Will Jr
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 5,125
- 7,521
Kwetu wabongo beki ni beki na striker ni striker, yaani beki azuie, striker afunge, mpira tunauona hivyo, lakini kumbe unaweza kusajili beki na akatatua matatizo ya attack, mfano, usajili wa calafiori lengo lilikuwa, ok, ku stabilize defense lkn kubwa zaidi ni kuaffect our attacking dynamics, ndiyo maana Mikel arteta anasema after Timber's ACL injury last season kulizuia plan yake ya kuifanya Arsenal kuwa unpredictable force, leo ukimtoa Skelly lewis na kumtumia Kieran Tierney usitegemee kuwa na similar dynamics, mfano mzuri ni namna tulivyokuwa wazuri na fluid going forward baada ya usajili wa zinchenko, leo tupo sawasawa kwenye kutengeneza nafasi lkn tupo hovyo kwenye finishing, naamini tunahitaji usajili wa striker sababu ya finishing, na ieleweke kwamba finishing ni suala la mtu binafsi sio jambo la system