Arsenal (The Gunners) | Special Thread

so martinell, nico , rodrigo we unaanza na martinell?
 
so martinell, nico , rodrigo we unaanza na martinell?
Mimi kama mimi, nitasema yes. Nitamuanzisha Martinelli maana ni msumbufu, ana press na anarudi sana kusaidia kukaba bila kuchoka na pia akipata balls huwa anakimbiza sana tu ila anachamgamoto ya umaliziaji. Ataanza yeye, halafu dk ya 60 huko wakati mpinzani amechoka na usumbufu wa Martinelli kwenye ushambulizi na ulinzi, namuweka Rodrygo kuja kumaliza kazi.
 
Wakipaki basi/low block wanasema ni haram football na wanajisifia ila timu nyingine wanaita underdogs.
Hili jukwaa ni sehemu sahihi kabisa ya kupunguzia stress sioni haja ya kwenda baa.
Sisi hatupaki basi mzee. Tunatengeza overloads. Manyumbu hawawezi kuona tofauti.
 
Em nitajie timu ambayo kwenye mechi 38 haikuathilika na maamuzi mabovu

Zipo timu zingine ndiyo. Siyo kama Arsenal lakini. Naamini pia ubora wetu na bahati pia imekuwa ikitusaidia sana. Sisi tunaweza dhulumiwa mechi 6 mpaka 8 na tukapoteza points kwenye 3 au 4 ya hizo mechi na zingine tukashinda. Mfano beki wetu alipigwa kadi nyekundu kihuni tu na refa game ya Wolves, tulishinda ile mechi. Ile kushidha kwetu licha ya dhulma ndiyo inafanya watu wafikiri hatudhulumiwi.

Madhara yapo pia ligi nzima. Ni kwamba utakuta sisi tukidhulumiwa tunakosa ubingwa tunabaki na top 4,
Ubaya ni dhulma hizi mbili tatu zikizikuta timu za chini, zinaweza kushuka daraja.
 
"Sisi tunaweza dhulumiwa mechi 6 mpaka 8 na tukapoteza points kwenye 3 au 4 ya hizo mechi na zingine tukashinda."

Kwa hio hizo points 3 au 4 mnazo dhulumiwa ndio zimesababisha mkakosa ubingwa pia msimu huu?
Liverpool amemaliza ligi akiwa na points10 zaidi yenu, kwa hio hizo points 4 mlizodhulumiwa hata tukiwaongezea points 4 tena nyingine bado hamuwezi kuwa mabingwa.

Tunaposema kila siku kua Arsenyau kuanzia Management, kocha, wachezaji mpaka mashabiki wana mentality za mid table team sio kama tunawaonea.
Siku Arsenyau atakapoamua kuchange mentalities zao na kuact kama timu kubwa ndio msimu watakaoanza kubeba makombe, ila kwa hii inferiority waliyokua nayo kila msimu wataishia kua wasindikizaji tu.

Hii mentality waliyonayo Arsenyo ndio hii hii mentality inayotutafuna Waafrika tuliyopandikizwa na wakoloni.
Tunashindwa kua na maendeleo kwa excuse kua kutawaliwa na wazungu ndio kulikosababisha tuwe hivi, wakati wachina na mataifa mengine ya Asia tuliopata nao uhuru miaka sawa wenyewe wametuacha mbali kimaendeleo baada ya kujitambua na kuachana na hizi fikra mbovu.
 
Siyo points 3-4, mechi 3-4. Ni kusema yaani kufungwa mechi 4 kwa dhulma ni kupoteza points 12.
 
Loosers siku zote hata kwenye real life huwa wana mentality ya kulalamika na kuamini external forces ziko against nao.

Tukirudi kwenye mpira, timu zenye mentality ya kibingwa hazina muda wa kulalamika,
Anakupiga kwa open play, ukikataa goli anafunga penati.

Unamnyima penati anafunga kona.

Unamnyima kona anafunga freekick.

Unamnyima free kick anafunga kwa long shots.

Yote hayo yameshindikana anapoteza hiyo game moja anaenda kushinda 8 mfululizo.

Hii ndiyo mentality ya kibingwa.
 
Siyo points 3-4, mechi 3-4. Ni kusema yaani kufungwa mechi 4 kwa dhulma ni kupoteza points 12.
Hii hapa kauli yako mwenyewe, inaonyesha licha ya kudhulumiwa na marefa lakini bado mnashinda na kuondoka na points3, umetolea mfano kabisa kua kwenye mechi 6-8 mnazodhulumiwa na marefa hua mnapoteza tu points 3 au 4, hivyo hoja yangu mimi ni kua hizo lawama zenu za kudhulumia sio sababu ya nyinyi kukosa ubingwa bali ni kichaka mnachokitumia kufichia tu mapungufu yenu.

"Zipo timu zingine ndiyo. Siyo kama Arsenal lakini. Naamini pia ubora wetu na bahati pia imekuwa ikitusaidia sana. Sisi tunaweza dhulumiwa mechi 6 mpaka 8 na tukapoteza points kwenye 3 au 4 ya hizo mechi na zingine tukashinda. Mfano beki wetu alipigwa kadi nyekundu kihuni tu na refa game ya Wolves, tulishinda ile mechi. Ile kushidha kwetu licha ya dhulma ndiyo inafanya watu wafikiri hatudhulumiwi."
 
Its very fun to deal with fun cases.
Mimi nawaelewa sana mashabiki wa liver au city wakija kutuchangamsha humu na ni haki yao kabisa as they are highly decorated with success in recent years.

Ila hata man u,Chelsea au Newcastle?
Hahaaa hii inanikumbusha tabia za mwisho kwa mtu anayekaribia kuitwa marehemu
 
Yes. Kote huko nimesema mechi, siyo points...labda nijazie ili isomeke kama hivi: "kudhulumiwa kwenye mechi 8 na kupoteza points kwenye mechi 3 au 4..."
 
Hoja kali sana hii.
Nafikiri pia ndiyo maana Arsenal haina wafungaji wenye magoli zaidi ya 10 ila ni miongoni mwa timu 4 za juu zilizoongoza kwa kufunga magoli mengi huku pia ikiwa katika timu zilizofungwa magoli machache. Kama ni kufosi, tunafosi, ingawa uzembe pia tunafanya.

Nikupe mfano. Je inakuwaje Arsenal iliongoza kwa kufunga magoli ya set pieces, licha ya kutofunga goli hata moja kwa direct free kick? Corner kicks na indirect free kicks. Jibu ni kwamba ulifika wakati Arsenal ilibidi ikazane na kutumia set pieces na ikafanyia kazi suala hilo.

Amorim akiwa Man United alisema hiki juu ya Saka na Martinelli- alisema hawa jamaa wakiingia kwenye box na kuruhusiwa ku cut in na kushoot, wanakuadhibu hivyo mabeki wanahakisha hawawaruhusu kucut in na kufunga.

Njia mbadala ya mabeki ikawa ni kuwaweka kwenye weak foot zao ili wakishindwa kushoot basi wapige cross. Cross inaweza ikazaa goli au mmaliziaji akakosa lakini pia mara nyingi cross hizo zilizaa kona. Arsenal ikajua hilo na ikajitahidi kuhakikisha inapata magoli kwenye hizo kona.

Hiyo ndiyo mentality ya kibingwa unayoiongelea.
 
ila rodrigo anakupa vyte kasoro ukabaji tu
 
ila rodrigo anakupa vyte kasoro ukabaji tu
Yes.

Ila ukabaji ni muhimu sana kwenye top levels za EPL na timu haziwezi kukubali kuwa na wachezaji wasiowajibika kisawasawa uwanjani. Kule mabeki wanakaba kibabe haswa na bado wanashambulia kama mawinga na mastriker hivyo unahitaji wachezaji wako wote wawe tayari kushiriki katika ulinzi ili kusaidia mabeki wako. Arsenal iankuwaga na defense bora si kwa sababu ya mabeki tu bali kwa sababu kina Kai na Odegaard na wengine kule mbele wanawajibika haswa, kama siyo kwenye 1v1 marking basi pia kwenye kujipanda kuziba mianya na kutengeneza overloads ( πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ mambo ya dark arts) bila kuchoka.

Rodrygo, Vini na Mpappe walichangia kiasi kikubwa sisi kuwachapa kwa sababu ya ukabaji hafifu wao. Na ndiyo sababu mimi binafsi nitaanza na Martinelli ili kuhakikisha tunamtawala adui katika kila idara halafu Rodrygo aingie baadae wakati mpinzani yuko hoi. Nafikiri pia zile enzi za subs 3 tu hii mbinu ingefaa zaidi kuliko enzi hizi za subs 5 ila bado inasaidia.
 
Kona zilipofeli what happened?

Timu ika seize.

Hakuna bingwa wa namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…