JE WAJUA??: Mikel Arteta na Arsenal yake pamoja na Kuongoza Ligi Epl Msimu huu 2025/26 Kwa Kukaa kileleni muda mrefu, yeye kama kocha au mchezaji wake wowote hawajachukua tunzo za Monthly Awards ya Kocha Bora Mwezi au Mchezaji Bora wa mwezi, zaidi zaidi tu, Zubimendi alichukua tunzo ya goli Bora la mwezi na Raya-save Bora ya mwezi baas..
Hii pia haitofautiani sana Kwa wapinzani wao wa karibu Mancity, Guadiola nae kama kocha hajachukua tuzo kocha Bora Mwezi mpaka sasa lbd tu Haaland alishinda mara1 tuzo mchezaji Bora wa mwezi, ila yeye pep na Mancity yake, Kuna matumaini anaweza kuchukua tuzo ya Kocha Bora mwezi February hii iliyoishia sababu alishinda karibia mechi4 hadi5 mfululizo ikiwemo jana ya Leeds, tofauti na arsenal,Chelsea,man Utd, Aston villa, Bournemouth,wolves, Sunderland nk wengine hapo walipoteza mechi wengine wdlidroo mfululizo mwezi feb. Km Arsenal...
Yan Arteta na guadiola tuzo za kocha Bora msimu huu wamezidiwa ht na makocha wapya na waliofukuzwa km Carrick, Maresca nk, sasa sijui hii inatoa ishara Gani au italeta mapinduzi na rekodi mpya kwamba bingwa Epl bila kocha wao au mchezaji kutwaa tunzo yoyote ya mwezi sio kawaida karibu misimu6 sasa ya Ligi Uingereza.