Arumeru Mashariki, CHADEMA kunyakua jimbo?

Arumeru Mashariki, CHADEMA kunyakua jimbo?

Janvini humu kuna mambo ya kitoto sana, mna cheka cheka tu humu! Sitta mara Nassari mara Mwakyembe, Mnafahamu kiwanda cha Urafiki kimekufa? siasa zimewaharibu watanzania na hata magazeti yenu muda wote ni siasa tu mara utakuta Sitta amesema, mara Zitto kasema mara Pinda kasema, basi mmeishia hapo? Aaah Bye bye Tanzania ya Kikwete!
 
Acha kutunga maneno na kuyaleta home of great thinkers......huna source wala nn............unaleta unafki hapa sio lazima utume thread kama huna idea soma za wengine usiichafue jf!!!!

naona sasa humu panataka kufanana na vijiwe vya kahawa.. inaletwa topic katika format ya hearsay/gossip na wanajamii wanatokwa na mapovu kubishania..
 
na wakichakachua itakula kwao wamuulize mzee wa kiraracha pale jamaa wakimkosa mtu panga ni kukata migomba na miti kwa kwenda kia. Mi naona mchi hii bila kutokea machafuko hatuta heshimia. Maana ili ukombozi wa kweli upatikane ni lazima mmoja afe kwaajili ya wengine hii ni formula hata nchi zilizopata mapinduzi zimepitia huko hata kama nyie ni wasomi wazuri wa vitabu vitakatifu mtajua nazungumzia nini. Na hii ndio dawa pekee ya kuleta heshima katika taifa hili . Na kama hutaki we mwoga



Ingekuwa vema kama ungeanza kufa wewe kwa ajili ya Tanzania.
 
uo sio utabiri,mtu akisema kweli siyo utabiri........................

Democratic, kama unadhani huo ndio ukweli, umenoa!. Ila pia nimegundua ni wanabodi wachache sana huwa wanaukubali ukweli halisi!, wengi zaidi huogopa ukweli halisi na badala yake kung'ang'ania ukweli wa kujifariji nafsi zao kwa kujipa matumaini ya uwongo na mwisho wa siku huishia kulia lia tuu!.

Baada ya kupitishwa Sioi, uchaguzi Arumeru ndio umemalizika!. Kinachoendelea sasa ni kwa NEC kukamilisha tuu taratibu kukidhi matakwa ya kidemokrasia kusubiria kumtangaza rasmi!.

Wenye akili wataisoma hii post na kujinyamazia kusubiria April 2!. Ving'ang'anizi wa maubishi mtaanza kubisha na kuendelea kujifariji kuwa mtu yule yule toka chama kile kile aliyeshindwa na mahututi kitandani, sasa anaweza kushindana na mwana mfalme wa mtu yule yule aliyewashinda mwanzo na akashinda!.

Wengi wanategemea zaidi kura za chuki za wana CCM dhidi ya siasa za uchifu, usultani na ufalme za CCM kwa mtoto kumrithi baba yake bila kutambua asili ya Wameru ni ufalme wa koo fulani fulani!. Jerry alikuwa ni mfalme wao na Sioi ndiye mwana mfalume!.
Kwa wapenzi wa demokrasia ya kweli mtanisamehe sana kwa kuwadondolea ukweli mchungu!. Ili kuupata ukombozi wa kweli, lazima tukubali kukimeza "the bitter pill"- Sioi ndiye Mbunge Mteule wa Arumeru akisubiri kuapishwa!.

Pasco (wa jf).
 
[1] Ngongo atabiri ushindi wa CDM.

[2] Ngongo atabiri mvua za masika zitanyesha mwezi huu.

[3] Ngongo atabiri Kenya watajenga bandari kubwa Lamu.

[4] Ngongo atabiri Lowassa ataongoza kampeni za CCM Arumeru.
Mkuu Ngongo, utabiri wa kweli ni number tatu tuu, kungine kote umenoa!.
 
democratic, kama unadhani huo ndio ukweli, umenoa!. Ila pia nimegundua ni wanabodi wachache sana huwa wanaukubali ukweli halisi!, wengi zaidi huogopa ukweli halisi na badala yake kung'ang'ania ukweli wa kujifariji nafsi zao kwa kujipa matumaini ya uwongo na mwisho wa siku huishia kulia lia tuu!.

Baada ya kupitishwa sioi, uchaguzi arumeru ndio umemalizika!. Kinachoendelea sasa ni kwa nec kukamilisha tuu taratibu kukidhi matakwa ya kidemokrasia kusubiria kumtangaza rasmi!.

Wenye akili wataisoma hii post na kujinyamazia kusubiria april 2!. Ving'ang'anizi wa maubishi mtaanza kubisha na kuendelea kujifariji kuwa mtu yule yule toka chama kile kile aliyeshindwa na mahututi kitandani, sasa anaweza kushindana na mwana mfalme wa mtu yule yule aliyewashinda mwanzo na akashinda!.

Wengi wanategemea zaidi kura za chuki za wana ccm dhidi ya siasa za uchifu, usultani na ufalme za ccm kwa mtoto kumrithi baba yake bila kutambua asili ya wameru ni ufalme wa koo fulani fulani!. Jerry alikuwa ni mfalme wao na sioi ndiye mwana mfalume!.
Kwa wapenzi wa demokrasia ya kweli mtanisamehe sana kwa kuwadondolea ukweli mchungu!. Ili kuupata ukombozi wa kweli, lazima tukubali kukimeza "the bitter pill"- sioi ndiye mbunge mteule wa arumeru akisubiri kuapishwa!.

Pasco (wa jf).

ndoto nzuuuuuuri,lakini ya mchana
 
sidhani kama taarifa hizi ni za kweli na zinatoka kwa Sitta mwenyewe kwasababu ninachojua Mzee Sitta yupo Marekani siku ya nne sasa na taarifa hizo amezitoa kwa nani? kwa waandishi wa habari au kwa msemaji wake. otherwise this is misconception
We ndo kilaza namba moja so ukw marekani unakuwa bubu? Tumepata hd picha za baba mwanaasha na 50 cent ndo ijekw maneno?
 
Sasa naanza kuona mwanga hasa kwa Democrasia ndani ya CDM ..! hakika ni fahari yetu sote kama watanzania na itapendeza zaidi CDM WAKISHINDA. lakini nina wasiwasi na huyu mzee alichoongea ikiwa Source ni ya kweli mbona kama haeleweki vile !! si ni huyu mzee akiwa bungeni huongea utumbo kabisa akidai wapinzani wataendelea kuwa wapinzani siku zote , ? leo kabadili mawazo NY-tunamkaribisha rasmi.
 
tumeanza kazi iliyotuleta Arumeru na jana tuliweza kuhudhuria mkutano wa chadema pale The Ice Age Usa-River,kilichotuleta hapa ni kutoa elimu ya raia,kama mkikumbuka post yangu ya last week tulipata nafasi ya kutembelea jiji la moshi vile vile tuliweza kujionea nini kinaendelea pale,kila tunapopita tunaongea na wananchi ili kupima uelewa wao na mambo yote yanayohusu haki zao na uendeshaji mzima wa serikali yao,sisi kama watanzania tumeguswa na hali halisi inayoendelea hapa nchini,tumeona jinsi serikali inavyoendesha nchi yetu kiholela, kwa hiyo basi bila kujali itikadi zetu za kisiasa tumejiunga watu wa kabila tofauti na dini tofauti kuja Arumeru kwa gharama zetu wenyewe na kuanza rasmi elimu ya uraia ambayo inapigwa chenga na serikali ya ccm ili watanzania wasijue haki zao!huo ni mwanzo wa kazi yetu ya kujitolea,
tulipofika Arumeru jambo la kwanza kabisa tuliloshuhudia ni usalama,tumeamua kupanga vyumba vya kukaa sehemu mbalimbali tukisaidiana na wenyeji wenye nia kama yetu,kitendo cha sisi kuamua kutokaa hotelini ni usalama wetu,kwa jinsi upepo unavyokwenda hapa tunahitaji ulinzi na kwa kuwa hatuna uwezo wa kujiwekea ulinzi tumeamua kujiunga na wenyeji na kuishi nao,tumetangaza rasmi hatuungi mkono upande wowote ule chadema au ccm,sisi tupo hapa kwa elimu ya urai,thats all,
kazi kubwa tunayofanya ni kuelimisha wananchi juu ya haki zao (kumbuka igunga)tunawaeleza kuhusu wajibu wao wa kupiga kura,tunawaeleimisha kuhusu ubaya wa wao kuuza kadi za kupiga kura,tunawaeleza kuwa wao ndio wanaunda serikali na serikali ni mali yao na wao ndio serikali na wao wanaweza kumtoa kiongozi yeyote yule wa serikali madarakani kwa kuwa wao ndio waliowaweka pale,mambo ya kuwaelimisha ni mengi lakini kwa kifupi ndio hivyo,
tangu tumeingia arumeru mimi binafsi nimeongea na watu 234,kati ya hao 221 wamenieleza kuwa wanaunga mkono chadema na 13 wanaunga mkono ccm hiyo ni asilimia 85%
hiyo inaonyesha wazi kabisa chadema watashinda kwa kishindo,lakini je wataweza kulinda kura zao?
update inakuja soon!
 
Tupe updates mkuu..sasa nadhani tufanye kazi ya kulinda kura zetu,mimi sina shaka na wakazi wa Arumeru maana hawataweza kukubali kuuza utu wao kwa mafisadi wa hii nchi.
 
Mkuu upo maeneo gani uliyochukua sample yako? Nataka uende maeneo kama Momela, Ngarenayuki, n.k ili upate data za uhakika. Hapo mjini utakuta wote uliongea nao ni vijana ambao hawana hata shahada za kura.

Uchaguzi ujao natumaini CDM itatoa upinzani mkali kuliko huu tunaouana kwa maana wamefanya kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura.
 
wameru mimi nawakubali sana, hapa Tanzania hakuna kabila ambalo lina msimamo mkali sana kama wameru,

Wale watu hata kwenye taarifa za maendeleo za vijiji vyao wakigundua kuna sh 200 haionekani imefanya nini ni msala wa kufa mtu,na wanaongoza kwa kufanya mapinduzi ya viongozi wao ngazi ya vijiji, haipiti mwezi mwenyekit wa kijiji bila kupinduliwa,
 
Pelekeni elimu hadi kwa wale wazee wa Kishiri ambao ndio inaonekana ni mtaji wa CCM kwa sasa. Eti ukoo wa Sumari ndio wasemaji wa washiri wote!!! Kweli Mwl Nyerere aliona mbali sana alipopiga marufuku tawala za koo
 
Mungu akubariki sana.

Nadhani imefikia mahali Mr Clean achoke kutumiwa kama chambo.ANGEISHAURI CHICHI IMTUMIE EL.SASA KWA KUKUBALI KWENDA ARUMERU ATABATIZWA JINA LA TINGATINGA2 IKIWA NI NI SAFARI YA MWISHO KWAKE KTK SIASA ZA TZ NA AMEDHIHIRISHA USWAHIBA WAKE NA FISADI'S TEAM.SIJUI MAPOKEZI YAKE YATAKUWAJE USA RIVER! AU SAFARI HII ATATUMIA HELKOPTA? IFIKE MAHALI CHICHI IMTHAMINI PIA KADA MZEE RUKSA KULIKO KILA SIKU RWAZA.
 
Back
Top Bottom