tumeanza kazi iliyotuleta Arumeru na jana tuliweza kuhudhuria mkutano wa chadema pale The Ice Age Usa-River,kilichotuleta hapa ni kutoa elimu ya raia,kama mkikumbuka post yangu ya last week tulipata nafasi ya kutembelea jiji la moshi vile vile tuliweza kujionea nini kinaendelea pale,kila tunapopita tunaongea na wananchi ili kupima uelewa wao na mambo yote yanayohusu haki zao na uendeshaji mzima wa serikali yao,sisi kama watanzania tumeguswa na hali halisi inayoendelea hapa nchini,tumeona jinsi serikali inavyoendesha nchi yetu kiholela, kwa hiyo basi bila kujali itikadi zetu za kisiasa tumejiunga watu wa kabila tofauti na dini tofauti kuja Arumeru kwa gharama zetu wenyewe na kuanza rasmi elimu ya uraia ambayo inapigwa chenga na serikali ya ccm ili watanzania wasijue haki zao!huo ni mwanzo wa kazi yetu ya kujitolea,
tulipofika Arumeru jambo la kwanza kabisa tuliloshuhudia ni usalama,tumeamua kupanga vyumba vya kukaa sehemu mbalimbali tukisaidiana na wenyeji wenye nia kama yetu,kitendo cha sisi kuamua kutokaa hotelini ni usalama wetu,kwa jinsi upepo unavyokwenda hapa tunahitaji ulinzi na kwa kuwa hatuna uwezo wa kujiwekea ulinzi tumeamua kujiunga na wenyeji na kuishi nao,tumetangaza rasmi hatuungi mkono upande wowote ule chadema au ccm,sisi tupo hapa kwa elimu ya urai,thats all,
kazi kubwa tunayofanya ni kuelimisha wananchi juu ya haki zao (kumbuka igunga)tunawaeleza kuhusu wajibu wao wa kupiga kura,tunawaeleimisha kuhusu ubaya wa wao kuuza kadi za kupiga kura,tunawaeleza kuwa wao ndio wanaunda serikali na serikali ni mali yao na wao ndio serikali na wao wanaweza kumtoa kiongozi yeyote yule wa serikali madarakani kwa kuwa wao ndio waliowaweka pale,mambo ya kuwaelimisha ni mengi lakini kwa kifupi ndio hivyo,
tangu tumeingia arumeru mimi binafsi nimeongea na watu 234,kati ya hao 221 wamenieleza kuwa wanaunga mkono chadema na 13 wanaunga mkono ccm hiyo ni asilimia 85%
hiyo inaonyesha wazi kabisa chadema watashinda kwa kishindo,lakini je wataweza kulinda kura zao?
update inakuja soon!