Arusha city Geneva ya Afrika imegeuka Mogadishu ya Tanzania

Mambo yote ni Chato na kwa wasukuma

Sio majengo tu hata viongozi, Kaskazini hata kutoa Waziri kwa awamu hizi tangu 2015 ni kitendawili
 
Kwa uelewa wangu (I stand corrected of course), kujenga ukumbi wa kimataifa Dar es Salaam hakujaua ukumbi wa Arusha. Dar es Salaam inashughuli za kibiashara nyingi zaidi, hasa za kimataifa, kuliko mikoa mingine ya Tanzania. Arusha inashughuli zaidi za kiutalii na "kidiplomasia" kuliko mikoa mingi. Dodoma ni Mkoa Mkuu wa Kisiasa. Tungeweza kuendeleza hizi brands vizuri, hakuna shida ya kuwa na kumbi za kimataifa katika mikoa yote mitatu. Tukumbuke kabla ya JNICC kuna kumbi za watu binafsi ambazo zilikuwa zinatumika kwa shughuli za kitaifa. Ndio maana kuzihamishia kwenye ukumbi wa JNICC kumeathiri sana kumbi za watu binafsi.

Hata mikutano iliyokuwa ikifanyika Arusha ingepungua, iwe JNICC ilikuwepo au la. Washindani wa AICC walikuwepo tayari katika sekta binafsi. Ukitaka kuelewa kuwa hospitality industry imedorora Arusha, angalia sekta binafsi inavyopata tabu. AICC, haiko peke yake kwenye pigo hilo.

Halafu, nilikuwa Arusha 2018 kufanya mkutano AICC, na nilisikitika kuona maintance inayofanyika ni ndogo sana. Jengo linahitaji ukarabati na upgrade kama linataka kuvutia mikutano ya ngazi za juu tena. Halafu, matokeo ya COVID-19 yanamaanisha kuwa mikutano na mihadhara mingi ya kimataifa itahamia mitandaoni, sijui kama huu ukumbi umejiandaa kwa hili...
 

Mikutano mikubwa yote ya Kimataifa leo hii inafanyika Dar wakati zamani ilikuwa inakwenda AICC, hizo kumbi nyingine ndogondogo siyo ishu zinadili na Mikutano ya level yake hilo siyo ishu ila hapa naongelea Mikutano ya Kimataifa sasa hivi AICC haiwezi kushindana na ukumbi wa Nyerere Dar na sababu ni urahisi wa mipango kwa sababu Serikali yote iko Dar hivyo AICC haiwezi ku- compete hata siku moja, ile Mikutano ya zamani ya Umoja wa Mataifa yote haiwezi kufanyika AICC tena.

Sasa kwa ninini Serikali hiyo hiyo ifanye hivyo ? Dar tayari ina karibia kila kitu, hivyo hili la Mikutano ya Kimataifa wangeiachia angalau Arusha City, kwanza kuna Uwanja wa Kimataifa tayari KIA hivyo kama Mkutano mkubwa ukifanyikia Arusha City ungesadia sana kiuchumi sehemu nyingine za nchi, Dar ina Bandari ambapo miji ingne haina, ina kila kitu, by the way wakati wanaamua kujenga ukumbi wa AICC Dar ilikuwa ni Mji Mkuu wa nchi kwa nini waliamua kuujenga Arusha City kipindi hicho na siyo Dar ? Sasa iweje leo hii tuwaone walioamua hivyo walikuwa wajinga ?
 
Ni kweli Arusha mahotel kudorora lawama kwa serikali. Zamani tulikuwa na lobbying za kufa mtu mikutano ya kimataifa kufanyikia Arusha. Arusha hii si ile ya miaka yetu ....
 
Wabunge ndo wanaleta Mikutano? Hiyo Dar zaidi ya ule mkutano wa SADC kuna mkutano gani wa Kimataifa umefanyika huko?

Ni lini Upinzani ulipinga mkutano kufanyika Arusha?
 

Mambo machache nayoyajua nikufahamishe mkuu

JNICC imejengwa na serikali kwa kushirikiana na China, kama ushawahi kutembelea mule utaona kuna mahala mpk maneno ya kichina china yapo.

I think ulikuwa ni uamuzi wa kidiplomasia zaidi na sio wazo la kibiashara, lakini pia ili-make sense kujengwa hapo ulipo kwa sababu Dar licha ya kuwa mji mashuhuri kibiashara na balozi za nchi zote zipo hapo haikuwa na ukumbi 5 star wa mikutano.

AICC ndo wanao-manage na kurun JNICC. Kwa kifupi, AICC ni taasisi chini ya Wizaya ya Mambo ya Nje so hizi kumbi zote mbili Arusha na Dar ziko chini ya management moja.

Kudorora kwa AICC imechangiwa na issues kadhaa mtambuka ikiwemo, moja ni kuhafifia kwa nyota ya TZ kwenye diplomasia za kimataifa kumepunguza movements za diplomatic gatherings pande hiyo, pili wapangaji wakubwa wa AICC kwa miaka ya hivi karibuni shughuli zao ni kama zinafikia tamati ikiwemo zile mahakama za genocide etc, tatu covid-19 imezorotesha shughuli za kukutana kwenye conferences watu mambo wanafanyia online meetings.
 

Lkn bado sijaona logic ya kujenga JNICC kama AICC ipo kwa maana sasa hivi tuwe wakweli Mkutano wowote mkubwa wa Kimataifa ambao utafanyika Tanzania utakuwa Dar JNICC na siyo Arusha City, kabla ya ujenzi wa ukumbi wa Nyerere Mikutano yote ilikwenda Arusha city.

Labda nikuulize swali kwa nini unafikiri Serikali ya wakati huo iliamua kujenga AICC Arusha City na siyo Dar? Kwa maana AICC nafikiri (sina uhakika lkn na tarehe ) ilifunguliwa miaka ya 70 ' sasa kwa nini hawakuujenga Dar kwa maana Dar ilikuwa ni mji Mkuu wa nchi, kwa nini waliamua kwenda Arusha ?

Ukumbi wa AICC-Arusha City
 
Wabunge ndo wanaleta Mikutano? Hiyo Dar zaidi ya ule mkutano wa SADC kuna mkutano gani wa Kimataifa umefanyika huko?

Ni lini Upinzani ulipinga mkutano kufanyika Arusha?
Tangu vyama hivyo vimeanzishwa lini uliwaona wakifanya mkutano Arusha mahali ambapo ndipo palipo na ngome kubwa kabisa ya Upinzani hasa Chadema.

Kila Siku ni mlimani City kwenye ukumbi wa bei ghali.


Kila kitu kinaoaswa kifanyike kwa mifano yenye dhamira safi na sio kulalamika tu.
 
Acha ujinga, Huko ambako kuna CCM miaka yote wana nini cha maana? Unataka uniambie Dodoma au Dar wana moundo mbinu bora na First classs?
Huoni Dodoma sasa hivi inabustiwa kinguvu kujengwa maofisi ya wizara na kila kitu kufanyika huko.
 
Tulijua wapinzani mtaiua Kaskazini. Mnaona sasa mnakumbuka shuka kumekucha. Poleni sana.
 
Sijaelewa mantiki ya hoja yako kujikita kwenye ukumbi pekee, unamaanisha hatukupaswa kujenga ukumbi wowote Nchi nzima sababu upo wa AICC?
Hata kufikiria kuwa mikutano kutofanyika AICC sababu pekee ni kujengwa ukumbi wa JNICC hilo pia ni jambo la kushangaza..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…