Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tutakoma mwaka huu kwa mbwembwe zenu.
 
Hili kombe kawashindia Everton sio Arteta. Game yenu na city hamkuwa na maarifa yoyote ya kuifungua defence ya city ila mnavyomtukana Ndiaye utadhani ninyi mlifanya la maana dhidi yake.
Anyway, naishi Mwanza hivyo msinisahau kwenye sherehe za ubingwa.
Coyg
 
Kama nina nafasi kwa kawaida hua naangalia mechi yoyote. Mbona humu hua naongelea mechi za timu ambazo hata hatupo nazo kwenye kushindania ubingwa?

Ila wana wanahisi nimeandika kuhusu hii game kwakua City tupo nao kwenye kushindana. Labda mkiwa attention mtaona hua naandika hata mechi za washuka daraja.
 
Rice, Skelly na Eze kwenye midfield tena, kwa kifupi lineup ni ile ile ilocheza na fulham imeanza tena na leo.. LET'S GO ARSENAL, COYG ⚪️🔴
 
Wazee kazeni Leo muende final ......

Natamani sana mfike final, Ili mkashangazwe na kufundishwa mpira unavyochezwA....
Mtachagua wenyewe forward ya kina olise, kane ama ya kina kvara , dembele ?

Hawa wahuni Atlet wakienda final wanaenda kuaibishwa vibaya sana kulingana mpira wanaocheza.... the same applies to kwenu !!!!

Football entertainment..... baadae mapema sana kwenye kideo
 
Tuliwaambia Zubi bado sana, hana kiwango, pasi ovyo hazina macho.....

Juzi kalamba ubao, kuna watu wakaja kusema anapumzishwa kwa ajili ya mechi ya Leo... OK OK Leo tena kalamba ubao ...... coaching staff wameshaona mapungufu yake. !!!
 
Hao wanaocheza kama wamekatwa vichwa tunawahitaji sana fainali tuwafundishe namna ya kubalance kushambulia na kukaba.

Hii Arsenal hakuna kima anaweza akaifunga goli 3 mkuu hakuna...hao akina Olise Hizo spaces watazitafuta kwa tochi...

Tuangalia game.
 
Tuliwaambia Zubi bado sana, hana kiwango, pasi ovyo hazina macho.....

Juzi kalamba ubao, kuna watu wakaja kusema anapumzishwa kwa ajili ya mechi ya Leo... OK OK Leo tena kalamba ubao ...... coaching staff wameshaona mapungufu yake. !!!
Ingawa tunajua kiasili Skelly ni CM ila kwa mara ya kwanza tumemuona mechi dhidi ya Fulham, Zubimendi tunajua ni CM kuanzia yupo Spain.

Madrid, Barcelona, Liverpool zote zinaenda kumfuata kwakua zinajua ni CM. Profile yake ni ile aliyonayo Busquet na ndiyo ile aliyonayo Partey.

Huu ni msimu wake wa kwanza. Unachoandika leo wapo walioandika msimu wa kwanza wa Partey. Na Partey msimu wake wa kwanza ulikua mbovu kwake na kwa timu.

Tutatafuta statistics.
 
Kwamba arteta yupo jf au coincidence tu! Anyway hiki inabidi kiwe kikosi cha kumaliza nacho msimu huu
 
Friends of Madrid tupo hapa mapema sana, kuhakikisha marehemu anazikwa bila sanda
 
Kwenye hii mechi Atletico kama kawaida hua wana hii set up ya kujaza viungo na kuhakikisha kwamba wanakupiga mid block. At the same time wanakuachia Alvarez na Griezman kule juu, hapa unakumbana na pace, flairs na ball curving ability ya kutosha. So hapa balaa lipo kwenye break in play na counter.

Arteta kaja na hii set up ya kuweka viberenge kwenye wings, kamuweka Skelly akisubiri zile muscles zake na explosive dribbles za kwenda mbele. Eze ingawa ni mzuri kwenye vision ila ana tabia ya kuhisi yupo peke yake uwanjani. Kwa hawa leo akijisahau tunaweza karibisha presha.

Atletico ana hii rekodi ya kutowahi tolewa na timu ya kiingereza kwenye nusu ya CL. Leo Arsenal tuna kazi ya kuiupset hii rekodi. Arsenal tutakua tunaingia fainali mara ya pili baada ya ile Messi aliyotunyoosha.

Yeyote atakayekua anataka zaidi ya mwenzake ndiye atakayetoboa hapa.

Anyways, Arsenal to death.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…