Dakika 90 zimekamilika Arsenal wakiwashughulikia waliowakosesha ubingwa 2023/24 kwa jumla ya magoli 2 kwa 0 yakifungwa na Leandro Trossard na Thomas Partey kipindi cha pili, Arsenal wakiwa ugenini Villa Park. Msimu uliopita Arsenal aligawa pointi zote 6 kwa Villa hivyo kumfanya ashindwe kupata alama za kutosha kutwaa ubingwa.
Baada ya mechi mbili kuchezwa leo Arsenal anasimama ktk nafasi ya 3 katika msimamo wa EPL akiwa na alama 6 na tofauti ya magoli 4 wakati vinara ni Man City wakiwa na alama 6 na tofauti ya magoli 5 huku Brighton akiwa na alama 6 na tofauti ya magoli 4 katika nafasi ya 2.
Ni hayo tu kutoka Villa Park