Kuna aina tofauti ya kushabikia timu pale unapojua unakutana na mpinzani gani. Nitajaribu kuelezea mbili ambazo ni rahisi kwangu:
Moja ni kuona umekutana na mpinzani ambaye unadhani ni mgumu kwako na hutaweza kumshinda isipo kwa bahati. Huyo unaweza kusema huna matumaini ya kupita hivyo unajihesabia ushapiwa. Au utasema 'lolote laweza kutokea' au kiubishi utasema 'huyu nampiga'. Hii ni mara chache. Zingatia ile miaka tunakutana na Bayern au Barcelona na tukawa tunaona hawa watatushinda. Bado kuna mechi tuliwashinda ila kwa game zote mbili tulijikuta tunaondolewa kwenye mashindano.
Ya pili ni kuona umekutana na mpinzani ambaye unadhani huyo umemzidi na unahesabu kuwa kwenye mechi mbili wewe utaibuka kidedea. Of course inaweza kutokea akakupiga. Hii ni football na underdog kumpiga top dog ni jambo la kawaida ila ukiona tu kuwa umempata huyu underdog, unatembea kifua mbele. Kwa historia yetu na Porto, wao ni watoto wadogo kwetu hivyo tunaongea kama tutawapiga. Hatujaweka factors kama hatujacheza champions league zaidi ya miaka sita na vikosi tunavyoviongelea sasa ni tofauti kabisa, walimu tofaouti kabisa bali kihistoria tu.
Ndiyo maana ni rahisi sana kuona kwa nini
hamis77 ameshanunua tiketi yake ya kwenda kucheki robo fainali, kwa sababu anaona hapo kwa Porto hatuwezi kuzuiwa. Hamaanishi hatuwezi kufungwa, ila sababu za kutufanya tuamini tutashinda zina nguvu zaidi ya sababu za kutufanya tuamini tutapigwa.