sifa alizozitaja kuanzia ya kwanza mpaka ya kumi ameorodhesha za Arusha tu,ukiondoa hiyokasoro ya kutaka kuazima sifa ya Serengeti,na hata ukiangalia hapo mwisho kwenye changamoto amejaribu kulinganisha mkoa wake na mwingine na picha alizo ambatanisha ameambatanisha picha za Arusha tu hajawekapicha za eneo lingine.
 
Inabidi nikupuuze tu.
 
We unayesifia Arusha yawezekana bado u mjinga hujatembea ukaona miji ya kusifia! Tembea kijana ukaone dunia ilivyo kisha uje na mapendekezo namna ya kuifanya miji yetu ipendeza.
Kama hujui, rankink ya miji mkuu hata Tanzania ni Dar es salaam, Mwanza Tanga, Mbeya ndio inafuata Arusha. Kama unakumbuka mji wa Arusha kipindi inapandisha kuwa jiji pamoja na Tanga na Mbeya, ilishushwa kuwa manispaa mpaka baada ya miaka kama mitatu hivi au minne kwa sababu haikuwa na kiwango.
Ukiichunguza Arusha utagundua kuwa tofauti yake na Moshi ni ndogo sana. Na unapokuta mji una maisha magumu basi hakuna income maana yake watu wengi hawazalishi. Acha kusifia kijinga. Tembea uone mengi ya dunia!
 
Umeumia sana.
 
Back
Top Bottom