Arsenal inajulikana kuwa ina tatizo ndani ya suluhu na suluhu ndani ya tatizo. Ila rafiki yetu naona analileta hilo suala kama vile kwetu ni tatizo kubwa sana au kama linatuathiri zaidi ya kiasi, wakati siyo hivyo. Tunakuwa maeneo ya juu kwenye goal difference ila siyo kuongoza goal difference (Unaweza kuta tutapitwa na timu 1-3). Unakuta tumefunga magoli mengi lakini wachezaji wetu hawafikishi hata magoli 20 kila mmoja, huku timu za chini yetu zinawachezaji wenye magoli zaidi ya wakwetu. Lakini hizo timu hazifungi magoli mengi kuliko sisi. Tumeshawahi kuwa na Aubameyang aliyehinda kiatu na Mane na Salah ila tuliishia wapi?
Hatusemi hatutaki wafungaji wa magoli 20+, of course tunataka na kila siku unasikia tunahusishwa nao. Ila ni wazi pia kuwa kumetengenezwa mfumo wa kufanya tufunge mengi na kushinda zaidi ya hao wenye 20+ goal strikers ila tunajua bado haitoshi. Nadhani Nketiah labda na Saka kama ikosei ndiyo wana hat-trick kwetu, ila kuna timu zimepiwa 5-0, 6-0. Lens alipiwa 6-0 hapa juzi juzi na tulikuwa na wafungaji 6, yaani nusu ya timu imefunga. Tunataka tufunge zaidi kwa system hii hii, kwa kuboresha wafungaji na system. Inawezekena yeye hajaelewa hili. Ndiyo maana hata watu walimuuliza nani anamtaka Wilson ama Isak? Na akaambiwa kuwa kiukweli hao jamaa wakija Arsenal wakimkuta Jesus yuko fit, hawamuweki bench. Mfumo. Theory yetu ni kwamba Arteta atakuwa radhi akomae kuboresha ufungaji wa Jesus kuliko kumweka bench kwa Isak au Wilson.