makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 37,428
- 108,438
Utulivu wake, anavyo receive mali, anavyoachia.. Zile turn zake akipokea mali toka kwa kipa, wakati mwingine nachelewa kujibu msg za mama watoto. 😂Kilichonifanya nimkubali zaidi ni alipoondoka ATM ambayo wakati huo ilikuwa bora kuliko sisi, na akasema siku zote alikuwa na ndoto ya kuchezea Arsenal. Alinipata pale hadi leo, namkubali kabla hajaanza kuichezea klabu yetu.
Halafu alivyokuja tu, wenzie wakatwaa kombe! Nilijisikia vibaya sana.