| HATUTAKI MAZOEA NA WATOTO. TUNALIPA ZILE MBILI KWANZA.
Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Aston Villa wakiwa ugenini dimba la Villa park. Trosaard na Thomas Partey wakipeleka ushindi Gunners huku Raya akiendeleza uhodari wake eneo la goal keeping.
FT | Aston Villa 0-2 Arsenal ( Trossard x Partey ).
Katika mechi ambayo Arteta ametumia hesabu kali sana kimbinu ni hii huku Unai Emery timu yake ikionekana kukosa baadhi ya vitu viwili ( Utimamu baadhi ya wachezaji na Subs za lazima).
1. Arteta anajua ubora wa Aston Villa bila mpira ni Kukabia eneo la katikati hadi chini sana wakiwa na uhodari mkubwa wa kufanya linkup bora sana wanapotapa mpira kwakuwa wana wachezaji wenye kasi.
2. LEON BAILEY, MORGAN ROGERS na WATKINS. Ili kuwatengenezea Big spaces kwenye flanks kuwapata Arsenal kwenye 1v1 baada ya kupata mpira unaadhibu ile rest defence ya Arsenal. Lakini leo Arteta alimgundua Unai how?
3. Usiwe na haraka ya kuwafanyia pressing wakati mashambulizi yanaanzia nyuma ( ili kusiwe na nafasi kubwa kati ya msitari wa ulinzi na ushambuliaji).
4. Thomas Partey kama atasogea. Rice atakuwa karibu na Saliba/Big Gabi. Ikitokea Turnsover tupo karibu na opponts kufanya Covering. Hapa walifanikiwa. Lakini how tunakuwa bora kwenye OFFENSIVE?
NOTE.
1. Nadhani Trossard amekuja kutoa somo la namna ya kufanya MAAMUZI SAHIHI UKIWA ENEO LA HATARI. Shida kubwa ya Arsenal ilikuwa kufanya decision wakifika final third.
2. Martin Odegaard, Kai Havertz na Martinelli walikuwa wanachelewa kufanya maamuzi pale opponents anapo-break defence.
3. Trossard mjanja mjanja sana akiwa eneo la hatari
4. DAVID RAYA ni really GOALKEEPING. Chagua wewe unapenda footworking yake au saves zake? Bila yeye mechi ingekua ngumu sana. Kashatoa SAVES YA MSIMU
5. Bukayo Saka anaibeba sana hii Gunners, Halafu mguu wa ZINCHENKO unahitajika sana kwenye Creativity in LCM? Kuna muda Martinelli anakosa chakufanya akikutana na msitu.
6. WATKINS kakosaje lile goli?
7. Mechi ya pili, Clean Sheet ya pili? Kuna kipa mwingine?
NB. Unai kapata dawa
Zingo