.
[emoji1593]Umewahi kuona ile Traffic anaita magari ya upande mmoja tu ? Basi ndio kilichotokea leo pale London Stadium , Arsenal utasema wapo tizi vile , mpira unatembea , movements tamu sana , pasi za uhakika , halafu umaliziaji mzuri ( imagine zinapigwa shots takribani 25 ) .!
[emoji1593]Hii ni aina ya mechi ambayo David Moyes atataka kuisahau haraka sana na vijana wake , maana walitawaliwa kila eneo kwa kila kitu , hawakumpa tabu hata David Raya . Hiki ni kitu ambacho Arsenal anaweza kukufanyia ukiingia kichwa kichwa .
[emoji1593]Position na majukumu ya Trossard yaliwapa tabu sana Zouma na Aguerd , kama beki wa kati unatamani ukabiliane na mshambuliaji ambaye mtakuwa mnagusana lakini Trossard hakuwapa hiyo nafasi , alikuwa anacheza zaidi mbele yao na nyuma ya kiungo cha West Ham na kuwalazimisha mabeki wa kati wa West Ham waanze kukabia juu na ndio sherehe iliponoga hapo
[emoji1593]Baada ya hapo ilikuwa ni ishu ya kwamba Arsenal watafunga mangapi na muda gani .!
NOTE
1: Kocha wa mipira iliyokufa wa Arsenal anatumia mshahara wake vizuri sana . Arsenal wazuri mabox yote . Wanazuia vizuri na wana madhara wakija kwako
2: Mashabiki wa West Ham wamemzomeaaaaa Rice halafu baadae ikabidi wampigie makofi tu hakuna namna
3: StarBoy Saka msimu uliopita alipiga 10+ goals na msimu huu tayari 10 goals zimefika na bado mechi kama 14
4: Kuna kitu nimeona kwa wachezaji wawili wa Arsenal na nimekipenda sana licha ya kwamba leo hawatoimbwa ... White na Havertz : White kwenye kona lazima afanye blocking kwa Kipa , na Kai pale West Ham wakianza mipira mirefu kutoka nyuma utamuona karibu na Rice kusaidia [emoji91][emoji91] small details
5: Kudus , Bowen na Paqueta ( bado majeruhi ) , West Ham wafanye kazi sana kubaki nao hao .!
6: Hizo mbio za ubingwa mpaka kieleweke
FT: West Ham 0-6 Arsenal
AMBANGILE