Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Ukitaka kumkaba kama mshambuliaji unamkuta zake anacheza kiungo ,mkishambulia unamkuta zake anacheza beki, tukiwashambulia unakuta anacheza mshambuliaji Tena anafika wa kwanza kutupia kamba...

King Kai
View attachment 2956276
Daaaah kulaalekiii
.Mkuu unajua kuwakera. Hapo baada ya kusoma yamevimba uso kwa hasira
 
Ndio uhalisia ,jamaa ameongeza sana kitu kwenye defence

Kai sio abiria uwanjani


Arsenal mule kukiwa na mchezaji abiria tu hata mmoja Kuna kitu utaona hakipo sawa
Miaka kadhaa kuna game City walitupiga. De Bruyne akasema forward line yetu (Auba, Ozil, Martinelli na Laca) Martinelli pekee, ndo alikuwa anasaidia kurudi nyuma na kukaba. Tena hapo Martinelli bado dogo kabisa.

Look how Arteta turned the table!Kule mbele ni mwendo wa pressing tuu. Odegard mda wote anakimbia.
 
Based on stats and form wa kwanza favorite kuchukua CL ni City anakuja Madrid kisha Arsenal.

City na Madrid watafutana. Arsenal tukimanage kutoboa hii robo means sisi tunakua wa pili kama favorites wa kombe. Hizo ni stats tu uhalisia ukoje?

Uhalisia kwangu mimi ni kwamba Arsenal tunaweza kumfunga yeyote kwa hapo quarter lakini sisi pia tunaweza kufungwa na yeyote. Lakini nitashangaa kufungwa na PSG na Barca kwakua PSG wana fallout na Mbappe wana talents lakini ni talents zinazocheza ligi ambayo PSG anatarajiwa kuchukua kila kombe na kila talent iliyopo Ligue 1, their best season wakafika final CL ila walichocheza ilikua kama utani.

Barca naamini transition yao kuna mahali imekwama, haijakamilika wanamuondoa kocha. Wana youngsters wanawahype, alikuepo Fati, hype kubwa kuliko wa sasa muda ukasema. So naamini hizi ndiyo timu ambazo sisi tutashinda bila maelezo.
 
Yaa
Nadhani uko sahihi pia. Tunabebana. Nataka mengi zaidi kutoka kwa Kai. Na siku hizi nawadai zaidi Martinelli, Saka, Trossard, Jesus na Odegaard. Naamini wako gia #3 na wanaweza kwenda #4 na #5.
Yaani yule kai angekuwa na miguu ya trossard tu, angekuwa hatari mnoo, kai kapoa saana, kai akiwa na mpira hayupo direct sana kwenye goli, mali ndain ya box ana turn analipa goli mgongo.
 
Yaa

Yaani yule kai angekuwa na miguu ya trossard tu, angekuwa hatari mnoo, kai kapoa saana, kai akiwa na mpira hayupo direct sana kwenye goli, mali ndain ya box ana turn analipa goli mgongo.
Miguu ya Jesus tu.

Kuna kitu kimoja, inatarajiwa mtu mfupi mikimbio yake inakua ya mkupuo kuliko mrefu. Mfano waliwahi tabiri mikimbio ya Martinelli itaathirika baada ya kuongezeka urefu ila imekua tofauti.

Tuje kwa Kai.

Wakati yupo Ujerumani hakua mrefu sana, ilimwezesha kunyumbulika kwa urahisi na kufanya runs za msingi zilizofanya awe hatari mpaka kenge wakamtamani wakampeleka darajani. Urefu kaanza kuupatia pale hivyo runs na unyumbulikaji ukapungua, plus uchezaji wa Kenge ukazidi kumfanya awe isolated.

Arsenal tumemchukua Kai, ana miaka 24, ana chansi ya kurefuka zaidi. Kuna picha moja yupo na Mertesacker gunners wa Reddit akasema sasa hapa ndiyo naelewa Kai ni mrefu kiasi gani. Per ni giant ana 6'6 lakini kamuacha Kai points 2 tu.

This means urefu wa Kai ni ishu kwenye acceleration na ishu kwenye unyumbulikaji, nafikiri ndiyo maana hata headers siyo mzuri ingawa ni mrefu.

Jana baada ya kutoa pasi kwa Trossard aliyekua anakimbia kumpa msaada Trossard nadhani ni Martin. Urefu wake unamzuia kuaccelerate fasta na kunyumbulika bila kumshtukia tofauti na Leandro, Martin, Partey, Jesus, Saka na wengine.

Haya ni maoni yangu
 
Kama kai ana 6.4 maana yake katifautiana na thierry henry kwa 0.2 maana henry ni 6.2 nafikiri, lakini ilikuwa tofauti unyumbulikaji mpaka mwendo.

Kuhusu kichwa ni afanyie mazoezi, ni idara ambayo inabadilika kwa mazoezi.
Inawezekana akapewa kocha maalum akampa hints mbili 3 namnagani ya kuwa mshambuliaji hatari akiwa na mpira na akaongezeka kiwango.
Kai si mchezaji ambae unamfurahia akiwa na mpira, ni anacheza ile basic ya mpira hana nyongeza hata kidogo.
 
Arsenal tumemchukua Kai, ana miaka 24, ana chansi ya kurefuka zaidi. Kuna picha moja yupo na Mertesacker gunners wa Reddit akasema sasa hapa ndiyo naelewa Kai ni mrefu kiasi gani. Per ni giant ana 6'6 lakini kamuacha Kai points 2 tu.
Point of correction.. hapo kwenye kurefuka, mtu anamaliza kurefuka anapofikia umri wa miaka 18 kwa mwanaume, kwa mwanamke may be earlier than that
 
sidhani kama urefu ni ishu sana kwenye suala la acceleration.. usain bolt kamzidi kai urefu ila ni fastest athlete.

mchezaji kunyumbulika mara nyingi inakuja na kipaji.. kanu alikuwa mrefu ila wote tuliona uwezo wake.
 
sidhani kama urefu ni ishu sana kwenye suala la acceleration.. usain bolt kamzidi kai urefu ila ni fastest athlete.

mchezaji kunyumbulika mara nyingi inakuja na kipaji.. kanu alikuwa mrefu ila wote tuliona uwezo wake.
Kila general rule ina exception.

Pengine Kanu na Usain ni exceptions
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…