Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Daaah unanikumbusha mbali sana
Naandika, nafuta. Naandika tena nafuta. Nina vingi Sana vya kuelezea kuhusu mpira

Tukio langu ambalo sitalisahau. Ilikua tanga muheza nilienda likizo kwa bro kipindi hiko nipo form six
Sasa mtaani pale kulikua na timu alafu kulikua na mashindano ya kombe limedhaminiwa na mbunge

Nikawa kwenye mazoezi naenda kupiga nao tiz, siku kwenye mechi naenda na mm kuangalia (pale pale muheza Mjini) uwanja upo karibu na hospital

Siku ambayo chama langu lipo uwanjani, Kama kawaida tukawasili uwanjani (hapo Mimi Kama mbeba maji ya wachezaji)

Mpira ulikua mkali Sana siku ile(tanga Wana vipaji Sana
)
Dakika ya 70 wachezaji wetu wawil waliumia namba nane na winger, sub moja ya winger ikapatikana
Ila huyu kiungo wachezaji walikua hawaiwez ile namba sijui ata sielewi

Mara kocha akaniita oya MKOREA vaa jezi kwasababu hauna tiz, kacheze namba 10. Namba kumi aje nane
chamsingi saidi kukaba tu.
Kumbuka Hadi hapo timu tulikua tunacheza nao ya kutokea amani/amana tupo moja moja

Nikaingia, kabumbu likaanza. kupiga One two one two Sana tu
Sasa damu ikachemka nasambaza upendo tu, zikitokea faulo au Kona huwa nakaa area ambazo mpira uki-bounce zile dead balls zinanikuta

Sasa Kuna Kona ilikua tunapiga dakika za lala salama, Mimi nikaka nje ya box. Ule mpira kipa aliutema huku yeye mwenyewe akaangua ukanikuta nipo on move
Ilisikika sauti moja tu 'misssssss' nilikandamiza shuti kimoja Cha mbuzi na kipa alikua ameanguka ule mpira ulipita kama upepo
Ubao unasoma 2-1
Mpira umeisha kocha ananiuliza ndio wewe au? Mbona haukusema mkorea

.
.
Kwenye mpira huwa nacheza namba nane, nikipatiwa namba sita mzuri kwenye kukaba na winger zinazotembea unaweza ukasema pirlo ana mdogo wake huku bongo
Pia napenda Sana kupiga, zile za Steve Gerald
Sehemu kubwa ya mpira nimecheza kishule shule zaidi, hizi zamchangani sijui ndondo nilikua zisikubali kabisa
Na ata nilivyokua mdogo, nyumbani wakisikia nimecheza mpira tena maeneo ya mbali ni msala, Yani nilizaliwa ili nisome kwaio nachangiwa na watu wawili mke na mume wake kwenye kupigwa


Kuna siku nilishuhudia pale kajiungeni Kama unaenda chanika mtu anavunjika mguu Kama kuni hivi kwa rafu ya makusudi kabisa. I was so sad, kama nimefanya Mimi hivi

Umiseta nilifika Hadi kibaha. Ila Bongo nyoso sana wazee kmmk. Tulioandikwa majina Tukaambiwa tutaitwa/kupigiwa simu. Hadi Sasa nasubilia huko kuitwa
 
Mikel Arteta’s Arsenal so far this season compared to last season…

Decent start, but it’s time to go on a run after the international break. #afcView attachment 2815683
Ile form yasimu uliopita ilikua balaa Sana, kiufupi naona gari bado halijawaka
Majerui ni wengi
Kuna watu nawaambia, Sasa hivi mkimuona arsenal yupo pale mjuu anapigwa na baridi. Basi msahau kushuka chini
 
Ukienda jukwaa la Man utd,liverpool ama Chelsea kidogo hautakutana na majigambo ya matumaini hewa kama yanayotolewa na vijana wa arteta. Sababu wana uzoefu wa kuongoza ligi mara kadhaa na kuishia kupokonywa ubingwa sababu wanaijua EPL sio maneno bali ni kazi kazi hadi dakika za mwisho. Sijui nyie huwa mnaangalia mechi za Arsenal tu ndio maana mnaishia kuandika uongo uongo mwingi humu?
 
Bongo miyeyusho wanapeana nafasi makazini hadi kwenye mpira, mengine hatusemi tutamwaga siri za watu, ila kuna uhuni mwingi saana, nimeishi kwenye soka na wanasoka pia, nayajua haya kwa kuona na kusimuliwa.
 
Katka stori zinazonishangaza kuhusu asenal ndio hizi ngonjera,mara ooo siaraseveni nilimtengenezea jezi namba sita.

Hiyo kesi ya hazad haina tofauti na usajili wa niko pepe, umafia kwenye soka hata aseno walifanya ila vikombe ndio ikawa sio sehemu yake
Mmesikia story ya hazard alitaka kujiunga Arsenal wakati anatoka ligue 1, hapa akaja Abramovich kuhonga €7m kwa agent wake ili kuhijack the deal, Chelsea haya mambo hawajaanza leo, sasa unashangaa nini kwa Mudryk?
Ri
 
Kuna makali fulani tumekosa naona, lakini si mbaya, muda unakwenda tunaimarika.
Arteta msimu huu wameshamsoma, mwaka jana yeye mwenyewe hakutarajia iwe vile,ila msimu huu kama atakosa epl basi ni kutokana na kutoa sare nyingi kuliko siti(bingwa mtarajiwa)

Manisiti kwenye mechi 3 yupo huru kushinda mechi mbili kikamilifu na kufungwa moja kikamilifu,ila asenali kwenye mechi tatu yupo huru kudroo mechi zote au kushinda moja,kufungwa moja na kutoa sare moja.
Nahapo ndio Pep anapowazidi ujanja wengi,hako katabia msimu huu ten hag amekaiga katamsaidia sana😆😆😆

Yuefa breki ya arteta ni namna ya kucheza mitoano hapa bado panamsumbua vibaya sana rejea olympiacos,lisbon zilivyomtoa.
 
Vipi nyie mmeshajikatia tamaa na timu zenu mnaunga mapambio ya kumsifia Guardiola?

Na kummilikisha ubingwa kabla ligi haijaisha?
 
Kwa ushauri tu, Acha kulopoka haitakusaidia.
 
Hapo Kuna positional plays za hatari sana kwa hao wote washambuliaji wanne
Na team Kama hiyo wakielewana inakua hatari sana, coz inakua ngumu kuwafanyia marking
Goli lilivyofungwa ndo maana halisi ya hii comment yako, uliona kitakachokwenda kutokea na ndo kilitokea kwa aslimia 100.

Mkorea kwenye 1 na 2
 
Sisi hatuongei maneno mengi
 
EXCLUSIVE

Everton kakatwa points 10

Wanafata wale wenye vidomo Domo

Wanapoint 15 watakatwa points 12
 
Goli lilivyofungwa ndo maana halisi ya hii comment yako, uliona kitakachokwenda kutokea na ndo kilitokea kwa aslimia 100.

Mkorea kwenye 1 na 2
Mkuu naona ulinielewa vizuri mno


Martinel alivyokua anakuja na mpira akitokea pembeni sehemu ya vini, vini alikua position ya martinel pale Kati
Move ya goal nimeiangalia imechezwa na hao watu wawili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…