Arsenal (The Gunners) | Special Thread

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nilisharidhika na kufika nusu fainali tu yaani. Ikitokea tumetolewa sitalaumu na ikitokea tumevuka nitafurahi tu.
Kwakweli kwa kufika hatua hii ni jambo la kujivunia sana na hasa ukizingatia ni muda mrefu sana umepita hatujafika kwenye hizi late stages za UCL..!! Lakin hatupaswi kuridhika kwa kufika nusu fainali tu hasa ukiangalia hili ndio kombe peked lililoko mbele yetu, aisee bado mechi tatu tu za hii michuano, yatupasa tucheze kufa kupona tusipoteza hata mechi moja na sisi tuweke heshima ulaya
 
Madrid akawaonee wajinga wenzake. Standard ipo na inazidi kuwepo ata msimu ujao madrid hatatamani kwenye mtoano akutane na arsenal

Kufunga paa ndio kuliko waponza, wangeliacha wazi tu
Saliba aliniudhi baada ya kuwapa lile bao, lakin baada ya kukumbuka kazi anayoifanya ikabidi niwe mpole tu.

Wapumbavu mikwala miingi sijui remontanda kila mtu aligeuka motivation speaker mpaka akina Ramos, na uwanja wao utafikiri hotpot ya kutunzia ugali wa mtama...!! Halafu mwisho wa siku wamechezea tena kichapo, nafikiri huu msimu hawatakuja kuusahau sikumbuki ni lini real madrid walitolewa kwa fedheha hivi.
 
Tunaanza circle tena.

Mwanzo ilikua Madrid atawatoa. Akafa 3.

Ikaahidiwa comeback for a week.

Madrid kafa tena.

Wameanza ujinga wa kusema PSG atatukomesha.

These fools never learn
Acha waendelee kupiga ramli mpaka mwisho wa msimu, mwisho wa siku wataanza kusema "mna bahati tu timu zote shiriki zilikuwa mbovu" hapo ni baada kazi kuwa imekamilika...!!
 
Hata kama tumeshinda kuna haja ya kuandika juu ya matukio kadhaa ya uwanjani na nje ya uwanja na kukabidhi FIFA.

Dani hakua na haja ya kuanzisha ugomvi na Saka kwa kumfuata kwenye tunnel.

Asencio na Rudiger walikua wanacheza kihuni unnecessarily.
 
Loserfools ilikua kila wakikutana na Vardrid Mudi ataanza kupost online 'Revenge' halafu wanabondwa.

Ilifikia hatua ikabidi aache kuandika revenge. Na bado wakabondwa.

Kwa Arsenal mambo yamekua tofauti
 
Mimi naiona Arsenal na Barcelona fainali, je tutalipa kisasi cha 2006?

Katika maisha yangu ya soka mechi zilizowahi kuniuma, sikulala kabisa ni,
1. Arsenal Vs Barcelona UEFA Final 2006
2. France Vs Italy WC Final 2006
3. Yanga Vs USM Alger Caf CC Final 2023

Tumeshatafuna kubwa la maadui Madrid nothing can stop us.
 
Na msimu huu tunabeba kombe la championship
 
Loserfools ilikua kila wakikutana na Vardrid Mudi ataanza kupost online 'Revenge' halafu wanabondwa.

Ilifikia hatua ikabidi aache kuandika revenge. Na bado wakabondwa.

Kwa Arsenal mambo yamekua tofauti
Acha utani dogo huyo Madrid hajabondwa na liver?
 
Mbape anajiona ana gundu sana, ameenda timu kubwa yenye mastaa wengi Kwa mbwembwe nyingi na ameishia kutolewa kwenye mashindano ila timu yake aliyotoka imesonga mbele kwenye hatua ya Semi final.

Luis Enrique ni bonge la kocha jinsi alivyoifanyia mabadiliko PSG kutoka kuwa timu ya Galacticos kuwa timu ya vijana wadogo wenye vipaji inathibitisha ubora wake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…