makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 37,428
- 108,438
Katika kucheza kwangu mpira, nimeitwa majina ya mafundi wengi, ila kuna jamaa yangu aliniita MTAKATIFU CAZORLA, mbele ya watu nikakataa lile jina.View attachment 3378696
OOOOO SANTI CAZOOOORLAAAAA
Jamaa ana miaka 40.
Kila mtu anaijua historia yake na sisi, ila tuangalie jamaa anavyomalizia historia yake kwenye boli la kulipwa.
Aliamua kurudi kwenye timu yake ya utotoni, Oviedo ambayo ina zaidi ya miaka 20 haijakuwepo La Liga na ilinusurika kufilisika kabisa ila kwa miujiza flani.
Jamaa alitaka kucheza bure kabisa na anatoa misaada na pesa zake kuliko anazopokea (kisheria, ilibidi apokee kile kiwango cha chini kabisa kinachoruhusiwa kisheria maana kisheria ni lazima alipwe) na kweli ameipambania sana timu.
Kifupi, jamaa alianzisha bonge la comeback kwenye play-off ya kuingia La Liga na Oviedo wameingia La Liga kwa msimu ujao. Bonge moja la stori kutoka kwa mchezaji niliyemkubali kuliko wote na mpaka sasa hakuna mchezaji ninayeweza kusema nampenda zaidi ya Santi.
Nikamwambia anachokifanya CAZORLA kwa mguu wake mmoja tu wa kulia mie nafanya kwa miguu yote, hapo hatujaongelea mguu wake wa kushoto.
Fundi sana jamaa.