.
Umewahi kuona ile Traffic anaita magari ya upande mmoja tu ? Basi ndio kilichotokea leo pale London Stadium , Arsenal utasema wapo tizi vile , mpira unatembea , movements tamu sana , pasi za uhakika , halafu umaliziaji mzuri ( imagine zinapigwa shots takribani 25 ) .!
Hii ni aina ya mechi ambayo David Moyes atataka kuisahau haraka sana na vijana wake , maana walitawaliwa kila eneo kwa kila kitu , hawakumpa tabu hata David Raya . Hiki ni kitu ambacho Arsenal anaweza kukufanyia ukiingia kichwa kichwa .
Position na majukumu ya Trossard yaliwapa tabu sana Zouma na Aguerd , kama beki wa kati unatamani ukabiliane na mshambuliaji ambaye mtakuwa mnagusana lakini Trossard hakuwapa hiyo nafasi , alikuwa anacheza zaidi mbele yao na nyuma ya kiungo cha West Ham na kuwalazimisha mabeki wa kati wa West Ham waanze kukabia juu na ndio sherehe iliponoga hapo
Baada ya hapo ilikuwa ni ishu ya kwamba Arsenal watafunga mangapi na muda gani .!
NOTE
1: Kocha wa mipira iliyokufa wa Arsenal anatumia mshahara wake vizuri sana . Arsenal wazuri mabox yote . Wanazuia vizuri na wana madhara wakija kwako
2: Mashabiki wa West Ham wamemzomeaaaaa Rice halafu baadae ikabidi wampigie makofi tu hakuna namna
3: StarBoy Saka msimu uliopita alipiga 10+ goals na msimu huu tayari 10 goals zimefika na bado mechi kama 14
4: Kuna kitu nimeona kwa wachezaji wawili wa Arsenal na nimekipenda sana licha ya kwamba leo hawatoimbwa ... White na Havertz : White kwenye kona lazima afanye blocking kwa Kipa , na Kai pale West Ham wakianza mipira mirefu kutoka nyuma utamuona karibu na Rice kusaidia
small details
5: Kudus , Bowen na Paqueta ( bado majeruhi ) , West Ham wafanye kazi sana kubaki nao hao .!
6: Hizo mbio za ubingwa mpaka kieleweke
FT: West Ham 0-6 Arsenal
AMBANGILE