Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Haya mmeshaanza kuota angalia usiyamwage kitandani, hivi mnafikiri Arteta anao uwezo wa kuwafikisha popote?
Wewe Migos , Timu yako ipo nafasi ya 12 ,soon wanaipeleka nafasi ya 17


Nachelea kusema Chelsea imesharudi ilipotoka

Wakati nakua ,Chelsea ilikuwa inashika nafasi za 7-17

Ndio nafasi inazoshika Sasa,


Naweza kusema mmeshakuwa kama Northgham forest
 
Wiki hii wanacheza na nani Hawa🤓🤓🤓...tutabiri tena matokeo yao
 
Ivan Toney:
Football.london wanasema sheria zinatubana kumpata kwa mkopo january kwa sababu hairuhusiwi kwa timu moja kuchukua zaidi ya mchezaji mmoja kutoka timu moja.
Tayari tuna David Raya kutoka Brentford.
Kama tunamtaka Toney January:
1. Tunamnunua mazima na siyo kwa mkopo.
2. Tunatumia mapema ile 'option to buy' ya Raya na kumnunua mazima. Hivyo tunakuwa na mchezaji mmoja tu kwa mkopo kutoka Brentford.
 
Kuna mawili au matatu yanaweza kutokea...kama wanamtaka kwli maana yake watamnunua Raya January Ili wampate Toney kwa mkopo....au labda kuna CF mwingine watamchukua then waachane na Toney....au nnavyowajua Arsenal wanaweza kuachana naye January wakatafuta kiungo halafu dirisha kubwa la usajili wakamrudia kutokana na kiwango atakachokionesha atakavyorudi
 
Arsenal mkimpata Toney nitaanza kuwachukulia serious sasa.
 
Tuone tutaamua nini. Tutahitaji mtu wa ziada iwapo tutampoteza Jesus au Nketiah au wote kwa majeraha. Toney naye anaweza akahitaji mechi kadhaa kurudi katika ubora wake
 
Very true
 
Inaweza kua kama ishu Caicedo tusimrudie tena dirisha kubwa, maana Arteta hasomeki uyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…