Arsenal (The Gunners) | Special Thread

kwa umoja wetu mashabiki wote wa Epl tunatakiwa tuwe humu tunawapiga spana 24/7 hawa wajaa laana.
Kwanza hii sio timu ni kikundi tu cha wauza karanga.
Na kwli kabisa ikifika February wte mtaungana kwny majukwaa yenu kutuombea njaa....maana tutakuwa tushafungua gepu la point pale juu🤠🤠🤠....tunza hii comment
 
Ze hadi wei mniga analiwa na mamba,
Enzi hizo marehemu lufufu kwenye ubora wake..
Dame wawili
Dame na tompoo
Komando kipensi
Anodi ya jeni
Anoni ya jini
Kipanya msosi.
Etc. 🤣😂
 
kwa umoja wetu mashabiki wote wa Epl tunatakiwa tuwe humu tunawapiga spana 24/7 hawa wajaa laana.
Kwanza hii sio timu ni kikundi tu cha wauza karanga.
Wewe siumeburuza mkia kule UCL mbele ya Copenhagen?
 
Wewe siumeburuza mkia kule UCL mbele ya Copenhagen?
Ni bora kuburuza mkia ukajijua mapema kua hauko sawa kuliko kuongoza ligi kwa siku 258 ukajipa false hope ya ubingwa halafu zimebaki mechi 4 ligi iishe ukalegeza kalio ukaishia kuwaona wenzio wananyanyua makwapa
 
Ila Mkuu Flano Unajua kusimanga watu, mbaya zaidi unakuja kutusimangia kwenye Jukwaa letu kabisa utasema umetumwa.

Kwa taarifa yako mwaka hu tunabeba kuanzia Epl na Uefa kabisa
 
Ila Mkuu Flano Unajua kusimanga watu, mbaya zaidi unakuja kutusimangia kwenye Jukwaa letu kabisa utasema umetumwa.

Kwa taarifa yako mwaka hu tunabeba kuanzia Epl na Uefa kabisa
we jidanganye tu kwa kusikiliza false hopes za Masingeli halafu mwisho wa msimu uje kuporomosha matusi humu kama wenzako hawa hapa

Mimi hua na screenshots halafu nawahifadhia kumbukumbu zenu maana nawajua vizuri arsenyau nyinyi huwa mnasahau haraka sana.
 
Mkuu kwa ushahidi huo wa screen shots sina ujanja wa kubishana na wewe, ndiyo maana unatusimanga kutwa kucha.

Ila mwaka huu lazima tubebe hivyo Vikombe maana mbabe wetu City ameshatema Bungo na kutukabidhi mbizo za Ubingwa Arsenal
 
Hapa duniani timu ninayoipenda kuliko zote ni Arsenal FC ikifuatiwa na Simba SC na national teams za Tanzania na France.

Lakini niseme wazi kwamba kwa jinsi Arsenal inavyocheza mpira slow basi hatutakuja kamwe kubeba makombe makubwa.

Aina ya mpira wetu ungeweza kuwa hatari sana kama tungecheza kwa kasi. Kucheza taratibu hivi kunataka uwepo wa wachezaji exceptional ili kuweza kubeba makombe.

Barcelona iliweza kubeba makombe kwasababu walikuwa na Messi, Xavi na Iniesta, pia Puyol, Alves, Bosquet, Pique, Villa etc. Mara kadhaa walicheza kwa kasi na kupiga counter lakini mostly walitegemea hao wachezaji hatari.

Sasa hapa kwetu Arsenal kuna wachezaji sita ambao angalau wana winning mentality ni Rice, Saliba, Martinelli, Trossard, Partey na Saka. Na hawa wote ukiondoa Saliba na Rice ni normal players, sio exceptional.

Wachezaji ambao nawaona ni squad players na watakupa output ya kueleweka mostly kwenye mechi ndogo ni Odegaard, Magalhaes, White, Zinchenko, Tomiyasu na Gabriel Jesus. Nawapa muda Kiwior na Raya.

Wachezaji mizigo ni Elneny, Nelson, Havertz, Vieira, Nketiah, Rowe, Ramsdale na Soares. Hawa waondolewe haraka maana hawana faida yoyote. Akina Lokonga na Marquinhos waliopo mkopo wasirudi.

Kwahiyo katika hali hii nategemea Arsenal tutatolewa UCL kwenye robo fainali na tutaingia top 4 ya EPL kwa tabu sana. Tutatolewa FA siku chache zijazo.

Mwezi huu wa December tunaweza kupata point chache sana maana tumeshapoteza kwa aston villa na hapo bado broghton, liverpool, westham na fulham.

January apatikane beki wa kati, winga wa kulia na mshambuliaji hatari ili angalau kuokoa jahazi lisizame kuanzia February 2024.

Arteta na Edu waache kuleta wachezaji laini na waache huu mpira slow slow.
 

Too pessimistic, Tuombe majeruhi wapone and no new long time injury; tunayo timu ya kupambana.
Hakuna timu duniani haifungiki
 
Sikuwa active huu muda....aisee ilikuwa ni mitusi mikubwa kwlikwli....mpira unafanya watu wanatoa maneno mazito hv🤠🤠🤠...kwli sisi wengine hatuipendi timu kihivyo maana tukifungwa nakuwa very optimistic ila kuna waungwana wanaumia kwlikwli....poleni sana mlioumizwa na madhila ya mwaka jana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…