Arsenal (The Gunners) | Special Thread

✍🏻Control spaces , shinda mipambano yako , fanya runs nzuri , kuwa sharp uwanjani ni vitu ambavyo wamefanya kwa usahihi sana dhidi ya Newcastle leo na kuwafanya vijana wa Eddie Howe kucheza mdundo wao

✍🏻Distance : Hii kitu muhimu sana , jinsi Arsenal walivyohakikisha distance kutoka mstari mmoja mpaka mwingine na mchezaji kwa mchezaji kuwa ndogo sana , faida yake ?

1: Iliwanyima muda na nafasi kwenye mpira Newcastle na kushindwa kupita ndani . Matokeo yake wakalazimishwa kufanya makosa au kupiga mipira mirefu ambayo Arsenal ilikuwa rahisi kwao

2: Inasaidia sana kufanya pressinf nzuri haraka pale walipokuwa wanapoteza mpira

3: Inasaidia ku control mechi kwasababu inakupa options za pasi ambazo sio za umbali mrefu hivyo mpira kutembea vizuri

✍🏻Yes najua kuna namna makocha wanasisitiza timu kuanza nyuma lakini kama pasi haipo kwanini usianze mipira mirefu kwa mawinga halafu uanzie hapo ? Newcastle mara kadhaa walijipiga risasi mguuni kwa risk pasi zao hasa ukizingatia Arsenal walikuwa sharp sana

✍🏻Arsenal waliwaonesha Newcastle sura yao ya pili kwamba nini wanaweza kufanya wakiamua kukabia chini ... compact 4-4-2 ambayo inafunga spaces , ndani hakuna njia , Newcastle walipata tabu sana kuwafungua Arsenal hasa kwa kutumia ile silaha yao ya combination play ( Bruno - Trippier - Almiron )

NOTE

1: Jorginho ali control sana mchezo hasa kipindi cha kwanza , simple passing na humuoni akiliacha eneo lake tupu

2: Arsenal kwenye mipira iliyokufa 🔥 hakika Nicolas Jover anafanya kazi vizuri

3: Leo Arsenal walikuwa wanacheza kama vile wana hasira na Newcastle , mbinyo huo 🔥😀

4: Sifa ya Newcastle ya msimu uliopita ya kuzuia vizuri msimu huu imepotea ... wameruhusu magoli 4 mechi kadhaa mpaka sasa

5: Bukayo Saka sasa hivi ukijaa tu kwenye mfumo unaokota kambani

6: Licha ya kurusu magoli 4 lakini performance ya Karius huwezi amini kama alikuwa hachezi 🤝

7: Mbio za ubingwa bado za moto sana

FT: Arsenal 4-1 Newcastle

 
Tunaomba radhi ndugu zetu leo kumekuwa na goli chache🤠🤠...tunaahidi tutalitatua hili tatizo mechi ijayo...asante kwa kuwa nasi usiku wa leo tukisheherekea kilele cha Tetaball
Mmefanya vizuri kutuomba radhi. Hatujafurahishwa kabisa na kitendo cha kuwapiga wale mijusi milia 4-1 badala ya 5-0, 6-0 na kuendelea.

Inakasirisha sana kuona tumepiga mtu 6-0, mwingine 5-0, halafu hiki kimjusi tunakipiga 4-1. Hii inamaana kiwango chetu kinashuka na tusipokuwa makini tutakuwa kama manyumbu.

Kurekebisha hili, Sheffield anatakiwa apigwe kuanzia 7-0 na kuendelea pale kwake ili mahesabu yetu yakae sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…