.
Listen .! Najua kazi ya namba 9 / straika ni kuweka mpira wavuni ( na katika timu kubwa ndio rada inakuwa kubwa sana kwako kufunga mara kwa mara ) ... So Yes najua hilo ni eneo ambalo Gabriel Jesus anatakiwa kuboresha ( ana miaka 26 sasa )
But kuna vitu anafanya uwanjani ... vinakunyanyua kwenye siti yako au vinakuacha mdomo wazi na pengine Arsenal wanahitaji namba 9 mwingine ili Jesus atumike eneo lingine la uwanja ( Kulia au kushoto pembeni )
1: Dribbling ( mpira unakuwa karibu sana na kiatu chake sio chumba kizima
)
2: Workrate yake akiwa uwanjani ( anakupa 100%)
3: Uwezo wake wa kuvuruga muundo wa ulinzi wa timu pinzani ( destabilization) kwa :- Movements, Flicks , Dribbling , Pace
4: Kuna hii ambayo naamini wengi wanachukulia poa , Jesus ana uimara mzuri wa kimwili kukabiliana na challenges / mipambano ( duels ) dhidi ya mpinzani wake
Kiufupi General Play yake ipo katika level nzuri sana ngumu kuifumbia macho :
VITU AMBAVYO VIPO HASI KWAKE
1: Majeraha
2: Umaliziaji wake sio wa ufanisi sana akipata nafasi
NOTE
Leo najua mashabiki wengi wa Arsenal watakuwa wanadumisha undugu wa jiji moja la London na Chelsea
Baada ya wao jana kuwafundisha Man United jinsi gani ya kumfunga Notts Forest katika uwanja wao .!
Ila yule AWONIYI , Arsenal mkae chini mmalize tofauti zenu . Ameshafanya kuwafunga Arsenal kama kitu cha kawaida , halafu kumuweka Saliba pembeni vile na kuuwa mali chini na kutumbukiza kambani ndio tabia gani ile ?
AMBANGILE