Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Why use such energy kubishana na hao Manufactured fan base.
Hakuna mpira hapo zaidi ya kufurahisha nafsi zao.
 
Ni sawa, Sijasema pesa haitumiki au haikutumika. Nimesema vilabu vilikuwa vinaitengeneza hiyo pesa vyenyewe, bila kupewa na mabilionea. FA walitaka na wanapenda sana vilabu vijiendeshe kwa pesa zake zenyewe tangu enzi hizo maana pia uchumi unaelewa umuhimu wa 'self-sustaining model', ili kudhibiti vilabu kujiendesha katika hali ya madeni na kuathiri uchumi wa nchi kwa ujumla. Huenda pia hujawahi kusikia sakata la Leeds uniited ilivyokuja kufilisika na kusota kutoka kushiriki champions league mpaka kuozea daraja la pili huko. Unaweza usijue kuwa Leeds ilishatamba Champions League. Matajiri wakaja kubadilidha game kwa kutumia pesa zao binafsi, na kwa kipindi kirefu, ukifanya tafiti, utakuta Arsenal lilikataa mfumo huu. Anyway, ndiyo pesa lazima itumike na hili si suala jipya. Iko hivyo tangu zamani. Ila pesa imepatikanaje?

Ukienda kwenye suala la mishahara, enzi hizo pia kuna wachezaji wakubwa walikuwa wanapata mishahara mikubwa sana tu. Mfano akina Sol Campell na Thierry Henry walikuwa wanakula mishahara ya 120,000 pounds per week, miaka 20 hiyo iliyopita. Unadhani ukiweka factor ya inflation, mishaharaa hiyo itakuwa ni kiasi gani kwa ligi ya sasa? Mpaka sasa kuna wachezaji wa timu kubwa tu wanalipwa 80000/week, yaani chini ya mishahara ya wachezaji fulani miaka 20 iliyopita. Ukiangalia suala la wachezaji kuwa masikini, badili na kusema wachezaji wa zamani wengi wamefilisika. Tambua pia hilo suala la kufilisika kwa wachezaji linatokea kwenye karibia kila mchezo wa kulipwa na sababu kuu ni ukosefu wa elimu ya matumizi ya pesa na uwekezaji ambayo inaathiri wachezaji wengi sana mpaka leo hii. Suala siyo hawalipwi vizuri. Ni wamefanya nini na pesa zao? Mtafute Mathieu Flamini. Amechezea Arsenal na kina Thierry Henry na kina Fabregas. Alikuwa mchezaji wa kawaida tu na hakuwahi kushika mishahara wala madili waliyopata kina Henry. Kina Henry wanafanya punditry saivi. Flamini ni bonge la bilionea. Je David Bekham unamfahamu?
 
Why use such energy kubishana na hao Manufactured fan base.
Hakuna mpira hapo zaidi ya kufurahisha nafsi zao.
Ni mdogo wetu huyu. Tunamuelewesha tu kuwa mambo yalivyokuwa na pia yalivyo sasa ni zaidi ya yeye anavyofikiria.
 
Sema unachekesha mkuu unataja super stars ambao walikuwa top ,MTU kama Beckham saizi ni billionear ndio lakin walikuwa wanalipwa pesa nyingi ,Hao kina Henry ndio tuseme kina kdb WA sasa lazima wapate pesa nyingi ...saizi wachezaji wanakula pesa nzuri tu hata wakiwa bench .......

Henry asingejiongeza kutoka hapo Arsenal na kusepa zake Barcelona saizi angekuwa masikin WA kutupwa ,ndio club imempa mafanikio ..

Mbona hujamtaja Emmanuel eboue mchezaji wenu Tena muivery cost aliyecheza Arsenal saizi kafilisika vibaya ...

Wes Brown huyu Ni legend kabisa WA man utd ,kaomba kukaa kwenye nyumba ya dogo rashford ...maisha yamemchapa hatari ....

Jermaine pennant huyu mwingereza nimeona juzi anasema kafirisika na kacheza Arsenal ....

Hao wote Ni baadhi ya wachezaji walicheza mpira Kwa kufuata ujinga WA mashabiki et kupigania timu Bila kujua mpira Ni just 32 yrs timu na mashabiki wanakutema .....and you fight fou your life

Timu kujiendesha yenyewe sikatai ,ila kukaa chini na kuona man city ndio anatumia pesa pekee yake ,Tena et zinatoka mfukoni MWA Mansour sio club Ni maajabu πŸ˜‚
 

Unakuwa mgumu sana kuelewa vitu virahisi sana.

Hakuna aliyesema Man City anatumia pesa pekee yake au wengine hatutumi pesa. Tunachosema ni mmefanya financial doping kupitia mfuko wa Mansour na mmechakachua vitabu. Unachotetea ndicho tunachokushtaki. Tunasema kwamba nyie mmetumia uhuni wakati wenzenu tumefanya vitu kihalali. Na wote tunaelewa hichi ndicho unachopinga. Nimeona tu nikupe ki elimu kidogo ili ujue mambo yako zaidi ya unavyofikiri.

Sijawataja akina Eboue kwa sababu nimekuambia kuwa wanamichezo wengi wanafilisika kwa kukosa maarifa, siyo kwa kukosa mishahara mizuri. Tena kina Eboue na Penant unakuta wamefilisika kwa sababu zao za kibinadamu zinazoeleweka kabisa. Wewe unaileta kama kucheza kwao Arsenal ni ishu hapa. Jiulize, je, Eboue na Flamini wameshawahi kucheza pamoja? Ukipata jibu, jiulize mbona mmoja ni tajiri sasa na mwingine siyo? Ndiyo maana nikakupa mfano wa mchezaji aliyekuwa anapokea kidogo kuliko kina Henry ila angalia yeye amefanya nini na chake na angalia wenzake wamefanya nini na vyao. Mbona ni simple tu? Hata kwenye maisha ya kawaida hii ipo sana.
 
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Nilikwambia mimi

πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ ni shida bro πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

Tumejaribu kumsaidia japo kidogo maana yeye kasema ni wa kizazi cha mbele yetu na bado ana attitude ile ya mtu akiambiwa kitu asichokipenda, hukimbilia kusema tunamwonea wivu kwa kuwa ametuzidi mahala fulani. Tuache aamue mwenyewe kupokea au kutupa kile tulichompa. πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Ni kwanin nyie mfanye uhuni Enzi zenu harafu watoto WA sasa wakifanya uhuni ionekana kosa kubwa ?

Kwanin nyie mshinde makombe yenu yote Bila FFP ,na mlikuwa mnatumia pesa Bila kupigwa ...

Wivu ,wivu ,wivu .....Hakuna kingine mkuu huo ndio ukweli .......

Uhuni mliokuwa mnatumia zamani city kawazidi saizi mnaanza kutoa mayowe....
 
Weewe ndiye una wivu kuwa sisi tuliweza kujiendesha kwa pesa za ndani huku nyie mlishindwa kujiendesha kwa pesa za ndani mpaka mbebwe na sugar daddy mwenye pesa zake. Sisi tulifanya kihalali. Nyie mmefanya kihuni. Unatulazimishia uhuni ambao sisi hatukufanya kisa nyie mlishindwa kufanya kihalali.

Hata hivyo, isiwe taabu. Kwa sasa umeona akina Livakuku na sisi tumeamka na tumeanza kuwapelekea moto kwenye hizi mbio. Muda si mrefu tutawapita na kuwarudisha matopeni mlikokota pamoja na uhuni wenu. Hatutakuwa na haja ya kugombana mambo ya nje ya uwanjani maana huko huko uwanjani mtakuwa mnaona moto wetu.
 
Umeshinda makombe yote Bila FFP ,var ,goal line technology,Hakuna hata social media ....kiufupi makombe yenu mmeyanyanyua gizani ......

Harafu unasema Ni Halali ....Ni board gani inawezadhibitisha uhalali wenu kuwa mlikuwa mnatumia pesa kihalali ....

Ndio maana mpira WA sasa unawashinda ,Kwa sababu mlikiwa mshazoea kuwin game pekee yenu sababu mnapesa Enzi hizoo ,saizi timu kibao Duniani zina pesa ......leta timu uwanjani tupishane na kuoneshana ubabe tu ...
 
sawa sawa, tukutane uwanjani tuonyeshane ubabe
πŸ˜€ πŸ˜€
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…