Wells
Senior Member
- Apr 21, 2017
- 171
- 415
Kuna mtu humu alileta logic kwamba Arteta hawezi kuondoka kwasababu ameingiza pesa nyingi msimu uliopita kuliko club zote ligi ya Uingereza. Ni kweli au sio kweli, mimi sifahamu hilo lakini hii haitoshi kumfanya awe na uhakika wa kuhakikisha kibarua chake pale Emirates. Arsene Wenger alikua professor kwenye upande huo aliifanya Arsenal the best pia financially lakini ilifika wakati mashabiki hawakumuelewa uwanjani. Nguvu ya mashabiki ikaamua mustakabali wake pale Emirates. Kocha unapofikia wakati unapoteza connection na Fanbase huwa na hatari zaidi na inahatarisha zaidi nafasi yako. Arteta msimu huu asipochukua kikombe na hizi sajili zake ambazo mashabiki wengi hawazielewi, naimani utakuwa wakati mgumu sana kwake.