Nilimaanisha kumuuza mapema akiwa anahitajika na timu zingine. Najua bado dogo ana 16, sasa sijajua kama atarefuka sana zaidi ya hapo ndani ya miaka 2-3. Nia ni ili tumsahau mazima tufocus na wachezaji wenye miili mikubwa, watakaoweza kustahimili mikiki mikiki ya ligi.
Wachezaji wenye miili midogo kama Wilshere, Carlos Vela, Fabio Vieira, kwa kiasi fulani hata Cedric, wanakuwa targetted sana. Wengine wanajikuta majeruhi mara kwa mara. Kusurvive baadhi ya wachezaji walibidi wawe tough kiasi na skills nyingi, kama Mtakatifu Cazorla.
Nilikuwa na wasiwasi wa hivi kwa Saka pia alivyoanza, ila jamaa sasa amejijenga physically na amerefuka kiasi.