Habari za kusikitisha kwamba Wilshere atakuwa nje hadi mitaa ya x-mas, naona ndio yaleyale ya TV5 msimu uliopita, tunaweza kumkosa pengine karibia msimu wote.
Wenger nahisi siku zake sasa zinahesabika, yote amejitakia mwenyewe na MAAMUZI yake mabovu. Msimu uliopita ilikuwa kama angesajili replacement ya uhakika kwa TV5 kwenye dirisha dogo la January na tulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda EPL na FA cup matokeo yake alikumbatia hela wakati akijua TV5 atakuwa nje hadi mwisho wa msimu.
Sasa msimu huu alijua Cesc anaondoka na asilimia kubwa Nasri atafuata, yeye ameenda kuzembea kusajili hadi dakika za mwisho.
Wilshere aliumia pre-season na hakika mafundi walijuwa atakaa nje muda mrefu, kwa nini Wenger haku-react mapema?
Kibarua chetu kimezidi uzito sasa kwa sababu hapa idara ya Viungo ambapo ndio mapishi yetu yote yanafanyika tumeumia vibaya. Midfield quarterer ya Song- Nasri - Cesc - Wilshere imekufa kabisa na amebaki Song pekee. Arteta ni mzuri lakini inabidi afanye kazi na watoto ambao hawana uzoefu Charmbelain na Frimpong, kwa kweli (Arsene) tunapenda kubahatisha mno.
Wenger amejichimbia kaburi mwenyewe kwa MAAMUZI yake mabovu. Tukipoteza mechi 2 tu zaidi itatuwia vigumu kucheza kwenye Champions league msimu ujao kwa sababu sifikiri ManU, Man City au Chelsea watapoteza mechi zaidi ya 3 na Liverpool na Spurs hawatopoteza mechi nyingi kwa vile vikosi vyao havijaathirika sana.
Tukikosa nafasi ya CL sidhani kama kibarua cha Wenger kitakuwa salama.