Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kama unashangaa kwanini Eze hajaanza game ya 3 mfululizo kumbuka goli la Cash wiki kadhaa nyuma walivyotufunga 2 - 1.

Angalia Cash alikua wapi, Eze alikua wapi na mpira ulikua wapi. Hapa ndiyo unakumbuka Martinelli hua anacheza 90 minutes ingawa hascore na hatoi assists mpaka fanbase inalaumu.

Ndiyo mambo kama hayo.
 
Hata mechi ya Chelsea jamaa alikuwa hovyo sana
 
Ana vision ya merino, ni press resistant mzuri zaidi ya merino.. kwenye kushambulia anakupa anachokuofa merino?
Simkatai Norgaard ila wachezaji huzidiana kwa sifa tofauti tofauti, na unaweza kuta mwalimu anamchagua mchezaji kwa sifa fulani tu
Merino angekuwa kachangamka kidogo tu basi angekuwa mzuri zaidi....shida yangu mm na yy Kuna mechi nyingi akicheza kiungo timu unakuta IPO kwny transition ila yy anapooza shambulizi kilofa tu....yule mm kumkubali itachukua karne aisee
 
Kenge wamemtimua kenge mkuu.

Baada ya kumpa sifa na kumfananisha na Arteta wamegundua jamaa ni tapeli.

Ikatokea anaenda City, halafu Arsenal ikachukua kombe la ligi msimu huu basi na msimu ujao tunachukua tena.
 
Hana pace na physically siyo strong sana, anategemea technic zaidi.

Kuna pasi fulani unagundua anazicheza yeye tu. Na sometimes unaona anataka kucheza one two ila wenzake hawaelewi.
 
Kenge wamemtimua kenge mkuu.

Baada ya kumpa sifa na kumfananisha na Arteta wamegundua jamaa ni tapeli.

Ikatokea anaenda City, halafu Arsenal ikachukua kombe la ligi msimu huu basi na msimu ujao tunachukua tena.
Kwenda city inaweza ikatokea kweli ila Arsenal kuchukua ligi hilo haliwezi kutokea mkuu.
Hapo mwisho umemaliziaje vile? Kwamba na msimu ujao mnachukua tena😂😂😂 ndo yale yale ya kushinda match na real madrid robo fainali mnaanza kutafuta wakucheza nae final
 
Merino angekuwa kachangamka kidogo tu basi angekuwa mzuri zaidi....shida yangu mm na yy Kuna mechi nyingi akicheza kiungo timu unakuta IPO kwny transition ila yy anapooza shambulizi kilofa tu....yule mm kumkubali itachukua karne aisee

😂🤣Yupo slow, lakini ubongo wake upo fast
Mie namkubali kwa 75%
 
Game dhidi ya Aston Villa.

Same plan wamezunguka nayo kwetu mara ya kwanza, wakaitumia pia kwa Chelsea.

Wanakuacha na mpira, wanaabsorb pressure wanakukamata ukiwa upande wao kisha wanascore. Kipindi cha kwanza iliwaleta kwenye hatihati ya kuscore zaidi ya mara tatu.

Maajabu yake hawakuweza hata kupata shot on target.

Arteta knew this, akamuacha Merino awe winner wa second balls. Odegaard anakukaba kulia Merino anakuja kuchukua mpira kushoto. Na Merino hakai sana na mpira akiupata anautoa.

Rice hua anajaribu take ons na dribble mara kwa mara kwa Merino haiko hivi. Na kipindi cha pili Villa akaachiwa yeye mpira Odegaard akawa anaforce winning mipira ikaleta magoli yote kasoro la Magalhaes.

Villa walikua victims wa mchezo wao wenyewe, hii tulishaifanya kwa Brighton na City aliwahi kutufanyia hii.

Anayefuata ni Bournemouth, alitunyoosha nje ndani last time.
 
Hivi huwa ni nani anafananisha? Kana kwamba Arteta ni bonge la kocha au ukilaza wake?

Enzo tu kimafanikio amemuacha mbali sana Arteta, hata tusimguse Slot, Conte au Tuchel next level, huyo Arteta wenu mfananisheni na hao makocha wenzie akina De Zebri na hata huyo De Zebri akipewa timu nzuri tu atamuacha mbali sana.
 
Hawa jamaa wako brain washed, ukiwasikiliza unaweza ukastaajabu. Kwa mujibu wao Arteta ni bonge la kocha wakat angekua timu nyingine alitakiwa awe ameshafukuzwa siku nyingi.
 
Mgeeni timu yenu sasa.
 
Na tukawaambia huyu tunampa kura anakua kocha wa mwezi halafu sikilizieni balaa.

Wakajidai hamna kitu kama hicho. Tukampa ukocha wa mwezi.

Leo kapigwa chini
 
Namna jinsi Sunderland anavyoenda sahani moja na city, hauwezi kujiliuza kwanini tuliangusha points 2 kwa hawa wajuba

So far Sunderland hajapoteza mchezo akiwa nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…