Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tupo pamoja wakuu, mie ndio nimejiunga hapa ,vipi game?

Game poa tu, mtanatoka droo leo...we kijana nakutafutaaa sanaa..ndo nn jana kuondoka na chupa za Bia kwa asira afy chicharito kusawazisha pale Rose Garden?..jana wale ma barmaid wamenivua kadet yangu.
 
Dah......

Ndio uwezo wetu msimu huu ndugu yangu tufanyaje.

Sema nimeshajiandaa msimu huu na naona powa tu kwa kutegemea kwamba matokeo mabaya ya msimu huu utaleta mabadiliko makubwa sanaaaa mwakani.

Tulikuwa tunahitaji msimu mbovu mmoja kuleta mapinduzi na huu ndio msimu mbovu ambao washabiki watachachamaa na kutuma ujumbe mzito sana kwa boarda. Na inawezekana mwakani tukianza msimu share zote zitakuwa zinamilikiwa na Kroenke.

Kwahio msimu huu tuvumilie tu wakuu mie kuna mchizi wangu mshabiki wa Wigan kanipa darasa zuri tu. Jinsi ya kukabiliana na matokeo ya ajabu ajabu kila siku. Kwahio presha haipo kabisa.
 
Jumapili leo mkuu , mechi imekuja mapema kidogo ndio nimeingia hapa naona 1-1.

Nataka kupata hali ya mchezo kutoka kwa ndugu zangu Katavi,Quesst. Na Viper.wakuu nipeni kidogo hali mchezo vipi kipindi cha kwanza?
Umaliziaji ni tatizo hasa dk zile za mwanzo. Lakini jamaa waliposawazisha arsenal walipoteana na kila mtu akawa anacheza anavyojua. Labda watabadilika kipindi cha pili!
 
Game poa tu, mtanatoka droo leo...we kijana nakutafutaaa sanaa..ndo nn jana kuondoka na chupa za Bia kwa asira afy chicharito kusawazisha pale Rose Garden?..jana wale ma barmaid wamenivua kadet yangu.

Hapa bado nina hangover , game ndio imenifanya ni niamke tu.

Nyie teseni tu vijana wa manchester lakini mkija emirates ni kichapo tu.
 
Aise game nzuri, goli la Larson hata angekua kipa gani, asingeokoa.

Ushindi upo. Ila vijana itabidi wafanye kazi ya ziada kidogo
 
Umaliziaji ni tatizo hasa dk zile za mwanzo. Lakini jamaa waliposawazisha arsenal walipoteana na kila mtu akawa anacheza anavyojua. Labda watabadilika kipindi cha pili!

Hilo ndio tatizo msimu huu na Wenger hana njia nyingine ya kubadilisha hali hio. Anaogopa kujaribu wachezaji kama Park au chamberlain.hata kuwaleta kipindi cha pili kuleta madiliko anaogopa yeye anaangalia tu meli inazama.
 
Gibbs nje kaingia Santos.

Dogo injury zimezidi.kule kushoto tulitakiwa tusajili kifaa kama Baines wa Everton.Jamaa atatutoa sana kama Wenger atamleta. Gibbs awe anacheza left wing na kukava kama mtu akiumia namba tatu.

Huyo Santos namuona mzito sana kwa maoni yangu.
 
Dakina ya 60 wenger hana mabadiliko ya kuja kushinda game anaaangalia tu mpaka dakika za mwisho ndio anafanya mabadiliko tunajikuta tunatoa draw au kupoteza
 
Back
Top Bottom