Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Salah, chelsea alifeli,
Swali dogo tu angekuwa na moto ule wa Roma tu ama huu wa liverpool, nani angemuweka benchi!?
Hakuwa na kiwango bora hichi ..
KDB nae si katokea Chelsea kwani alikuwa mmbaya ni vile tu hakuaminiwa but alikuwa mchezaji mzuri huyo dogo wenu mnaoangaika nae kumuongezea mkataba kwani ni mmbaya? au haaminiwi? Ngoja nikupe pia mfano mwingine ni Cole Palmer kwani alikuwa mmbaya man city? Ni vile Kama Chelsea wamemuamini na kumpa muda ndio maana umeona moto wake
 
Cole Palmer? Moto? Labda moto wa penalty
 
Unajua kama anawekwa bench na Saka? Halafu maajabu yake timu ya taifa Noni anamuweka benchi Cole Palmer
msimu uliopita Palmer kafunga magoal 15 na ukaweka assist 8 nitajie kiungo wako yoyote wa EPL kamzidi kwa takwimu na hapo striker ni Jackson tungekuwa na strikers wa maana Kama tulivyopata msimu angekuwa na assist nyingi sana maana anatengeneza nafasi nyingi
 
Unajua kama anawekwa bench na Saka? Halafu maajabu yake timu ya taifa Noni anamuweka benchi Cole Palmer
Nadhani kuwekwa benchi na Saka sio kipimo sahihi cha ubovu au ubora wa Palmer.
Timu ya taifa ya uingereza inacheza kwa kuvizia zaidi kaunta na wachezaji wake wanahitajika sana kukaba muda mwingi.
Palmer sio mkabaji mzuri sana kama Saka, Plamer hana ukomavu wa michuano mikubwa ya kimataifa kama Saka na vile vile Plamer kucheza pembeni kabisa kama Saka sio sehenu sahihi sana kwake.

Nami nawaunga mkono jamaa wanaotetea Palmer kuwa ni bora na sio mchezaji wa msimu mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…